Mwanachama wa Harakati ya Nasser kwa Vijana nchini Kenya ashikilia nafasi ya Afisa mtendaji mkuu wa mfuko wa kiserikali wa kitaifa kwa Shughuli chanya

Mwanachama wa Harakati ya Nasser kwa Vijana nchini Kenya ashikilia nafasi ya Afisa mtendaji mkuu wa mfuko wa kiserikali wa kitaifa kwa Shughuli chanya

Kiongozi kijana wa Kenya "Roy Sasaka Telewa", aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa zamani wa baraza la vijana la kitaifa la Kenya na mwanachama wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, amechukua nafasi ya Afisa Mtendaji mkuu wa Mfuko wa serikali ya kitaifa wa kazi chanya, inayohusishwa na Wizara ya Utumishi wa Umma, Vijana na Masuala ya Jinsia ya Jamhuri ya Kenya, nao ni mfuko wa kuboresha maisha ya maskini kama wanawake, vijana, watu wenye ulemavu, watoto na wazee, kwa ajili ya kuwawezesha kijamii na kiuchumi kupitia kutoa msaada wa kifedha ili kuhakikisha maendeleo endelevu kikamilifu kwa wote.


Kwa upande wake, "Roy Sasaka Telewa" alisema kuwa atafanya juhudi kubwa kuwahudumu vijana na Jamii ya Kenya kwa uwezo na nguvu zake zote, akiashiria utayari wake wa kusaidia na kuunga mkono mipango yote ya jamii na miradi ya vijana inayowezekana kutekelezekwa na inayolenga kufikia malengo ya mfuko katika kuwahudumia walengwa na kuwawezesha kijamii na kuimarisha ushiriki wao katika maisha ya umma, pia akiwaita vijana kuendelea na utekelezaji wa mipango na miradi yao kwa nguvu na kujiamini.


Katika muktadha unaohusiana, "Hassan Ghazaly", Mwanzilishi na mratibu mkuu wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, kupitia akaunti yake binafsi kwenye mitandao ya kijamii, alionesha fahari na shangwe yake kwa hatua za ujasiri zilizochukuliwa na viongozi na wanachama wa harakati katika njia zao za kitaaluma, na shughuli zao za chanya zenye ushawishi mkubwa sana, akisisitiza uangalizi wake juu ya uendelevu wa programu zilizozinduliwa kuwekeza katika nguvu za vijana, katika nyanja za maendeleo, ujenzi wa ujuzi na uhamisho wa uzoefu wa kitaifa, aiashiria kuwa harakati ni jukwaa linalojumuisha  vijana wenye ushawishi mkubwa zaidi katika ngazi ya mabara matano (Afrika, Asia, Ulaya, Marekani ya kusini, Australia), waratibu wake wanafanya kazi bila kustarehe na kuendeleza wenzao na kuimarisha ushiriki wao katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.