Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser kwenye kiwanda cha kupambana na vifaru mnamo mwaka 1954

Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser kwenye kiwanda cha kupambana na vifaru mnamo mwaka 1954
Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser kwenye kiwanda cha kupambana na vifaru mnamo mwaka 1954

Imetafsiriwa na/ Malak Hazem
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed

Sifa ziwe kwa Mungu aliyetuwezesha - shukrani kwa nguvu za wale walioshiriki katika uanzishwaji wa kazi hii kubwa - kutimiza ahadi; mapinduzi yaliahidi Julai 23 na kuweka tarehe fulani za ufunguzi wa viwanda mbalimbali vya kijeshi, na ahadi hii ilitekelezwa katika kiwanda kidogo cha risasi huko Alexandria, kilichofunguliwa Julai 26, na leo kiwanda cha pili kinafunguliwa ambacho mapinduzi yaliahidi.

Baada ya ziara hii, najisikia fahari kwa wale walioshiriki katika uanzishwaji wa kazi hii kubwa, na ikiwa tunataka kupima mambo lazima iwe ya jamaa, hii ni kazi kubwa kuhusiana na kile kilichoenea katika siku za nyuma.

Ninajisikia fahari kwa wale walioshiriki na kufanya kazi, na ninahisi fahari ya nchi na kila raia, na wakati huo huo ninahisi fahari kwa kile nilichokiona leo cha tasnia nyeti, na kazi ya wafanyikazi wa Misri katika matokeo ya tasnia hii nyeti, na ninahisi fahari na nguvu, na ninahisi kuwa mapinduzi haya tayari yameanza kuchukua hadhi imara ya kimwili, pamoja na hali ya maadili niliyopata katika siku zake za kwanza.

Kama hali hii ya kimwili inakwenda sambamba na hali ya kimaadili, tunaweza kufikia matumaini yote na malengo ya kuona katika nchi yetu ukuu, nguvu, utukufu na heshima.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy