Kiswahili na Jukumu Lake Katika Maendeleo ya Ushirikiano ya Kikanda Katika Afrika Mashariki
Imeandikwa na/ Alaa Yahia
Tangu wakati wa nyuma, Bara la Afrika linajitahidi kushirikiana na kujitosa kati ya nchi na nyingine, ili kuhakakisha ushirikiano wa kikanda kwa aina zote, na mojawapo ya aina hizi ni “Jumuiya ya Afrika Mashariki” ambayo ni methali halisi kwa ushirikiano wa kikanda katika Afrika Mashariki, kwa kuwa malengo ya ushirikiano wa kikanda ni kuongeza maendeleo ya kiuchumi, kupunguza vikwazo vya kibiashara, kuongeza utulivu wa hali ya kisiasa katika eneo, kuongeza biashara, kuunda nafasi za ajira na kuboresha miundombinu.
Jumuiya hii inajumuisha nchi za Afrika Mashariki, na ndiyo Kiswahili inachukuliwa kama nguzo ya pamoja kati zao, ambapo imekichukua kama njia kwa kuimarisha maslahi ya kisiasa na ya kiuchumi, kuimarisha Umoja na kuhakakisha Usalama wa Taifa, na pia kuhafidhisha utambulisho wa kiafrika.
Lugha ya kiswahili ina jukumu kubwa muhimu sana katika maendeleo ya kiuchumi, kwa kuwa kugeukia biashara hakukamili ila kwa lugha, hakuhusiani na fedha na bidhaa tu, na lugha hii ni mojawapo kati zao na inaenea kwa upana kujumuisha sehemu kubwa zaidi inawezekana chini ya mfumo wa kimkakati cha kiuchumi cha taifa moja, na unaochangia mipango yake maalumu bila ya kukosa uwezo, na kutumia lugha vizuri ni msingi katika mchakato wa maendeleo ya kiuchumi, kwani hii tu inaweza kubadilisha maarifa na mazoefu ya kisayansi na kuyafikisha baina ya watu ikiwa jamii au taasisi zake na hata kwa sehemu zote za mfumo wa kiuchumi kama fedha inavyofanya kwa ugeukaji wa biashara.
Haya yanatufikisha kwa lengo la pili kwa ushirikiano wa kikanda katika Afrika Mashariki, nayo ni kupunguza vikwazo vya kibiashara kati ya nchi za Kanda, na hii ni kwa njia ya kupunguza ushuru wa forodha na vikwazo sivyo forodha kama vile: ushuru na sheria za udhabiti, na kupitia kupunguza vikwazo vya kibiashara, nchi za kikanda zinaweza kuongeza ushirikiano wa kiuchumi unaokuwepo, kwa kuwa kupunguza vikwazo vya kibiashara na maendeleo ya kiuchumi ni michakato miwili inayoambatana na inayoisongika ni lugha.
Jukumu la lugha katika utulivu wa hali ya kisiasa unaochangia ushirikiano wa kikanda wa Mashariki ni ikiwa na chombo ambacho utawala unaweza kuelekeza raia na kubadilisha maoni ya umma kuhusu suala lolote, na kwa sababu hii inageukia kwa kudhibiti na kutawala na kuipitia inaweza kutawala kwa watu wote, na kupitia kufanya kazi pamoja, nchi za kikanda zinaweza kukubiliana na changamoto zinazofanana kama: vitisho vya usalama na ukosefu wa utulivu wa kisiasa, ikisababisha kuongeza utulivu wa hali ya kisiasa na kuboresha utawala katika kikanda, na Kiswahili ni lugha ya rasmi katika nchi za Afrika Mashariki, nacho ni lugha ya kisiasa na utawala wa nchi hizi.
Ushirikiano wa kikanda unasababisha kuboresha miundombinu katika kikanda kupitia kufanya kazi pamoja, nchi za kikanda zinaweza uwekezaji katika miundombinu kama vile: barabara, reli na bandari. Nayo yakisababisha kuboresha mawasiliano na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi, na huku Kiswahili inachangia katika kupunguza gharama za mradi wa miundombinu kupitia: kupunguza mahitaji ya wafasiri, kuwasiliana na wafanyakazi vizuri na kuzuia vikwazo vya sarufi kwa kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki imeanzisha pia miradi mingi ya miundombinu kama mfano mpango mkuu wa reli katika Afrika Mashariki zinazolenga kuunganisha miji mikubwa katika kikanda kwa njia ya reli.
Jumuiya ya Afrika Mashariki pia imefikisha mafanikio makubwa katika kuboresha ushirikiano wa kijamii, kwa kuwa kuanzishwa kwa mfumo wa kusomo wa pamoja ni lengo la kimsingi kwake, na imezuia mipango inayolengwa kwa kuongeza ubadilishaji wa kitamaduni na utambulisho wa kikanda, kwa mfano: imefanya tamasha la kitamaduni la kikanda ambalo liliwaleta pamoja wasanii na waagizaji kutoka kanda kote ili kuonesha vipaji vyao na kufanya Kiswahili ifundishwe shuleni na vyuo vikuu.
Ndoto ambayo Rais “Julius Nyerere” aliota kueneza Kiswahili barani kote na kama lugha ya Afrika, hiyo inakarabia kuhakakisha, kwa kuwa lugha hii haikukuwa kama awali, bali imekuwa mojawapo ya lugha muhimu zaidi duniani, sio tu kwenye bara la Afrika, bali ilipanua nje na imechukua nafasi ya saba duniani, na inachukuliwa kama Lingua Franka katika shughuli na Afrika.
Karibu sana… Lugha ya Bara … kwaheri lugha nyingine.
Marejeleo:
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ni jumuiya ya kiserikali inayoundwa na nchi saba za Afrika Mashariki, nchi wanachama ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jamhuri ya Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Uganda na Tanzania. Jumuiya ilianzishwa mwaka 1967, iliporomoka mwaka 1977, na ilifufuliwa tena mnamo tarehe julai 7, 2000, makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mjini Arusha, huko Tanzania.