Mapambano Ndiyo Yanayolinda Raia

Mapambano Ndiyo Yanayolinda Raia

Imetafsiriwa na/ Neema Ebrahim 
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled 

Ni jambo la kikawaida kwamba mkutano na Umoja wa Wafanyakazi wa Kiarabu una athari kubwa katika nafsi na kuchochea hisia kubwa. Kuwa Umoja wa Wafanyakazi wa Kiarabu, kama ulikuwa umoja ulio kweli na ufanisi - sio tu muungano ya kimaandishi tu - unaweza kufanya mengi kwa umma la Kiarabu. 

leo, Tabaka la wafanyikazi au wafanyikazi wa Kiarabu wanawakilisha umma wote wa Waarabu, na mfanyakazi leo ana jukumu lake la mapambano, na watu ndio wanaweza kufikisha matarajio yote, na wafanyikazi lazima wawe mstari wa mbele wa watu ili kutimiza matakwa.

Na kila nachotakia ni kwamba Muungano wa Wafanyakazi wa Kiarabu utachukuliwa kama mfano wa kuigizwa  kwa ajili ya maadili na hali ya juu na matumaini wanayahisiwa kwa watu wanaofanya katika umma wote wa kiarabu.

 Ninaposema watu wanaofanya kazi, nakusudia watu hawa wenyewe;  Kwa sababu watu wasiofanya kazi hawawezi kujihisi mwingine na hawawezi kuwa na matumaini, kwa sababu watu wanaofanya kazi wamefikisha matumaini yao na matakwa yao, watu wanaofanya kazi wanaowakilisha wafanyakazi, na kila mtu anayefanya kazi katika umma wote wa Kiarabu ... ni nchi ambazo zina matamanio na Umoja wa Wafanyakazi wa Kiarabu unayoweza kuthibitisha kwamba matakwa yanaweza kuhakikisha umoja wa kimawazo kati ya wafanyakazi wa Kiarabu wanaounga mkono umoja wa kiarabu, Umoja wa kiupambana kati ya wafanyakazi wa Kiarabu - na kuna mifano mingi- husaidia umoja wa kiarabu, Umoja wa kiarabu kwa maana yake kubwa unaweza usiwe umoja wa katiba, lakini ni umoja wa malengo na umoja wa hisia.

Kinyume na hili ni kwamba kila watu wa Kiarabu wametengwa katika nchi yao ya Kiarabu, na hawajali au kuuliza kwa kile kinachotokea katika umma wote wa Kiarabu.  Kwa hiyo umoja wa kiarabu, kwa maana kubwa, ni umoja wa watu na umoja wa malengo, bila kujali umoja wa katiba; Kwa sababu umoja wa katiba unaweza kupambana na vikwazo vingi na haujiweza kupatikana kwa muda mrefu.

 Kwa hivyo lazima tufanye kazi kwa ajili ya umoja wa kiarabu, ambapo kila watu wa kiarabu huhisi matumaini na matarajio ya watu wengine wa Kiarabu, na kila watu wa kiarabu anagusia masuala ya watu wengine wa Kiarabu, na kila watu wa kiarabu anawatetea watu wengine wa Kiarabu. kama ilivyotokea katika mwaka wa 1956 wakati wa nchini Misri iliposhambuliwa. Misri ilipambana na uchokozi wa pande tatu hakuwepo umoja wa kikatiba, lakini watu wa Kiarabu walitoka katika kila nchi ya Kiarabu.  Kwa sababu umoja ulikuwa kweli kukusanya watu wa Kiarabu katika kila nchi ya Kiarabu, watu wa Kiarabu walitoka Iraq wakati wa utawala wa Nuri al-Saeed, aliyeunga mkono hali ya uchokozi, na waliotakia kwamba utawala wa Misri ungeisha. na watu wa Kiarabu huko nchini Iraq walipigwa risasi na baadhi yao waliuawa.
 Yote haya yanaashiria kuwa kuna umoja wa kweli wa kiarabu ambao unawaunganisha watu wa umma wote la Kiarabu kutoka mashariki magharibi yake, bila kujali katiba.
 
 Kuna jambo lingine ninalotakia kusema: nguvu za kiitikadi na hata wafuasi wa ukoloni katika umma wote wa Kiarabu wanaulinganisha kama umoja ulio imara ... umoja wa masilahi, na umoja wao ili kupiga nguvu za kitaifa na nguvu zinazoendelea katika Umma wa Kiarabu. Je, ni nani anatetea faida za watu wa Kiarabu? ni nani anapambana na matokeo ya mapambano ya watu wa Kiarabu katika kukabiliana na kiitikadi na washirika wa ukoloni?
 
Kazi zinazoendelea za kitaifa za Kiarabu zisizo na ushabiki;  Ikimaanisha kuwa ni wajibu wa vipengele vyote vya kimaendeleo na nguvu za kimaendeleo katika umma wote wa Kiarabu na katika kila nchi ya Kiarabu kuunganisha ili kukabiliana na kuacha uchoyo na isipokuwa washirika wa ukoloni na kiitikadi kuwa kupiga nguvu ya kitaifa na ya maendelezo ika kiini yake.

Nani analinda harakati za mapambano?.... Anayelinda harakati za mapambano ni raia wenyewe, na watu hawa wa wanaofanya kazi ni mbele na wafanyikazi ni mbele.  Kwa sababu vigezo vya kimaendeleo na kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo kunamaanisha kwamba raia na tabaka la wafanyakazi wanapata haki zao  kupitia  mitaji ya kigeni, na kwamba tabaka la wafanyakazi na watu wanaofanya kazi wanapata uwiano ulio sawa, na kwamba inageuzwa katika jamii, watu wote ni sawa, hakuna faida za kitabaki... Haya ni matumaini ya tabaka la wafanyakazi na haya ndiyo matumaini ya watu wa Kiarabu.

 Kwa hivyo, ikiwa una matumaini, lazima uwe mbele ya mapambano, na viongozi wanapaswa wafikie vyeo vizuri hawatengwi na misingi ya wafanyakazi; Kwani kujitenga kutoka kwa misingi ya wafanyikazi; kunaweka misingi ya wafanyikazi katika kiitikadi na washirika wa ukoloni.
 
Sote tunajua kwamba tabaka la wafanyakazi ni watu wazuri wananoridhiana hata vitu vidogo bila ya malalamiko, na mawazo yao ni rahisi na kiitikadi kinaweza na ukoloni na washirika wake wanaweza kupiga nguvu za maendeleo dhidi ya tabaka la wafanyakazi.  Kwa kupotosha tabaka la wafanyakazi, kuyaweka mbali kutoka kwa malengo yake, na kulipamba maana na mitazamo tofauti na nyinyi wote mnaweza kuwa na uzoefu katika mambo haya.
 
 Ni jukumu letu kupa ari  nguvu za kazi, ni jukumu letu kuwa mbele ya mapambano, ni wajibu wa wafanyakazi katika umma wote wa Kiarabu kukabiliana na kiitikadi, ukoloni na wafuasi wa ukoloni. Jukumu la  wafanyakazi katika umma wote wa Kiarabu kuwa na jukumu la msingi katika kuunganisha baina ya nguvu zinazoendelea na za kitaifa na Ina jukumu la mapambano na jukumu la kimbele.  Kwa sababu wafanyakazi wanaathiriwa kwa kikwazo chochote, Wakati utengano ulipotokea huko nchini Siria - na utawala wa kiitikadi ukirudi - wafanyakazi  walikuwa watu wa kwanza kuathirika katika utawala wa kujitenga na ninadhani kwamba kaka wa Siria ambao wapo katika viwanda vilivyotaifishwa Na vile alivyifuta kutaifisha na marupurupu ambayo wafanyakazi walichukua, kiitikadi kilipochukua madaraka yaliwaangamiza faida za wafanyakazi wote.

 Kwa hivyo, ni nani anayeumizwa na mafanikio ya kali na washirika wa ukoloni?  Watu wanaofanya kazi.. tabaka la wafanyakazi.. nguvu ya kazi.. wanachama, ambayo ndiyo nguvu za maendeleo zinafanya kazi na nguvu za kitaifa zinawafanyia kazi,  je,ni nani anayepaswa kuhifadhi mapinduzi ya kiarabu, faida za kiarabu, na Mapambano ya kiarabu?  Wananchi ndio pekee wanaoweza kuhifadhi mapinduzi, malengo yake, matarajio na matumaini, wananchi ndio wanaweza kuhangaika kufikia mafanikio.
 
 Wajumbe wa Siria wananiambia kuwa wewe ni afisa kwa umoja, nasema kwa wajumbe wa Siria: Hapana.. Siwajibiki na umoja.. Waarabu katika kila nchi ya Kiarabu ndio wenye jukumu la umoja kwa sababu rahisi kwamba kila mmoja. Anakuja na kupita na kuisha, kila mtu huishi siku zake na kuishi maisha yake, na hiyo inaisha, lakini watu hawamaliziki/ hitimia, watu wanaweza kuhakikisha jambo haliwezekani.

 Ni wajibu wenu - wafanyakazi wa Kiarabu - kweli kuwa mbele ya mapambano ya kiarabu, mbele ya maendeleo, mbele ya utaifa wa Kiarabu, mkiweka mfano kwa watu wote wa Kiarabu wa kujitolea na ukombozi, na kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya umma wa kiarabu. Kwani nyinyi ndio askari mnaoweza kweli kuinua umma wa kiarabu, tuna askari uwanjani ambao wanaweza kupata ushindi na wanaweza kutetea ardhi zetu, ama wafanyakazi ni askari ambao wanaweza kulijenga umma  wa kiarabu, kujenga uwezo wa kiarabu. na kuendeleza umma wa Kiarabu kutoka nchi zinazoendelea hadi nchi za zilizoendelea kuwa nchi iliyoendelea, inaweza hivyo kufikia kile inachotaka bila kutegemea serikali yoyote ya kigeni. Mungu akupe mafanikio.


 Hotuba ya Mhe. Rais Gamal Abdel Nasser  alipowapokea wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Muungano wa Wafanyakazi wa Kiarabu.

Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy