Misri na Ugiriki zina mahusiano ya kihistoria na kiutamaduni tena vifungo vya urafiki na ndugu
Imefasiriwa na / Mervat Sakr
Misri na Ugiriki zina mahusiano ya kihistoria, kiutamaduni, urafiki na udugu, nami nachukua fursa ya furaha ya Ugiriki katika maadhimisho yake ya Uhuru; kuwapongeza watu wa Ugiriki na jamii ya Wagiriki, inayoishi kati yetu katika maisha mazuri yanayoonesha mahusiano makubwa ya ndugu baina yetu.
Misri haisahau kile ambacho jamii ya Wagiriki inakifanya katika nyanja zote za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni, na kwa hivyo tunapaswa kuishukuru, na kuipongeza kwa maadhimisho yake ya furaha, na twaomba Mwenyezi Mungu awafanikishe watu rafiki wa Ugirik kueleka ustawi na maendeleo yake.
Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser kwa Wagiriki nchini Misri wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Ugiriki.
Mnamo Machi 25, 1955.