Hazem Abdel Wahab ni Sauti ya Afrika kupitia Vituo vya Redio vya Misri

Hazem Abdel Wahab ni Sauti ya Afrika kupitia Vituo vya Redio vya Misri

Hazem Abdel Wahab alikuwa mojawapo wa viongozi wakuu wa redio ya kimisri, baada ya kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Afrika ya Mtandao wa Redio kwa Afrika. Alianza kazi yake mnamo mwaka 1993 akifanya kazi katika Programu ya Kiswahili ya Utawala Mkuu kwa Afrika baada ya kupata Shahada ya Kwanza ya Lugha na Tafsiri kwenye Sehemu ya Lugha za Kiafrika.

Kupitia miaka 30, alikuwa na jukumu muhimu katika kuandika matukio na shughuli za Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri, haswa zile zinazoambatana na mahusiano ya Misri na Afrika, na akapanda nafasi kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Kiswahili hadi akiwa Mkurugenzi wa idara, kisha kuwa Mtayarishaji Mkuu wa vipindi mnamo mwaka 2014, hadi Mkurugenzi wa vituo vya redio vilivyoelekezwa Afrika kutoka 2016 hadi kifo chake mnamo tarehe Aprili 27, 2024.

Marehemu Hazem Abdel Wahab alichangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya vipindi vilivyoelekezwa Afrika, na mojawapo ya mafanikio yake makubwa ni kurekodi na kutafsiri Qurani Tukufu kwa Kiswahili. Alituachia urithi tajiri wa vipindi vya redio kama vile "Angalia matukio", "Nuru kuhusu matukio", na "Ziara katika viwanja vya michezo". Pia alisimamia maandalizi na kurekodi mfululizo wa "Ubinadamu wa Uislamu" kwa Kiswahili na Kiarabu, uliooneshwa mwezi wa Ramadhani uliopita.