Mradi wa Bozoor wahitimisha shughuli za 2023 na kuwaheshimu wanufaika wake

Mradi wa Bozoor wahitimisha shughuli za 2023 na kuwaheshimu wanufaika wake

Mradi wa Bozoor kwa Elimu Sambamba ulihitimisha shughuli za 2023 kwenye maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kujitolea, katika makao makuu ya Maktaba ya Umma ya Misri huko Dokki, na sherehe hiyo ilijumuisha semina kuhusu "Maandalizi mazuri kwa Soko la Kazi" iliyowasilishwa na mwandishi wa habari Amira Sayed, Mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje kwenye Gazeti la Egyptian Gazette, na Mwalimu Msaidizi katika Kitivo cha Habari kwenye Chuo Kikuu cha Amerika, na iliyosimamiwa na Hassan Ghazaly, mwanzilishi wa Mradi wa Bozoor kwa Elimu Sambamba na mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Sayansi ya Siasa katika Baraza Kuu la Utamaduni, kwa hudhuria ya viongozi kadhaa wa vijana, watoa maamuzi na wataalamu katika sekta ya maendeleo ya Utamaduni, wawakilishi wa taasisi za kiraia na sekta ya Umma, na Kada za Wakufunzi na wajitolea wa Mradi huo kutoka wanafunzi wa vyuo vikuu vya Misri na Chuo Kikuu cha Al-Azhar, kwenye Vitivo vya Al-Alsun, Habari, Uchumi, Sayansi ya Siasa, Lugha na tafsiri na Mafunzo ya Binadamu, na kundi la wasomi wa waandishi wa habari na wawakilishi wa taasisi za vyombo vya habari na televisheni ya Misri.

Katika muktadha unaohusiana, Mwandishi wa habari Amira Sayed alizungumzia Uzoefu wake kama mfasiri na mwandishi wa habari, wakati ambapo alielezea jinsi mwanafunzi wa chuo kikuu anavyojiandaa kwa soko la ajira, akielezea Umuhimu wa kushiriki katika shughuli za wanafunzi na kujitolea zinazohudumia Uwanja wao wa Utaalamu huwasaidia kuwekeza katika Uwezo na Ujuzi wao, akisisitiza kuwa hii ndio inayotofautisha mfasiri wa Misri na vyombo vya habari kutoka kwa wengine katika vikao vya kimataifa na kimataifa na kumweka katika safu za kwanza za Uchaguzi. 

Katika muktadha huo huo, Hassan Ghazaly alielezea mwanzoni mwa hotuba yake, muhtasari wa Utangulizi wa Mradi wa Bozoor kwa Elimu Sambamba, ambapo safari ya kazi ilianza miaka saba iliyopita chini ya kauli mbiu "Mjifunze...Muwe huru", akibainisha kuwa Mradi huo una sehemu kuu tatu: Mpango wa Shule ya Kitaifa kwa Maandalizi ya Kada, Mpango wa Mipango ya Jamii, na Programu ya Saluni ya Bozoor, akisisitiza kuwa Mradi huo ni bure na hauna faida yoyote, akibainisha kuwa shughuli za leo ni hitimisho la Shule ya Kitaifa kwa Maandalizi ya Kada ya Wanafunzi, iliyofaidika na wanafunzi wa chuo kikuu cha 416 na takribani 100 kati yao walishinda nafasi ya kwanza katika idara za mafunzo na lugha mbalimbali, zikiwemo vyombo vya habari, Uandishi wa maudhui na Ufasiri kwa Kifaransa, Kiingereza, Kiswahili na Kihispania.

Ghazaly aliongeza kuwa Mradi wa Bozoor ulilenga mwaka huu katika kuandaa na kushiriki kwenye shughuli za maadhimisho ya miaka 50 ya kifo cha Mkuu wa Fasihi ya Kiarabu, Taha Hussein, akielekeza nia ya Mradi wa Bozoor kwa Elimu Sambamba ili kuimarisha dhana na maadili ya familia ya Misri, na kutoa nafasi pana kwa kubadilishana Utaalamu na Uzoefu ili kuongeza Uwajibikaji na Ushiriki wa jamii ya vijana katika hatua tofauti, akibainisha kuwa Mradi huo ni moja ya njia za kutekeleza nyaraka tatu za msingi zinazotegemea, ambazo ni Dira ya Misri 2030, Ajenda ya Afrika 2063, na Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030, pamoja na alisisitiza azma ya mradi huo kukamilisha matembezi yake kwa mipango na njia za hali ya juu ili kukidhi mahitaji ya jamii na soko la ajira, ili kuamsha mapendekezo ya wanafunzi na wajitolea wa mradi huo.

Ghazaly alihitimisha hotuba yake kwa kutoa shukrani na shukrani zake kwa taasisi zote za elimu na Utamaduni, taasisi za kiraia na za kiserikali zinazounga mkono Mradi wa Bozoor kwa Elimu Sambamba, ukiongozwa na Maktaba ya Umma ya Misri kwa maandalizi ya tukio hilo, kisha akaheshimu wawakilishi kadhaa wa taasisi hizo, ikiwa ni pamoja na Jumuiya ya Afrika huko Kairo, Mheshimiwa Balozi Mohamed Nasr El-Din, na kupokea Ngao ya Heshima Dkt. Amna Fazza, pamoja na kumheshimu vyombo vya habari Amira Sayed, Mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje kwenye Gazeti la Egyptian Gazette, na Mwandishi wa habari Randa Khaled, anayehusika na faili ya Afrika kwenye Gazeti la Al-Wafd, na Mwandishi wa habari Hanaa Mohamed kwa ajili ya Gazeti la Al-Gomhouria, na Mhandisi Ahmed Barrani, Mtaalamu wa Sera za Vijana wa Kimataifa.