Siku ya Kimataifa ya Ufasiri
Imetafsiriwa na/ Ahmad Emad
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed
Umuhimu wa tafsiri ni kuimarisha mawasiliano na uelewano kati ya watu wa dunia, na kisha kuimarisha uhusiano kati yao na ushirikiano; kwa ajili ya maendeleo na kujenga amani katika jamii. Siku ya Kimataifa ya Tafsiri inaadhimishwa tarehe 30 Septemba, sambamba na sikukuu ya Mtakatifu "Jerome" mtafsiri wa Biblia hadi Kilatini, anayejulikana kama Mlinzi wa wafafsiri, na kukumbuka kumbukumbu ya kifo chake mnamo Septemba 30, 420BK. Umoja wa Mataifa hufanya shindano linalojulikana kama "Shindano la Mtakatifu Jerome la ufasiri katika Umoja wa Mataifa" mwakani, ambalo hutoa tuzo kwa ufasiri bora katika yoyote ya lugha zake rasmi sita (Kiarabu, Kihispania, Kifaransa, Kirusi, Kichina, na Kiingereza); ili kuimarisha kanuni ya lugha nyingi kama thamani ya msingi ya kutumia maarifa ya kina na teknolojia katika maendeleo endelevu."
Siku hii inakuja kama shukrani na kuthibitisha umuhimu wa ufasiri. Ufasiri ni taaluma ya heshima ambayo inategemea shughuli ya utambuzi, nafasi ya kitamaduni na ubunifu. Wafasiri pia wanachukuliwa kuwa wajumbe wa lugha kati ya watu. Ni jukumu lao kuleta karibu tamaduni, kurahisisha kiwango cha uelewa kati ya watu binafsi na vikundi, na kuimarisha maadili ya amani na usalama duniani.
Ufasiri ni mchakato wa kuhamisha mazungumzo au maandishi kutoka lugha moja hadi nyingine. Ni taaluma ya zamani inayoanzia nyakati za kale. Asili ya neno "Ufasiri" ni Kilatini "traducere", ambalo linamaanisha "kuhamisha".
Ufasiri umegawanywa katika aina kadhaa, zikiwemo:Ufasiri ya Simultaneous,ufasiri ya Uandishi ufasiri ya Maandishi,ufasiri ya Sauti.
Mwaka wa 1953, Chama cha Kimataifa cha Wafasiri (FIT) kilianzishwa. FIT ilianza kuhamasisha na kuendeleza sherehe za Siku ya Kimataifa ya Tafsiri. Mwaka wa 1991, FIT ilizindua wazo la Siku ya Kimataifa ya Tafsiri, ambayo ilitambuliwa rasmi na FIT. Mnamo Mei 2017, kwa mujibu wa Azimio A/71/L.68, lililosainiwa na nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Azerbaijan, Bangladesh, Belarus, Costa Rica, Cuba, Ecuador, Paraguay, Qatar, Turkey, Turkmenistan, na Vietnam, Umoja wa Mataifa uliidhinisha Siku ya Kimataifa ya ufasiri kuadhimishwa kila mwaka tarehe 30 Septemba; Kutokana na umuhimu wa ufasiri katika mazungumzo ya tamaduni, Shirika la Elimu, Utamaduni na Sayansi kwa Nchi za Kiarabu (ALECSO) liliandaa Mpango wa Kitaifa wa Tafsiri ambao ulipitishwa na Mkutano wa Mawaziri Wanaohusika na Masuala ya Utamaduni katika Nchi za Kiarabu huko Algeria kuanzia Mei 9 hadi 11, 1983. ALECSO pia ilielekeza vituo na idara zake kuelekea kuimarisha maktaba ya Kiarabu kwa ufasiri za fasihi na kitamaduni.
Vyanzo:
Shirika la Elimu, Utamaduni na Sayansi kwa Nchi za Kiarabu (ALECSO)
Tovuti Rasmi ya Umoja wa Mataifa
Tovuti Rasmi ya Islam Online
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy