Harakati ya Nasser kwa Vijana nchini Chad yazindua Mpango wa Mabalozi wa Nia njema kwenye ngazi ya Jamhuri
Imetafsiriwa na: Loaai Adel
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Kozi ya maandalizi ya uongozi kwa toleo la mikoa ilizinduliwa katika mji wa Abcha, mji mkuu wa mkoa wa Ouadi, iliyoandaliwa na Harakati ya Nasser kwa Vijana, tawi la Chad, kwa kushirikiana na Mpango wa Mabalozi wa Goodwill na mpango wa Msaada wa Ndugu wa Raia Wako, na kupangwa na kikundi cha makada wa Ottoman wakati wa kipindi cha 24 hadi 29 Septemba.
Kozi hiyo inalenga kuwaandaa wakufunzi 200 katika fani ya uongozi na maendeleo ya binadamu kwa kuwafunza ujuzi mwingi na kubadilishana uzoefu katika nyanja mbalimbali hususani fani za utaalamu na ujasiriamali. Aliwasilisha uzoefu mwingi wa vijana wenye matumaini na mafanikio katika nyanja za ujasiriamali na asasi za kiraia, na pia walifundishwa juu ya misingi ya kompyuta na jinsi ya kuandaa mfuko wa mafunzo.
Shughuli za kozi hiyo zilihitimishwa kwa sherehe ya kufunga kwa heshima ya wanafunzi na wale wanaosimamia mipango miwili, iliyohudhuriwa na Naibu Meya wa Tatu wa Manispaa ya Absha.