Majaada Hashem.. Mpalestina aongozaye kampeni ya kutambulisha Udhamini wa Nasser wa Uongozi kupitia Taasisi ya Red Crescent
Ndani ya mfumo wa kampeni za uhamasishaji wa Udhamini wa Nasser katika nchi kadhaa za Kiarabu na Kiafrika, mmoja wa wanafunzi wa Udhamini katika kikao chake kilichopita, Majaada Hashem, alianzisha kutambulisha Udhamini wa Nasser kwa Uongozi miongoni mwa shughuli za huduma za Tiba " Red Crescent" huko Palestina, na hiyo pamoja na idadi ya vijana wafanisi katika jamii kule .
na Hiyo ilitokea kutokana na mazungumzo kuhusu Rais Marehemu Gamal Abd El Nasser na nafasi yake katika kesi ya Palestina na kuhifadhi uraia wa kiarabu . Majaada Hashem alisimulia tajriba yake binafsi nchini Misri na jinsi alivyoathiri katika kuunda tabia zake baada ya alipokuja Misri akiwa na umri wa miaka 18 na ufahamu wake na mitazamo imeshaunduliwa ndani ya Nchi hiyo.
Majaada Hashem alisema kwamba ndani ya mfumo wa majadiliano hayo na vijana wafanisi katika jamii ,imeshazungumziwa Uongozi wa Misri mnamo miaka ya hivi karibuni, uzoefu wake wa kiuchumi na kiusalama, na uwezo wake wa kufikia malengo yake ambayo iliyatilia mkazo vizuri .
Aliongeza kusema kuwa kupitia Udhamini wa Nasser kwa Uongozi , aliweza kufahamiana na vijana wafanisi katika jamii kutoka uraia mbalimbali , na jinsi alivyoweza kufaidika na hayo , akisisitiza kuwa japo uhanganiko wa vyombo vya habari , tovuti ya Udhamini wa Nasser inaweza kutoa makala na taarifa zinazoaminika, na hilo lililothibitishwa na vijana katika mkutano wa uhamasishaji baada ya kusoma maudhui inayotolewa .
Katika muktadha huo, inatajwa kuwa idadi ya waombaji wa Udhamini huo kwa umri kati ya miaka 35 mpaka 40, imefikia hadi sasa kwa 11.6% .
Kwa upande wa wenye umri kati ya miaka 25 na 30, ilifikia 35%, wakati ambapo idadi ya walioomba Udhamini huo wenye umri kuanzia 16 hadi 25 hadi ilifikia 26.3%, na kati ya miaka 30 hadi 35,ilfikia 22.7%, na kutoka 40 hadi 45, idadi ya waombaji ilifikia 2.6%, na inatarajiwa ongezeko la idadi ya waombaji mnamo siku zijazo.
Kwa wale waliopata masomo ya Juu kutoka waombaji,kiasi chao kilifikia 19.3% ambapo walio na Shahada ya Uzamili walifikia 17.6%, na wenye Uzamivu walifikia 8.2% miongoni mwa jumla ya waombaji.
Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa; unatolewa Kukamilisha juhudi za Misri za kutekeleza jukumu lake lililohusisha kuimarisha nafasi ya vijana kwa upande wa ndani , kikanda, bara na kimataifa kupitia kutoa aina zote za misaada , kuwezesha na mafunzo , pamoja na kuwawezesha katika nafasi za uongozi na kufaidika kwa uwezo na mawazo yao.
Inapangwa kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa utaanza mnamo Mei 28 ujao , na utaendelea kwa siku 15.