Siku ya kimataifa ya Viziwi

Siku ya kimataifa ya Viziwi

Imetafsiriwa na/ Neema Ibrahim
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled  

Mwandishi maarufu wa Marekani Helen Keller alisema, “Mlango wa furaha unapofungwa, mwingine hufunguka, lakini mara nyingi tunatazama milango iliyofungwa kwa muda mrefu sana na hatuioni ile ambayo imefunguliwa kwa ajili yetu.”  Mwandishi huyu ni mmoja wa watu ambao ni wenye ulemavu wa maono (vipofu) na wenye ulemavu wa kusikia (viziwi), na mwandishi wa kitabu "Ikiwa Niliona kwa Siku Tatu," ambacho kinaweza kukutia moyo katika magumu na changamoto tunazokabiliana nazo katika maisha yetu ya kila siku.

 Historia inatuambia kuhusu watu mashuhuri na nembo za jamii mashuhuri zaidi kutoka kundi la viziwi ambao waliweza kukumbukwa na kazi zao kuu. Wahusika hao kama mpiga kinanda na mtunzi maarufu Ludwig van Beethoven, ambaye ni kiziwi, lakini yeye ndiye mpiga kinanda na mwanamuziki mkubwa zaidi katika duniani.

 Katika muktadha unaohusiana, maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Viziwi yalianza huko Roma, mnamo Septemba 28, 1958. Siku hiyo haiishii tu kwa sherehe za kimataifa, lakini pia hafla za kitamaduni na shughuli na vikundi vya majadiliano hufanyika ambapo wawakilishi wa watu viziwi na wasiosikia wenyewe hushiriki, ili kujadili njia za kutekeleza haki za viziwi na kuongeza ufahamu. Na kuzilinda, na kufanyia kazi changamoto zinazowakabili viziwi na wasiosikia vizuri na kujaribu kutafuta suluhisho kwao, pamoja na kufanya kazi kutoa kozi za mafunzo ya kufundisha lugha ya alama, na kujaribu kutoa njia za kiteknolojia zinazochangia katika kuimarisha mawasiliano na viziwi, na kufanya semina ili kuongeza uelewa wa jamii kwa umuhimu wa lugha ya alama ndani na ya nje. kuunganisha kundi hili katika jamii.

 shirika la Shirikisho la kimataifa la Viziwi huchangia katika kutoa sauti/ kura zao, kueleza mahitaji yao, na kuwasilisha mapendekezo yake kwa watoa maamuzi katika nchi nyingi. Shirika hili linajumuisha takriban vyama vya kitaifa 130. Vyama hivi vinawakilisha viziwi milioni 70 kote ulimwenguni


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy