Hotuba ya Mheshimiwa Rais Gamal Abdel Nasser Katika Kongamano Maarufu huko Taiz, Yemen, mnamo 1964

Hotuba ya Mheshimiwa Rais Gamal Abdel Nasser Katika Kongamano Maarufu huko Taiz, Yemen, mnamo 1964
Hotuba ya Mheshimiwa Rais Gamal Abdel Nasser Katika Kongamano Maarufu huko Taiz, Yemen, mnamo 1964
Hotuba ya Mheshimiwa Rais Gamal Abdel Nasser Katika Kongamano Maarufu huko Taiz, Yemen, mnamo 1964

Imetafsiriwa na/ Tasneem Mohamed
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled

Enyi Ndugu wapendwa, ndugu wenye uhuru, ndugu wanamapinduzi:
 Leo nimewaona watu wa Yemeni miongoni mwenu huko Taiz, kama nilivyowaona jana huko mji wa Sanaa  wakiwakilishwa na nguvu, majivuno, mapinduzi na uhuru, watu hawa wa Yemeni walijikita kupata Uhuru, waliasi, na Mungu awape ushindi na uwape majivuno, heshima na uhuru.

Enyi Ndugu wapendwa:
Watu wa Yemen daima walikuwa wakinyanyua bendera ya Uislamu na kunyanyua Bendera ya Uhuru katika mashariki na magharibi mwa ardhi hadi maimamu wakawakusanyikia na kuwafanya wajisikie fedheha na mateso, wakawafunga ndani ya mipaka yao, na wakawazuia kueneza ujumbe ya Uhuru. Uislamu duniani kote lakini ,Je watu wa Yemen walitulia? Kamwe…watu wa Yemen hawakutulia kamwe.Badala yake, waliasi dhidi ya unyonge, ya utumwa, ya utawala wa dhulma, na dhidi ya  utawala wa kigaidi, waliasi daima, na hawakutishia kutokana na kukatwa vichwa, wala hawakutishwa na kifo, wala hawakutishika na kukamatwa mwa magerezani, waliasi kwa sababu wao ni watu wenye majivuno, watu wenye uhuru,  hawawezi kukubali dhuluma na utumiwe hadi watu wa Yemeni ikiongozwa na Rais Al-Hur Al-Salal, ilifufuka mnamo Septemba 26, 1962 ilipanda kuharibu dalili za unyonge, majibu na dhuluma, Mungu akataka iwe ni ushindi na ilishinda,na ushindi wake ulikuwa ushindi  kwa nyinyi nyote, watu huru wa Yemen, ambao walipanga uhuru, na kila wakati walijitahidi na kupigania kwa ajili ya kupata Uhuru wake. 

 Leo ninapoona nguvu yenu, kama jana nilivyoiona kwa ndugu zako huko mji wa Sanaa, nimeona kuwa watu wa Yemeni hawakudhoofika au hakutulia  kamwe katika mamia ya miaka ya unyonge na utumwa, kwani kupitia mapambano yao walikuwa wakizidisha nguvu na imani yao iliimarisha, niliona kwako leo, kutoka uwanja wa ndege hadi hapa, nguvu halisi za Waarabu na za Kiislamu, pia niliona jana kwa ndugu zako huko mji wa Sanaa; niliona kwao roho ya Uhuru na ya Mapinduzi.

Enyi Ndugu wapendwa:
Nyinyi ni watu wa Yemen wenye umoja , lakini Ukoloni  uliotaja kuwagawanya kwa makundi kadhaa  na vyama, lakini utashi wa  Mungu na utashi wenu  ulikuwa kuliko zaidi  ya utashi wa ukoloni,kwa hivyo ukoloni haukufanikiwa, wala kiitikio hakikufaulu kuwagawanya na kuwatenganisha ; kwa sababu ninachokiona hapa leo ndicho nilichokiona jana kule mji wa Sanaa: watu wenye nguvu… watu walioungana… watu huru… wanamapinduzi.

Enyi ndugu wananchi wapendwa
Mnamo tarehe 26 Septemba, Wakati wa Mapinduzi yako yalipofanyika, yalitikisa viti vya nguvu za kiitikio na kutikisa nguvu za ukoloni,kiitikio kilikukabili na ukoloni ukakabiliana nanyi; mpaka wakushinde na wakuangamize mapinduzi yanu, lakini nguvu yako na imani yako kwa Mwenyezi Mungu na nchi yako na imani yako yenye nguvu zaidi ya uhuru wanu na maisha yako ya kupendeza na ya heshima, yote haya yaliweza kuondoa njama za kiitikio na kukumbatia mwezi mzima, na ukoloni ukakabiliana nanyi na kuwasanya maimamu mliowahukumu uhamishoni, na mliowahukumu kifo, mkawaamuru waondoke nyumbani mwenu kwa sababu wameharibu ardhi yenu, ukoloni uliwakabili na huku ukaamini kwamba umeeneza mgawanyiko kati yenu na utashinda lakini nguvu zao -Enyi ndugu huru-zikaweza kushinda ngome za kiitikio na ukoloni.

Uingereza iilyokukabilii kwenu, Uingereza Mkuu – kama wanavyosema – kwa nini ikakukabili? Kwa sababu ya hofu yake kwenu na hata mapinduzi yanu; Kwa sababu mapinduzi yenu na mafanikio ya mapinduzi yako yanaondoa ukoloni na hila za kikoloni ambazo Uingereza ilikuwa inakabiliana na mapinduzi yenu, sisi tunavyojua – na leo tunatangaza hadharani – kwamba Uingereza imetuma silaha zake kwa muda wa miezi kadhaa ili kupiga mapinduzi yako, lakini silaha hazikutumiwa dhidi yako, badala yake zilirudi kwenye vifua vya ukoloni na kwa maeakala ya kikoloni huko Aden.

Nyinyi – Enyi ndugu- watu wenye uhuru , na umoja, watu wenye nguvu, watu wa mapinduzi ambayo hakuna mtu yeyote anayetumia silaha dhidi ya ndugu yake, lakini ukoloni ulimtaka kutumia silaha zake dhidi ya mtu yeyote; ili kuweza kujihakikishia kubaki kukaa huko kwenye Aden na kusini iliyochukuliwa, Uingereza ilinyakua Aden kutoka kwenu, na Uingereza ikateka sehemu ya kusini ya Yemen iliyochukuliwa kwa kutumia nguvu, njama na mapatano na maimamu wa zamani, lakini Uingereza inajua kweli  kwa hakika kwamba taifa la Yemen litakombolewa na watu wa Yemen wanamapinduzi  watavua vazi la unyonge na fedheha kwa kuwafukuza maimamu na wahaini; Watu wenye nguvu wa Yemen hawataruhusu Uingereza – ambayo wanasema ni kubwa – kubaki Aden au kubaki katika maeneo yaliyonyakuliwa kwenye kusini.

Watu wa Yemen walioasi Septemba 26 na walioasi kabla ya Septemba 26 na  waliotoa mhanga maisha na kutoa damu, watu wa Yemeni ambao Mungu aliwaandikia ushindi kwao mnamo Septemba 26 wanajua kwa hakika kwamba ushindi huu unamaanisha deni kwa ndugu zao waliokamatwa na ukoloni na waliosambuliwa na unyonge kwa sababu ya matendo ya ukoloni huko Aden na sehemu ya kusini iliyochukuliwa.

Watu wa Yemen walioishi maisha ya uhuru na walioshiriki  katika mapinduzi, hawatawaacha ndugu zao wa Aden waliopitia hali ya utumwa kutoka kwa ukoloni wa Uingereza, na katika kusini inayokaliwa kwa mabavu waliosambuliwa na ugaidi na magerezani kutoka kwa ukoloni wa Uingereza.Taifa zima la Kiarabu linaunga mkono Aden na kusini iliyokaliwa kwa ajili ya kupata uhuru wake. 

Na niliposikia tarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza juzi, ikiupinga Umoja wa Mataifa dhidi ya hotuba yao niliyowaelezea ndugu zenu wa Sanaa, ilipinga hotuba hiyo na kumfahamisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba yote yaliyoelezwa na Abdel Nasser huko Yemen kuhusu uhuru wa Aden na kuhusu uhuru wa kusini unaokaliwa husababisha ukosoaji wa azimio la Baraza la Usalama.

Uingereza inafanya makosa na hata haioni aibu, inafanya makosa-Enyi ndugu wapendwa-kwa nini Uingereza inafanya makosa? Kile alichoelezewa na Abdel Nasser huko Yemen ni kilekile kilichoelezewa na  Umoja wa Mataifa,kile kilichosemwa na Abdel Nasser huko Yemen ndicho kilichosemwa na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Kuondoa Ukoloni, alichosema Abdel Nasser ndicho kilichoamuliwa na Umoja wa Mataifa na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Kuondoa Ukoloni, umoja wa Mataifa iliamua kwamba Aden na kusini inayokaliwa kuwa huru na kwamba ilitangaza haki za  kujitawala.

Umoja wa Mataifa na Kamati ya Kuondoa Ukoloni ilitangaza kwamba Aden na kusini inayokaliwa itakuwa huru, kwamba kanuni za kujitawala itatumika, kwamba msingi wa wakoloni wa Uingereza huko Aden utafutwa, na kwamba kamati ya Umoja wa Mataifa itatumwa Aden na kusini iliyokaliwa ili kuchunguza ukweli, tabia ya Uingereza ilikuwaje? Uingereza ilikataa mapendekezo ya Umoja wa Mataifa, na Uingereza ilikataa pai kupokea kamati iliyoamuliwa na Umoja wa Mataifa, Jana, Uingereza ilisahau haya yote, ikapoteza kila kitu, hata aibu, na kujaribu kudanganya ulimwengu wote kwa kusema kwamba  kilichosemwa na Abdel Nasser nchini Yemen ilipinga kile kilichosemwa na Umoja wa Mataifa.

Tunawaambia kuwa matendo ya  kikoloni katika eneo la kusini yaliyochukuliwa na pia huko Aden, na kubakia kwenye misingi ya Waingereza huko Aden,linapingana na uamuzi wa Umoja wa Mataifa na Kamati ya Kuondoka Ukoloni Kwa hivyo uwe na aibu …Enyi Uingereza Mkuu… aibu hata kwa kidogo ili tusihisi ukoloni wowote kwako.

Idhaa ya London tangu siku kadhaa zilizopita – saa 48 zilizopita – ilitoa wito wa ulazima wa kuondolewa na majeshi ya Misri kutoka Yemen, kwa hivyo Uingereza inaweza kupenyeza  wafanyikazi wake. Tunawaambia kwamba tuko hapa watu wote  wa pamoja katika taifa moja, kwa hivyo hakuna tofauti yoyote kati ya mtu wa Yamen na Mmisri.. sisi ni taifa moja la Kiarabu.. Tunawaambia sisi ni taifa moja la Kiarabu. Ukoloni ulitaka tugawane, na ukoloni ukaweka mipaka kati yetu,Ukoloni ulitaka tuwashambulie wengine dhidi yetu, na ukoloni ulitaka tugawane umoja wetu na kugawanya kati ya malengo yetu,  lakini leo tunahisi nguvu zetu na kuhisi kuwa tunaweza kushinda mataifa makubwa.

Mnamo mwaka wa 1956 walikuwepo ndugu zanu Por Said na Misri waliweza kuyashinda mataifa makubwa na kuyarudisha nyuma,  Enyi ndugu zangu- tunayajua wenyewe sasa hivi, ndugu zetu- kinachojua kuhusu nchi yetu sasa,sisi waarabu ni taifa moja kila nchi mmoja anamtia nguvu mwenzake.Mapinduzi yalipozuka Septemba 26, tulikuunga mkono tangu dakika ya kwanza, lakini wakati wa upinzani na ukoloni ulipokukabili; tumekusudia kusimama nao na kukuunga mkono dhidi ya itikadi za upinzani na ukoloni. Kwa sababu sote tunahisi kwamba uhuru wenu ni uhuru wetu, kwamba mapinduzi yenu ni mapinduzi yetu, na kwamba nguvu zenu ni nguvu zetu. Tulihisi hili na kwamba mapinduzi yenu ni mapinduzi ya Waarabu wote na nguvu zenu ni nguvu za Waarabu wote.Tulihisi kwamba uhuru wenu ni sawa na uhuru wa Waarabu wote.Tulihisi kwamba Yemen, ambayo siku zote ilijitahidi na haikuacha kuhangaika, na ambayo mara zote iliasi na haikuacha mapinduzi; Mungu alitaka awe mshindi, na Mungu alitaka amuunge mkono wakati alipokabiliwa na ukoloni na wakati upinzani ulipomkabili.

Sisi – Enyi ndugu –Mungu akipenda,  tuko pamoja nanyi hapa, na pamoja nanyi hapa kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, ili kuyashinda mapinduzi yenu na watatimiza jukumu lenu la milele miongoni mwa taifa la Kiarabu la kutangaza ujumbe wa Uislamu, na kuinua ujumbe wa uhuru ambao wameuinua kwa miaka mingi. Kwa maelfu ya miaka, tangu wito wa Kiislamu, Yemen imekuwa ikinyanyua bendera ya Uislamu na kuinua bendera ya uhuru, na leo, mwaka mmoja na nusu baada ya mapinduzi, nahisi kuwa wameshinda na watarejea jinsi ulivyofanya  katika maisha yenu ya kwanza, wanainua bendera ya Uislamu na kuinua bendera ya uhuru kila mahali na kuinua bendera ya umoja wa kitaifa, hamtawezesha ukoloni kamwe na hamtawezesha upinzani kamwe unawagawanya kwa jina lolote na kwa sababu yoyote; chini ya majina ya uhuru au majina ya madhehebu,sote ni waarabu, hakuna mtu mmoja  atakayeweza kututofautisha, sisi sote ni waarabu tunaojua wajibu wetu sote ni waarabu tunaojua lengo letu,na vilevile lengo letu ni uhuru..lengo ni uhuru na lengo letu ni kujitegemea, Mungu alitaka tupate uhuru na Mungu alitaka tuufikie uhuru tukashinda.

Leo, na baada ya mwaka mmoja na nusu baada ya mapinduzi, tunamshukuru  Mwenyezi Mungu kwa mioyo yetu yote ya kina kwamba tumepata ushindi dhidi ya upinzani na ushindi wetu dhidi ya ukoloni, na tunaahidi kwa  Mwenyezi Mungu kwamba tutatembea katika njia ya uhuru, kwamba tutatembea katika njia ya mapinduzi, na kwamba tutatembea katika njia ya umoja wa Waarabu kwa ajili ya fahari ya Waarabu wote, na kwa ajili ya kuwainua vyeo vya Waarabu  wote. 

Haya yote- Enyi ndugu  – ni jukumu letu sote kwa taifa la Kiarabu, hili – ndugu – ndilo lililotufanya tuitishe Kongamano la Kilele la Waarabu ili kualika taifa zima la Waarabu wote… marais na wafalme wa taifa zima la Waarabu wakutane huko mjini Kairo ili tuunganishe juhudi zao dhidi ya Israel, na ili tunaweza kuunganisha juhudi dhidi ya ukoloni, kwa sababu ukoloni ndio ulioiunda Israel, bila Uingereza isingekuwa Israel; Baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia, Uingereza ilitoa Mamlaka juu ya Palestina, na Uingereza ikawawezesha Wayahudi kuhamisha watu wa  Palestina.Waingereza walipoingia Palestina, Wayahudi walikuwa zaidi ya 5%, na mnamo mwaka 1948, Wayahudi huko Palestina walifikia zaidi ya 50 %, kutokana na Uingereza, ambayo iliwapa azimio la Balfour mnamo mwaka wa 17 kuifanya Palestina kuwa nchi ya kitaifa ya Wayahudi.

Uingereza yote ilikula njama dhidi yenu ni kama ilivyokula njama dhidi ya Waislamu duniani kote, ilikula njama dhidi ya Waarabu na ilitaka kuwadhalilisha Waarabu kwa sababu iliamini kuwa unyonge wa Waarabu ni udhalilishaji wa Uislamu duniani kote.  Uingereza iliwapa Palestina kwa Wayahudi, na ikaondoka mnamo Mei 15, 1948, wakawaacha Wapalestina iliopewa mamlaka kwa njia ya Umoja wa Mataifa baada ya Vita Kuu ya Kwanza … iliwaacha kama mawindo rahisi kwa Uzayuni wa kimataifa, kuwaua na kuwahamisha hadi zaidi ya milioni moja ya wakiarabu waondoke Palestina.

Baada ya yote, Uingereza ndiyo hasa inayohusikwakiamambo haya,ni Uingereza iliyotaka kudhoofisha ulimwengu wa Kiarabu, lakini leo hii tulipoishinda Uingereza, tunajua nguvu zetu ni nini na tunajua kwamba ulimwengu wa Kiarabu kila mahali na kila sehemu yake wanaweza kuja pamoja, kuungana, na kukabiliana na ukoloni; ndiyo maana mkutano wa kilele uliweka masharti kwamba tukabiliane na Israel, uliweka masharti kwamba tuanzishe uongozi wa umoja kwa ajili ya majeshi ya Waarabu, ikaweka masharti kwamba tofauti kati ya taifa la Kiarabu ziondolewe, na ikaweka Iliweka bayana kwamba itaondoa utofauti kati ya taifa la Kiarabu, na kueleza kwamba itapiga marufuku utangazaji na kuzuia mashambulizi kati ya nchi za Kiarabu, tulikuwa tumejitolea katika hili, na tulikuwa tumejitolea kwa kila kitu kilichoelezwa katika Mkutano wa Marais na Wafalme wa Taifa la Kiarabu.

Rais Ahmed Bella na Rais Abdel Salam Arif walichukua hatua bora. Ushindi wa Abdel Salam Arif huko nchini Iraq ulikuwa ni ushindi kwako, ulikuwa ushindi wa utaifa wa Waarabu, Ushindi wa Mapinduzi ya Waarabu, Ushindi wa Uhuru wa Waarabu.

Wakati wa Abdul Salam Arif alipofanya mapinduzi ya hivi karibuni ya Ahrar mnamo Novemba 18 huko Iraq, tulihisi kwamba nguvu ya Waarabu ilikuwa imeongezeka kwa Abdul Salam Arif na mapinduzi ya Abdul Salam Arif, na wakati Abdul Salam Arif na Abdul Salam Arif ndugu zake walipopata ushindi, tulihisi kwamba Mungu atatusaidia huko nchini Misri na kwamba Mungu atatushinda huko Yemen ; kwa sababu Baath walitukabili na kufuata mpango wa kikoloni dhidi ya utaifa wa Waarabu, dhidi ya taifa la Kiarabu, na dhidi ya mapinduzi ya Waarabu, na wakati Abdul Salam Arif aliposhinda na kuishinda Baath huko Iraq, hii – ndugu – ilikuwa ushindi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwao pahali popote.

Ningependa kuelezea kuwa ushindi wa Abdel Salam Arif,  ambaye ni shujaa huru na mwanamapinduzi … shujaa wa Kiislamu wa Kiarabu … mtu aliyeinua bendera ya utaifa wa Kiarabu mnamo 1948. Siku ambayo Abdel Salam Arif alishinda mnamo mwezi wa Novemba, nilimshukuru Mungu kwa moyo wangu wote. Kwani nilijua kuwa ushindi wa Abdel Salam Arif ni ushindi wa watu huru kila mahali, ushindi wa mapinduzi kila mahali, ushindi kwako hapa Taiz.. Ushindi kwako hapa Sanaa.. Ushindi kwako hapa Yemen, yenye mapinduzi huru. .. Ushindi kwetu Misri.

Abdul Salam Arif alitembea katika njia ya utaifa wa kiarabu, njia ya uhuru, na njia ya uhuru, Mungu alikuwa ametupa ushindi kabla ya hapo kwa kumuunga mkono Ahmed bin Bella huko Algeria.Algeria ilipopata uhuru na Ben Bella kushinda Algeria, tulimshukuru Mwenyezi Mungu kwa mioyo yetu yote; kwa sababu tuliona kuwa ushindi wa Algeria ni ushindi kwetu, na kwamba mapinduzi ya Ben Bella huko Algeria ni mapinduzi kwenu hapa Yemen na hii ni mapinduzi kwetu huko nchini Misri, na ni mapinduzi kwa wanamapinduzi wote wa Kiarabu na Waarabu wote huru.

Kwa hivyo tulikutana kwenye mkutano huo, na baada ya mkutano huo, Abdel Salam, Arif, na Ahmed bin Bella walituma wajumbe wawili mjini Kairo, kisha Makka na Riyadh, ili kutatua utofauti kati ya Misri na Saudi Arabia, na kuondoa njama ambazo ukoloni ulitaka kueneza miongoni mwa watu. Juhudi hizi za kusifiwa za Ahmed bin Bella na Abdel Salam Arif ziliweza kugusia mioyo yetu na mioyoni mwa Mwanamfalme Faisal huko Saudi Arabia, na baada ya hapo akaenda Field Marshal Abdel Hakim Amer na Bwana Anwar Sadat kwenda Saudi Arabia, na lengo lao kufanya hivyo lilikuwa ni kuihakikishia Saudi Arabia kwamba hatuna nia mbaya dhidi ya watu wa Saudi Arabia, kwa kuwa wao ni ndugu zetu.. ni Waarabu.. Ni Waislamu, na sisi ni wao daima.. Sisi ni nguvu zao zinazowasaidia kwa hali zote na katika hali zote, nyinyi pia … nyinyi ni Yemen, nguvu inayosimama kwenye mipaka yao na kuwaunga mkono katika hali zote na nyakati zote. Sisi pia – ndugu – hatuhifadhi ubaya wowote kwa Mwarabu yeyote, bali tunataka wema, fahari na utu kwa Waarabu wote, lakini tunakabiliana na mawakala wa ukoloni ; kwa sababu ya mawakala wa ukoloni ni  maadui dhidi ya taifa la Kiarabu, tunatakia enzi mpya ya  upendo, udugu na maridhiano  ianzishwe kati yetu na Saudi Arabia ili tusije tukaupa ukoloni wa Kiingereza fursa ya kueneza mgawanyiko na mifarakano kati ya taifa la kiarabu.

Jana, ndugu zangu, nilishangaa sana niliposikiliza hotuba ya watawala wa Baathi huko nchini Damascus, waliposema: Misri inahusika na mapinduzi yanayotokea huko nchini Syria sasa : inamaanisha kuwa watu wa Siria si watu mashujaa, watu wa Syria siku zote wamekuwa watu mashujaa wasioogopa risasi, hawaogopi kifo, wala hawaogopi mateso, wananchi wa Syria hawajawahi kuhitaji, Mtu wa kuwahamasisha kufanya mapinduzi.Watu wa Syria wamekuwa watu wenye uhuru  daima, Hawasubiri kupa ari ili kufanya mapinduzi,wala hawangojei uchochezi ili kutekeleza mapinduzi.Wananchi wa Syria hawajawahi kukubali kudhalilishwa, wala hawakukubali Aibu, watu wa Syria waliopoteza mamia ya majeruhi katika wiki zilizopita, ndio walioasi; kwani hawakubali udhalilishaji wa Baathi na hawakubali kudhalilishwa na Wabaath, watu wa Syria wenye majivuno walioishinda Ufaransa na kuikabili kwa vifua visivyo na ulinzi kamwe hawaogopi na hawangoji mtu awafadhili kwa pesa na hawangoji mtu anawafadhili kwa silaha. 

Najua juu ya siku chache zilizopita kwamba watu wa Syria wasio na ulinzi walitoka nje na kupokea risasi za vifaru vifuani mwao, risasi za vifaru  mioyoni mwao, na mabomu ya vifaru yaliyozukia majumbani mwao, hakuwa na mtu anayemsaidia isipokuwa Mwenyezi Mungu, nguvu ya imani yao juu ya haki yao ya uhuru na maisha na haki yao ya kufanya jukumu lake huru  lakini watawala wa Syria kutoka Baathi walitaka kuwatukana watu wa Syria tusi lingine, kwa hiyo walisema jana kwamba Misri iliwapa pesa, na wanasema uwongo; wanamdanganya Mwenyezi Mungu, wanajidanganya wenyewe, na wanawadanganya watu wa Syria.Watu wa Syria sio watu wanaopokea pesa; Kwa sababu ni watu wa watu huru, mapinduzi ya mahali popote hayawezi kufanywa kwa pesa,mapinduzi ya mahali popote yanaweza kufanywa tu kwa imani. Imani ya Mwenyezi Mungu, imani ya nchi ya asili, na imani ya uhuru.

Wakati Syria ilipoasi huko mtaa wa Hama na ilipokabiliana na vifaru, na ilipoinuka Hams na ilipokabiliana na vifaru, na ilipoasi Aleppo na ilipokabiliana na mizinga, na ilipoasi Damascus na Daraa na Deir Al Zor na kukabiliana na mizinga na ndege, haikuwa ikifanya hivi kwa malipo yanayojulikana, kama watawala wa Baathi wanavyosema; Lakini walifanya hivyo kwa sababu wanamwamini Mungu, wanajiamini, na wanaamini katika haki yao ya uhuru na uhai.

Kwa mara ya kwanza, leo nazungumza kwa sababu watawala wa Baathi huko Syria jana walikiuka kile kilichoamuliwa na Mkutano wa Marais na Wafalme wa Kiarabu na walituhumu hadharani na kumtukana Abdul Salam Arif.Tulikuwa tunasikia matukio huko Syria huku mioyo yetu ikiwa  tukichuruzika damu, lakini tulinyamaza kwa kusitasita kwa sababu tulikuwa tunazingatia kile ambacho Mkutano huo uliamua. Lakini baada ya watawala hawa wa Baathi – siku hizi au jana – kufuta uamuzi huu ulioamuliwa na mkutano wa kilele, tunajiuliza: Kwa nini walibatilisha? Je, wanashirikiana na Uingereza? Tuko katika vita na Uingereza. Je, wao ni mawakala wa Uingereza hadi wasimame wakati huu kuunga mkono Uingereza na kueneza fitina na migawanyiko kati ya sehemu za taifa la Kiarabu, na kuharibu maamuzi ya mkutano wa kilele ?

Jana nilipopokea ripoti hiyo, shutuma hii, na matusi haya huko Misri, dhidi ya Abdel Salam Arif, na Iraq, nilihisi kwa mara ya kwanza kwamba kuna uhusiano kati ya kile kinachopangwa huko Aden na kile kinachopangwa huko Damascus, na kwamba kuna uhusiano unaopamgwa na Waingereza wa kikoloni na watawala vibaraka wa kusini iliyokaliwa, uhusiano na kile Jana, kilitangaza kauli za watawala wa Baathi wa Damascus. Je, kuna ajira inayohusika? Au watawala wa Syria wanataka Wabaath wawapotoshe na kuwahadaa watu wa Syria? Watu wa Syria hawawezi kupotoshwa.Waarabu hawawezi kupotoshwa.Je, Uimamu uliweza kukupoteza? Kamwe, mlikuwa mmedhamiria na Je, mliasi kwa sababu tu mlimwamini Mungu na kuamini haki yenu ya uhuru na maisha?

Huu ndio uelekeo wa wanamapinduzi wa Syria.Tunatumai kwa Syria,  Syria ndugu, Syria mpendwa, , Mungu ataiepusha na ugaidi huu, unyonge huu, na unyonge huu. Tunawaunga mkono watu wa Syria walio huru, mashujaa kwa nguvu zetu zote na kwa roho zetu zote, tunawaunga mkono kwa maadili, lakini hatuwalipi pesa. Kwa sababu tunajua kwamba wanaochukua fedha hawawezi kuwa wanamapinduzi. 

Enyi ndugu walio huru:
Mliomba umoja wa Waarabu na ningependa kuwaambia kuwa Umoja upo kwelikweli Umoja upo kati yetu na nyinyi… Umoja huu upo kati yetu na nyinyi.

Enyi Ndugu , ndugu wapendwa
Nilisema haya jana kwa Rais Sallal, Tangu siku ya kwanza ya mapinduzi, umoja huu ulikuwepo kweli kati sisi na nyinyi, lakini sio umoja wa mapatano na sio umoja wa katiba, badala yake, ni umoja wa damu. Damu ya Wamisri ilimwagika pamoja na damu ya Yemeni hapa milimani, mabondeni, na mipakani.Huu ndio umoja wetu, umoja wa mioyo… umoja wa damu.Umoja wa imani…umoja wa lengo. Nilishawahi kusema kuwa hatutaweza kufikia umoja wa maandishi kabla ya kuisha operesheni  za kijeshi, na kabla ya majeshi ya Misri kurejea, lakini nakwambia umoja upo kweli.

Enyi ndugu wapendwa,  walio na uhuru, wananchi wapendwa, ndugu wanamapinduzi, na ndugu huru:
Leo nimeona nguvu zako, kama nilivyoziona jana nguvu za ndugu zako huko Sanaa, niliona nguvu za watu wa Yemeni, na nimefarijika sana juu yenu na mapinduzi yenu, basi kwenda mbele kwa baraka za Mungu, na Mungu ndiye msaidizi wenu na Mungu awape mafanikio.

Wassalamu Alaikum warahmat Allah.

Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy