Harakati ya Nasser yashinda Tuzo za Kituo cha Kitaifa kwa Ufasiri

Harakati ya Nasser yashinda Tuzo za Kituo cha Kitaifa kwa Ufasiri
Harakati ya Nasser yashinda Tuzo za Kituo cha Kitaifa kwa Ufasiri

Kituo cha Kitaifa kwa Ufasiri kilitangaza majina ya washindi wa toleo la nne la Mashindano ya Ugunduzi wa Wafasiri, yaliyokuja katika kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya Mkoa wa Qalyubia, wakati orodha ya washindi ilijumuisha majina ya wafasiri wanne wa Harakati ya Nasser kwa Vijana walioshika nafasi ya kwanza: Mervat Sakr, Aya Nabil, Zainab Makky, na Fatima El_Sayed, ambao walijiunga na harakati ndani ya mpango wa Uwezeshaji wa kitaaluma uliotolewa na Harakati ya Nasser kwa Vijana kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Misri kutoka vitengo za ufasiri, fasihi, lugha, vyombo vya habari na taaluma za kisiasa.

Katika muktadha unaohusiana, mwanzilishi wa Udhamini na Harakati ya Nasser kwa Vijana " Hassan Ghazaly" alionesha fahari yake kuhusu juhudi na ubora wa wafasiri wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, akionesha ubora wa wafasiri hao, hata katika kiwango cha mafunzo ya kitaalamu ndani ya programu za harakati, akionesha kuwa hii ilisababisha kuhitimu kwao katika hatua nyingi za mafunzo, ikiwa ni pamoja na mabadiliko yao kutoka kitengo cha kutafsiri kama Wafasiri kuwa Mabalozi wa harakati, wakati baadhi yao walifaulu hadi akawa Mkaguzi katika idara ya lugha ya Kiswahili, ambayo ni hadithi ya mafanikio halisi kwa programu ya Uwezeshaji wa kitaaluma kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Misri, inayowasilishwa na Harakati ya Nasser kwa Vijana kwa kushirikiana na Mpango wa Bozoor"Shule ya Kitaifa ya Maandalizi ya Kada za Wanafunzi".

Ghazaly amesisitiza juhudi za Harakati ya Nasser kwa Vijana kuwawezesha vijana katika nyanja mbalimbali kupitia programu nyingi za Uwezeshaji na mipango ya kujenga uwezo katika ngazi mbalimbali za kitaifa, kikanda, na katika ngazi za bara na kimataifa, akibainisha kuwa Harakati ya Nasser kwa Vijana imeweza zaidi ya miaka minne kuenea katika nchi 65 duniani kote na kwamba idadi ya walengwa wake inafikia wanufaika 11,500 kama ishara ya kufikia uendelevu na uwezekano rahisi, pamoja na tovuti yake, inayotangazwa kwa lugha tano (Kiarabu - Kiingereza - Kifaransa - Kiswahili - Kihispania) Ina takriban makada 223 wa watafsiri katika programu zetu.