Mahusiano kati ya Kiswahili na Kiarabu

Mahusiano kati ya Kiswahili na Kiarabu

Imeandikwa na/ Ebrahim El-Saqqa

     Kiswahili kimeathiriwa na lugha mbalimbali, ambapo mojawapo ya lugha hizo ni kiarabu, Lugha ya Kiswahili imechukuliwa kama lugha rasmi huko nchini Tanzania na Kenya, na vilevile baadhi za nchi za kusini mwa Afrika na Mashariki zimeongea lugha hii kama vile: Riwanda, komoro, Uganda na Jumhuri ya kidemokrasia ya Congo.

     Aghalabu ya  wazungumzaji wa lugha hii wakaa eneo hilo la Pwani za kiafrika katika upande wa  mashariki, huko  Oman na Waswahili walikuwa na ubadilishaji wa kibiashara kwa muda mrefu. Na vilevile,  waarabu na waaswahili walikuwa na historia yenye mahusiano na ubadilishaji wa kibiashara iliyokuwa na athari yenye kina kwenye lugha ya Kiswahili. Mahusiano mema haya kati waarabu na waswahili yanarudia wakati wa kati kupitia kipindi cha kuanzisha biashara ya  utumwa kati ya warabu na wakazi wa upande wa Mashariki mwa Afrika.

     Athari za mahusiano kati waarabu na waswahili zinajitokeza katika maneno ya Kiswahili, ambayo maneno mengi ya kiarabu yaliyatoa athari, na hayo yanajidhihirishwa na baadhi ya maneno kama, Subiri, kwa maana yake ileile kwenye lugha ya kiarabu, kitabu pia kwa maana yake ileile kwenye kiarabu na vilevile maneno mengine mengi.

     Mwanzoni, lugha hii ilikuwa ikiandikwa kwa kiarabu, na hiyo inatuonesha kiasi cha mahusiano yenye imara kati ya warabu na waswahili tangu enzi za zamani.

    Isalmu ilikuwa na athari kubwa, ampabo lugha ya Kiswahili iliathiriwa na maneno mengi ya kidini kiarabu kama, “Allah”, “mskiti”. “Sala”. Na vilevile Utamaduni na mila zilichangia kuingiliana  maneno mengi ya Kiarabu kwa lugha hiyo, na alama za  kitamaduni kati ya hizo mbili zilichanganya  na kuunda utambulisho wa kipekee wa jamii za waswahili.

    Kwa njia hii, Mahusiano ya Kiswahili na Kiarabu ni mfano imara wa mwingiliano wa lugha na utamaduni unaotokea kufuatia kwa wakati na mipaka.