Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani

Imefasiriwa na/ Omnia Muhammed
Imeharirwa na/Mervat Sakr
Mwanadamu daima anahitaji utulivu wa kudumu na amani, hivyo operesheni za kulinda amani zimesaidia kuhifadhi maisha ya watu wengi, pamoja na kuleta amani na utulivu kwa nchi nyingi kwa miongo kadhaa. Lakini operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa pekee haziwezi kufanikiwa katika kuweka mazingira muhimu ya kumaliza mzozo na kupata suluhisho la kudumu la kisiasa. Ushirikiano wake na nchi wanachama, taasisi za kiraia, mashirika yasiyo ya kiserikali, mashirika ya Umoja wa Mataifa na wengine ni muhimu kufikia maboresho yanayoonekana katika maisha ya umma, kwenye maeneo kama vile: maendeleo ya kiuchumi, utawala wa sheria, haki za wanawake, haki za binadamu, na upatikanaji wa afya na elimu.
Mnamo Tarehe Mei 29 kila mwaka, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, katika azimio lake la 57/129, liliitambua kama Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa. Katika siku hii ya 1948, ujumbe wa kwanza wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, Ujumbe wa Usimamizi wa Malori ya Umoja wa Mataifa (UNTSO), ulianza shughuli zake kwenye Mashariki ya Kati.
Tangu kuanzishwa kwa ujumbe wa kwanza wa kulinda amani, Ofisi za Umoja wa Mataifa, kwa ushiriki wa nchi wanachama na mashirika yasiyo ya kiserikali, zimeadhimisha kumbukumbu ya walinda amani waliobaki. Operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa ni chombo cha kipekee, chenye nguvu na kinachozunguka kila wakati kusaidia nchi zilizokumbwa na migogoro kujenga mazingira ya amani ya kudumu. Mchango wa Misri kwa vikosi vya kulinda amani unatokana na jukumu muhimu na la upainia la serikali ya Misri, na nia yake ya kusaidia juhudi za amani na usalama ulimwenguni kote kwa kushiriki katika ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na vikosi vyenye sifa.
Misri ni mojawapo ya nchi 10 zinazochangia kwa kiasi kikubwa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa, kwani ni miongoni mwa nchi kumi za juu ambazo zinachangia zaidi katika vikosi vya kulinda amani duniani, vya kwanza katika ulimwengu wa Kiarabu na vya tatu kwenye ngazi ya nchi zinazozungumza Kifaransa.
Sifa maarufu zaidi za jukumu la Misri kwenye operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa:
1- Misri ni nchi ya tatu duniani kuchangia kwa kiasi kikubwa vikosi vya polisi katika operesheni za kulinda amani.
2- Misri ni nchi ya tatu kwa ukubwa duniani kuchangia wataalamu wa kijeshi katika operesheni za kulinda amani.
3- Misri ni nchi ya saba kwa ukubwa kuchangia vikosi vya kijeshi katika operesheni za kulinda amani na vikosi vyake vya kijeshi, polisi na raia.
4- Misri inachangia wanajeshi wake katika operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa katika nchi 6.
5- Kituo cha habari kiliorodhesha nchi Misri inazoshiriki katika operesheni za kulinda amani, ambazo ni Mali, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sahara Magharibi, ujumbe wa mseto huko Darfur, na Sudan Kusini.
Katika siku hii, tunaheshimu taaluma, kujitolea na ujasiri wa wanaume na wanawake wanaohudumu katika operesheni za kulinda amani, na tunaheshimu kumbukumbu ya wale waliopoteza maisha yao kwa amani.
Dunia ya leo huhitaji amani na utulivu
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy