Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Indonesia mwaka 1955
Imetafsiriwa na/ Sara Saed
Imehaririwa na/ Mervat Sakr
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu...
Inanipa furaha kubwa kutuma leo pongezi za wananchi wangu na pongezi kwa taifa linalopendwa na mioyo yetu, ambalo lina nafasi nzuri kwetu sote, serikali ya Indonesia na watu. Nchi hii pendwa imepata uhuru wake baada ya mapambano makali na mapambano ya muda mrefu, na haikuwa ajabu kwamba taifa la Misri - kwa umbali kati yake na Indonesia - ni nchi ya kwanza kubariki Uhuru huu na kuiunga mkono na kutoa wito wa mafanikio, ni muumini kwamba dada yake katika Mashariki ya Mbali anastahili Uhuru huu na Ushindi, watu wake wanaopigania Uhuru hawajui Utii au Ujitiisho, wakiongozwa na Uongozi wa busara na kiongozi mwenye historia ya taifa tukufu ni kaka yangu na rafiki yangu Dkt. "Ahmed Sukarno".
Kiongozi huyu mkuu ameonja Uchungu wa mateso, kufungwa jela na Uhamishoni, lakini moyo wake mkubwa, uliojaa Uzalendo na Uaminifu, ulipunguza tabia zote na maumivu kwa ajili ya taifa lake, Uhuru na Ustawi wake.
Nilipokuwa Bandung, nilihisi nguvu ya watu hawa na uaminifu wa kiongozi na kiongozi wake wakati nilipowakilisha nchi yangu katika Mkutano wa Watu wa Kiafrika na Asian, uliofanyika katika moja ya miji ya kindugu ya Indonesia, iliyokuwa tukio la historia, na ulimwengu wote ulihisi kwamba miale ya amani ilianza kutoka kwenye Ukumbi wa mkutano huu, kutoka kwa moyo wa nchi hizi za Ushirikiano, na kutoka kwa kina cha watu hawa waliowakilishwa ndani yake.
Mapambano ya Indonesia ya kupenda Uhuru na kupenda amani hayajakoma kwa hilo; Indonesia imewakilisha uwakilishi mzuri zaidi mwaka huu katika Siku ya Taifa ya Misri wakati tunasherehekea kumbukumbu ya tatu ya mapinduzi ya Misri, na nilifurahi kupata rafiki yangu Dkt. "Ahmed Sukarno" anashiriki furaha yetu katika Siku ya Ukombozi nchini Misri, na kama isingekuwa kwa wasiwasi wangu mwingi ningetamani kuwa karibu na kiongozi wa Indonesia kusherehekea pamoja nchini Indonesia siku yake ya Uhuru na watu wake huru na wanaojitahidi.
Ikiwa serikali ya Misri na watu leo wanashiriki furaha ya Siku ya Uhuru wa Indonesia, wanahamasishwa na mahusiano yenye nguvu kati ya watu wawili na mahusiano yanayozidi kuwa imara siku hadi siku, na ninamwomba Mwenyezi Mungu kutimiza matumaini yetu ya Ustawi wa watu wetu wanaoteseka.
Wassalmu Alaikum Warahmat Allah.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy