Maadhimisho ya Miaka 100 ya Ugunduzi wa Makaburi ya Tutankhamun

Maadhimisho ya Miaka 100 ya Ugunduzi wa Makaburi ya Tutankhamun

Imetafsiriwa na/ Hasnaa Hosny
Imeharirwa na/ Mervat Sakr

Makaburi haya ni muhimu zaidi na maarufu duniani, kati ya Uvumbuzi wa kiakiolojia, kwa sababu ya Ugunduzi unaoambatana na kuibuka kwa mabaki ya dhahabu, vipande vya anasa, na utajiri mwingine mkubwa, licha ya ukubwa wake mdogo, na heshima ya muundo wake wa usanifu ikilinganishwa na makaburi mengine, inajumuisha mabaki ya 3,500 yaliyohifadhiwa sana.


Makaburi ya Farao wa dhahabu «Tutankhamun» Nambari 62 katika Bonde la Wafalme, kwenye Ukingo wa magharibi wa Nile huko Luxor, ni mali ya mfalme ambaye alichukua kiti cha enzi akiwa na umri mdogo, na alitawala Misri kwa miaka saba tu, lakini umaarufu wake ulizidi mfalme mkubwa wa Misri ya kale, makaburi yake lilianzia nasaba ya kumi na nane, kipindi (1336 - 1327 KK) kiligunduliwa mnamo 1922, na ni makaburi pekee ambayo yaliyomo yamegunduliwa kamili na sauti.

Kuta za chumba cha mazishi zina picha nyingi sana, zikielezea eneo la mazishi, zikionesha "Tutankhamun" katika kundi la miungu na miungu mingi. Pia zimepambwa na maandishi ya funerary kama vile Kitabu cha Emmy Duat au Kitabu cha Milango, kwa lengo la kumsaidia mfalme aliyefariki dunia kufikia maisha ya baadaye.

Mabaki yaliyogunduliwa makaburini ni pamoja na zana Tutankhamun alizotumia katika maisha yake ya kila siku kama vile nguo, Uvumba, vipodozi, mapambo, vitu vya kuchezea, samani, viti, vyombo vya dhahabu na Ufinyanzi, taa, na vifaa mbalimbali, magari, silaha, nk, zinazoonesha mtindo wa maisha ya jumba la kifalme.

Makaburi ya mfalme kijana liligunduliwa na mwanaakiolojia wa Uingereza, "Howard Carter" wakati alipokuwa akifanya uchimbaji kwenye mlango wa handaki linaloelekea kwenye Makaburi ya Mfalme Ramses IV katika Bonde la Wafalme, na aliendelea kuchimba hadi ilipopatikana chini ya magofu ya vibanda vya wafanyikazi vilivyojengwa tangu enzi za Ramests, na makaburi sasa yanachukua nafasi ya kwanza katika orodha ya maeneo ya juu ya akiolojia yaliyotembelewa zaidi nchini Misri.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy