Maadhimisho ya uhuru wa Jamhuri ya Meksiko

Maadhimisho ya uhuru wa Jamhuri ya Meksiko

Imetafsiriwa na/ Mervat Sakr

Tarehe Septemba 16 ya kila mwaka, Siku ya Uhuru wa Mexico huadhimishwa...Uhuru wa Mexico ni mchakato mrefu wa kihistoria ulioanza Septemba 16, 1810, unaojulikana kama Greto de Dolores, na ulidumu hadi Septemba 27, 1821, wakati jeshi la Trigarante liliingia Mexico City.

Katika masaa ya mapema ya Septemba 16, 1810, padri Don Miguel Hidalgo y Costela aliwaita watu wa Mexico, kwa kupiga kengele za kanisa lake, kuchukua silaha dhidi ya ukoloni wa Hispania. Tukio hili lilijulikana kama "Kilio cha Uhuru" kwa sababu ilikuwa hatua ya awali na kuamsha iliyotikisa nguzo za watu wote kuanza mapambano dhidi ya mkoloni wa kigeni.

Tangu wakati huo, kipindi cha kihistoria kinachojulikana kama "Vita vya Uhuru" kilianza,  kilichodumu kwa miaka 11, ambapo watu wengi muhimu na wenye ushawishi, wanaume na wanawake waliochangia mapambano dhidi ya ukoloni na wanaokumbukwa katika historia ya Mexico... 

Baada ya miaka 11 ya vita na migogoro, mnamo Septemba 27, 1821, uhuru wa Mexiko kutoka Dola ya Hispania ulitambuliwa rasmi. 

Tangu wakati huo, maadhimisho ya "Kilio cha Uhuru", yaliyoanza miaka 212 iliyopita na ambayo athari zake bado hadi leo, yamekuwa yakifanyika kila mwaka. 

Idumu Uhuru!

Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy