Tatizo la Palestina, kwa maoni yetu, kwanza ni suala la haki za Waarabu wa Kipalestina

Tatizo la Palestina, kwa maoni yetu, kwanza ni suala la haki za Waarabu wa Kipalestina

   Swali la Mhoji:

 " Mheshimiwa Rais, utafanya nini ikiwa wafanyikazi wa bandari huko Marekani wangeendelea kususia meli za Kiarabu? "

  Rais Nasser : "Naona kwanza kabisa kwamba suala hili ni kinyume na maslahi ya Marekani na Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu sawa, na tumefanya kazi mnamo miezi iliyopita kuboresha uhusiano kati ya nchi zetu, tulijaribu kusahau yaliyopita, lakini tulishangazwa na tukio hili.

  Na Msimamo wa Serikali kuhusu hilo bado unajadiliwa, lakini kwa hakika umeona kwenye magazeti msimamo wa wafanyakazi wa Kiarabu kuelekea hilo, na nadhani wafanyikazi wetu waliliona tukio hilo kama hatua ya kiuadui dhidi ya nchi yao, ambayo iliathiri maslahi yake, na heshima yake. "

Ni wazi kuwa sisi katika Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu tuna jukumu muhimu la kuhifadhi uhuru wetu, pamoja na ukuu wetu. Na ikiwa sisi si nchi kubwa, tuna nguvu za mali zinazotisha; kwa nguvu zetu za kimaadili, ya kwanza ambayo ni chanya katika kukabiliana na matatizo; tunaweza kupaza sauti zetu kwa kiasi kikubwa na kwa heshima katika kila jambo linatokea kwetu.

 Swali la Mhoji: Ikiwa ingechukuliwa - Mheshimiwa Rais - kwamba Wafanyikazi wa Kiarabu waliamua kususia meli zote za Marekani, je, serikali yako ingeunga mkono au kupinga uamuzi huu?

Rais Nasser: nilisema kuwa serikali inalichunguza suala hilo kwa kina.

 Swali la Mhoji: Je, Mheshimiwa unaweza kututajia kwa nini haswa unazuia meli za Israeli kupita kwenye Mfereji wa Suez? Na ni masharti gani unayodai kutoka kwa Israeli ili kuondoa kizuizi hiki?

 Rais Nasser: Suala la kupitishwa kwa meli za Israel kwenye Mfereji wa Suez ni sehemu ya tatizo la Wapalestina, na lilianza mwaka 1948. Tatizo hili liliwasilishwa kwa Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama, na maazimio kadhaa yalichukuliwa kuhusiana na suala hili, na miongoni mwa maazimio hayo ni azimio lililowataka wakimbizi hao wa Kiarabu kurejea makwao, na kuwalipa fidia kwa hasara iliyowapata. baada ya kufukuzwa katika nchi yao na kunyang'anywa mali zao na kila kitu katika nchi yao Palestina.

 Lakini nini kilifanyika baada ya maamuzi haya? Israel ilikataa kutekeleza lolote kati yao, na ikatangaza kwamba haitamruhusu Mwarabu yeyote wa Palestina kurejea makwao. Ama Waarabu walisisitiza juu ya ulazima wa kutekeleza maazimio haya yaliyotolewa na Umoja wa Mataifa. Sio tu kwamba Israeli ilikataa maazimio yote ya Umoja wa Mataifa; Pia ilidai matumizi ya Ghuba ya Aqaba, ingawa maji yake ni maji ya eneo la Waarabu kweli, na ilidai matumizi ya Mfereji wa Suez.

Kuna maoni ambayo ningependa kusema kuhusu hili; nayo ni kwamba magazeti ya Marekani yalipuuza haki za Waarabu wa Palestina,na yalianza kuzingatia maombi ya Israeli, ikiwa ni -kama nilivyosema -hamu/matumaini yake ya kutumia Mfereji wa Suez. Hata hivyo, tunaona bidhaa na mali ambazo Israeli inataka kutumia Mfereji wa Suez kuwa mali ya Waarabu؛Kwa sababu Israel iliwanyima Waarabu wa Palestina mali zao, ardhi zao na kila kitu.

 Swali la Mhoji: Mheshimiwa Rais, unaweza kuniruhusu kutoa maelezo? Je, unamaanisha kwamba marufuku iliyowekwa kwa meli za Israel kupitia Mfereji wa Suez inahusu pia meli za Israel zinazotoka Afrika Mashariki na kuelekea Israel kupitia mfereji huo?

Israel imekuwa ikiuza kiasi cha nyama kutoka Afrika Mashariki kwa miaka mingi,na kusafirisha kwa meli ambazo zina jokofu maalum,na zinazopandisha bendera tofauti na bendera ya Israeli.Je, una pingamizi lolote la kupita kwa meli hizo kwenye mfereji huo?

Rais:Tunaichukulia mali yote ya Israel kuwa ni mali ya Waarabu wa Palestina walionyang'anywa ardhi na mali zao,shehena zilitwaliwa zikielekea Israeli,na miongoni mwa meli hizo ni meli iliyokuwa imebeba shehena ya nyama iliyoagizwa kutoka Eritrea.Shehena hiyo imechukuliwa;kwa sababu tunaiona kuwa ni mali ya Waarabu, iliyotekwa na Israeli.

 Swali la Mhoji : Ikiwa anwani ya shehena itabadilika kabla ya kusafirishwa kutoka Israeli; ili itangazwe kuwa mtu asiye Mwisraeli ameinunua, je, unaingilia shehena hiyo na kuzuia kupita kwenye Mfereji wa Suez?

Rais Nasser : Suala si suala la anwani, -kweli- ni suala la kumiliki ,na tunachukulia kila kitu ambacho Israeli inamaliki ni haki ya Waarabu , Israeli inaichukua kutoka Waarabu kwa nguvu na bila haki.

 Swali la Mhoji: Mheshimiwa Rais .. ningependa kuthabitisha kutoka ninaelewa Maoni yako katika suala hili.. Je , unamaanisha wewe utaendelea kuzuia meli za Israeli kutoka kupitisha kwenye Mfereji wa suez ikiwa tatizo la wakimbizi wa wapaleatina lanaendelea?

 Rais Nasser : tatizo la Palestina tuliangalia kwanza ni suala la haki waarabu wa wapalestina , Ilimradi haki hizi hazirudishwi kwao, ilimradi hakuna nafasi kwa kutekeleza maamuzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki hizo, basi sisi hatutaruhusu kwa meli za Israeli kwa kutumia mfereji wa Suez.

 Swali la Mhoji : Mheshimiwa Rais, baadhi ya idara katika Umoja wa Mataifa zilieleza wazi kwamba "Monsieur Hammarskjöld" alipotembelea Kairo hivi karibuni, mlijadili pamoja tatizo la kupitisha bidhaa za Israel kupitia Mfereji wa Suez, na kwamba mlikubaliana naye. sio kuzuia bidhaa hizo kupita kwenye mfereji ikiwa zilisafirishwa kwa meli za  upande wowote, na bado umesimamisha meli zisizo za Israeli zinazobeba bidhaa za Israeli, tafadhali tuambie ikiwa tayari umekubaliana na "Monsieur Hammarskjöld" juu ya utaratibu kama huo ?

Rais Nasser: Hakuna makubaliano yoyote na "Monsieur Hammarskjöld" kuhusu suala hili, na moja ya magazeti lilichapisha ulichotaja katika swali lako, lakini jibu  lilitolewa na  "BiBi Golda Meir" - Waziri wa Mambo ya Nje wa Israeli - kama alivyosema wakati wa ziara yake Amerika Kusini Agosti iliyopita kwamba jambo hili lilikubaliwa kati ya "Hamarskjöld" na Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu, lakini ukweli ni kwamba hatukukubaliana hili, na tulilikataa, na yote ambayo Waisraeli walitaka - inaonekana - ilikuwa ni kujaribu kutumia habari hizi za uwongo kama propaganda dhidi yetu katika nchi za Kiarabu, lakini umati wa watu wa Kiarabu hawaamini yoyote kati ya hizo tena.

  Swali la Mhoji: Mheshimiwa Rais, moja ya kamati za Jumuiya ya nchi za  Kiarabu hivi karibuni ilipendekeza kuanzishwa kwa  Muungano wa  Palestina na jeshi la Palestina. Hii ina maana kuwa Muungano huo wa Palestina na jeshi hili la Wapalestina utaanzishwa  kwa gharama ya Jordan.

Je , hamuoni kwamba hili ni jaribio la kuharibu mshikamano wa Waarabu badala ya kuuimarisha na kuuunga mkono?

Rais Nasser: Sidhani kama lengo lolote   miongoni mwa malengo yetu litatekelezwa dhidi ya mshikamano wa Waarabu, au kukusudia kuwa kitendo cha uadui dhidi ya maslahi ya nchi yoyote ya Kiarabu. Madhumuni ya kuanzisha muungano wa Palestina ni kukabiliana na shughuli za Israel za kumaliza tatizo la Palestina, na kupoteza haki za watu wa Palestina. Ama kuhusu jeshi la Palestina, lengo lake kwa hakika ni kutetea haki za Waarabu wa Palestina, na hilo ni jambo la kimaumbile na la kimantiki. Kutokana na hili ni wazi kwamba sio moja ya malengo yetu hata kidogo kuibua matatizo yoyote  , au kuchukua hatua yoyote,  inayohusika na nchi yoyote ya Kiarabu.

Swali la Mhoji: Mheshimiwa Rais, unafikiri kwamba Mfalme Hussein - Mfalme wa Jordan - ana mipango ya wakati ujao?

 Rais Nasser: Kwa kweli, siwezi kuangalia suala hili kwa njia hii. Kuna tofauti kati ya fikra za uandishi wa habari na fikra za mkuu wa nchi anayehusika na kauli zake kuhusu masuala ya kimataifa. Bila shaka, tunashughulika na Mfalme Hussein akiwa Mfalme wa Yordani, na tunajaribu kuwa na mahusiano mazuri naye, lakini hatimaye tulikabili matatizo fulani. Kwa sababu Mfalme wa Yordani na serikali yake wamekuwa wakiendesha kampeni za uhasama dhidi yetu, wakidhani kwamba kupitia njia hii wanaweza kuongeza nafasi zao na baadhi ya nchi kuu ambazo zina maslahi katika Mashariki ya Kati, lakini kwa kweli siwezi - kwa njia yoyote- kujadili swali kama hilo, ambalo ni kama Mfalme Hussein ana wakati ujao au la, nadhani mtu yeyote anaweza kujibu swali kama hilo.

 Swali la Mhoji : Je, unadhani katika mazingira gani - Mheshimiwa Rais - inawezekana mchakato wa kumuunganisha Mfalme Hussein na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu ufanyike, kulingana na ulivyosema ungependa? Ni nini kinachohitajika ili hili lifanyike?

 Rais Nasser: Ni wazi kwamba tunachoomba kwa serikali ya Jordan ni kufanya kazi kwa ajili ya mshikamano wa Waarabu na sio kufanya kazi dhidi yake. Maadamu serikali ya Jordan inafanya kazi dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu; Ni vigumu kutoa fursa ya kuanzisha mahusiano mazuri kati yetu na serikali ya Jordan.

 Swali la Mhoji : Je, hii inatumika kwa Iraq?

Rais Nasser: Ndiyo.

Swali la Mhoji :

Mheshimiwa Rais... Je, hujisikii hata kidogo kuhusu hali ya Iraq, baada ya Jenerali Qassem alikataa kutambua chama cha kikomunisti chini ya maagizo ya Moscow na alitosha kutambua chama cha kikomunisti hakijali kuridha "Comintern"Je, hii inaonekana kama ishara ya kuboreka kwa hali ya Iraq?

 Rais Nasser: Hili sio tatizo kuu kamwe; tatizo kuu kwetu ni sera ya serikali ya Iraq  wakati wa muungano wa waarabu na msimamo wake kuhusu masuala ya Waarabu, hivyo ni katika kipaumbele cha kwanza ni inaamua msimamo wetu juu ya serikali yoyote katika nchi yoyote ya Kiarabu.

 Swali la Mhoji: kwa kutaja suala la Kujipenyeza kwa Kikomunisti katika mashariki ya Kati,ni Kuna kipengele kingine ambacho nataka kuonesha kwako Mheshimiwa; serikali ya  huru ya Algeria iliomba watu wa kujitolea kujiunga na jeshi lake kama unavyojua Je, serikali yako itakuwa na msimamo kuelekea wajitolea wowote kutoka Jamhuri ya  China  wanataka kuja kwa mashariki ya Kati kama wajitolea katika Jeshi la Algeria?.

 Rais Nasser: kwa maoni yangu  ni lazima kwa Watu wa Algeria kupata Uhuru, na hatutapinga njia anayofuata kupata uhuru.

 Swali la Mhoji: Sielezi suala la uhuru wa Algeria Mheshimiwa  Rais, lakini nieleza suala la kuja kwa Wachina kama wajitolea na ushiriki wao katika Harakati za uhuru wa Algeria?

 Rais Nasser:  ndani ya jeshi la Ufaransa linajumuisha   wanajeshi kutoka Ujerumani na nchi zingine, kwanini ulipingana na haki za Waalgeria kujiunga jeshi lao  kama wajitolea kutoka nchi zote, miongoni mwa China?!Sioni sababu ya kupinga.

 Swali la Mhoji: Huoni_Mheshimiwa Rais _ Kuna jambo kwa Mashariki ya Kati kuhangaikia kuhusu suala hili?

 Rais Nasser: Nina hakika hakuna watu wa kikomunisti wanaweza kuathiri _chochote kitakachotokea _ kuhusu Utaifa wa Kiarabu nchini za Kiarabu, ikiwemo Algeria  bali kinyume nina hakika kwamba mawazo ya Utaaifa wa kiarabu utadumu mwishoni na milele.

Swali la Mhoji: hatuoni_ Mheshimiwa Rais _ Hili linachukuliwa kuwa jaribio la kuingilia kijeshi la kikomunisti,msingi wake ni wajitolea kwa Algeria  kwenda  Jamhuri ya china au Umoja wa Kisovyeti  Uingizaji wa kikomunisti wa kijeshi una hatari kuhusu ulimwengu wa Kiarabu ?

 Rais Nasser : niliona tatizo la Algeria kuwa ni tatizo la nchi na wananchi.Watu milioni moja wa Algeria wameuawa katika mapinduzi ya Algeria ; yaani 1/10 ya watu wa Algeria waliuawa hivyo nilidhani ikiwa wananchi wa Algeria walipata msaada wowote; msaada huo  utaokoa milioni ya watu hawa kutoka uharibifu.

 Ama kile kinachohusiana na maoni yangu katika suala la Kujipenyeza kwa Kikomunisti; nataka uangalie , kwa mfano, Misri na Syria, Uko wapi huo upenyezaji wa kikomunisti?!

Magazeti ya Marekani yaliyotangaza kwa muda mrefu " sisi pamoja na ushawishi wa kikomunisti,na yalizidi pia sisi tunakabiliana hatari za upenyezaji wa kikomunisti; kwa sababu mikataba ya silaha ambayo tuliyifanyiwa  pamoja na nchi za kikomunisti na sababu ya Uhusiano wa kiuchumi pamoja nchi hizi, lakini yale yaliyotangazwa na magazeti hayo ni ya kweli?

 Swali la Mhoji: Mheshimiwa Rais... Ulirudia kutoka ziara ya India na Pakistan, hivyo Je, una maoni gani kuhusu Mkataba wa zamani wa Baghdad uliojulikana sasa kwa jina la mkataba mkuu?unaona ni kama tishio kwa Umoja wa Kiarabu.

Rais Nasser:ninakuomba kwanza mkumbuke kwa sababu gani tulipiga Muungano wa Baghdad,na tishio gani ambalo Muungano huo ulikuwa nao kwetu,baada ya kuanzishwa ,nchi za kiarabu ziliitwa na kujiunga nayo na tulipokataa,tulianza kukabiliana na njama,na tulianza jukabiliwa na aina mbalimbali ya shinikizo,tulikataa kushiriki katika Muungano tangu mwanzo,kisha majaribio yalifanywa kutulazimisha kushiriki katika huo,ambalo lilifanyka-kama mnavyojua-kwa kiwango cha kila aina ya vizuizi,na hata kusababisha uchokozi.nilijadili suala la Muungano huo na Rais "Ayoub Khan"na nilizungumza naye kuhusu njama zote za Muungano huo didhi yetu,na nilimweeleza jinsi ya nchi za muungano kwa mfano,haswa Uingereza-zilipa 160,000-mmoja wa marubani  katika jeshi letu la anga.kwa ajili ya kufanya mapinduzi didhi ya serekali yetu,kama nilivyosimulia na "Ayoub Khan"jinsi ya nchi za muungano zilifanya kampeni ya propaganda didhi yetu,Rais "Ayoub Khan"alinihakikisha kuwa hakuna chochote kati ya haya kitakachotokea mnamo siku zijazo,na hakuwa na maarifa ya chochote kinachoendelea dhidi ya nchi yetu,na msimamo wa nchi za Muungano sasa ni kuutumia kama Muungano wa ulinzi tu,sio kama chombo cha kutekeleza hatua yoyote ya uadui.

 Ikiwa shirika jipya - yaani muungano unaojumuisha Uturuki, Pakistani na Iran - ni shirika la ulinzi na halina sera yoyote ya uadui dhidi ya nchi nyingine za Kiarabu;basi tunaweza kuanzisha mahusiano ya kirafiki na nchi hizi huko tukihifadhi maoni yetu Muungano kwa ujumla.

 Swali la Mhoji:  Mhe Rais, Je ulijadiliana na Rais?Ayub Khan, hatua zozote za ulinzi za pamoja?

 Rais Nasser :Kweli naamini kuwa unajua maoni yetu kuhusu hatua za ulinzi,tunapinga ushirikiano wa kijeshi; kwa sababu tunahisi kwamba shirika lolote la kijeshi ambalo ndani yake kuna nchi kubwa litaiwezesha nchi hii kuweka udhibiti wake juu ya nchi ndogo, hasa kwa vile nchi ndogo haziwezi - kwa njia yoyote - kuwa sawa na nchi kubwa katika mashirika au miungano kama hiyo. Kadhalika, hatuamini kuwa kambi za kijeshi ndiyo njia sahihi ya kudumisha amani.

 Swali la Mhoji: Mhe Rais, inawezekana kurudi kwenye suala la Mfereji wa Suez? Suala hili linahusiana na azimio lililopitishwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1951 kuhusu Uhuru wa kusafiri katika Mfereji wa Suez.Kulingana na maelezo yangu, natambua kuwa Mhe alitangaza Julai iliyopita kuwa uko tayari kutekeleza uamuzi huu, ikiwa Israeli ilijitolea. kutekeleza maazimio ya Umoja wa Mataifa yaliyoelekezwa kwake.Je, huu bado ni msimamo wako?

 Rais Nasser: Ndiyo, maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusiana na haki za watu wa Palestina lazima yatekelezwe kabla ya jambo lolote lile.

 Swali la Mhoji: Mheshimiwa pia alisema katika mahojiano nawe kama miezi 6 iliyopita - yaani, Oktoba iliyopita - kwamba ikiwa Umoja wa Mataifa utaanzisha kamati au chombo maalum cha kutekeleza hili jambo ni mtashirikiana nao.

Rais Nasser:Ndiyo,Umoja wa Mataifa umeanzisha kamati ya Tawfik mnamo 1949 kamati hiyo iliyoundwa na Ufaransa, Uturuki na Marekani, tena imefanya mkutano katika Lausanne, na mwakilish wa Israeli na wakilishi wawili wa mataifa ya kiarabu walishiriki katika mkutano huo .watu wote  walijadili jinsi  ya utekelezaji wa maamuzi ya Umoja wa Mataifa, kisha Israeli ilikubaliwa katika uchama wa umoja wa mataifa.katika siku ya pili mwakilishi wa Israeli alikata kuendelea ushirika katika  mikutano ya kamati hiyo.

  Suala la kimsingi ni la haki za waarabu wa Palestina.Na Israeli inajaribu kwa njia zote  na kila aina za matangazo,kufanyika ulimwengu kusahau haki za waarabu wa Palestina.Ni waarabu milioni waliofukuzwa kutoka nchi zao na kunyimwa kila kitu.Israeli hujaribu kuzingatia juhudi na shughuli zake katika nia yake  ya kutumia mfereji wa Suez.

 Swali la Mhoji: Msimamo wenu bado Umoja wa Mataifa ukianzisha kamati au taasisi nyingine badala ya kamati ya Tawfik, Je tayari kushirikiana na kamati au taasisi mpya?

 Rais Nasser:Hiyo kweli..tuko tayari kushirikiana ili kutekeleza maamuzi ya Umoja wa mataifa kuhusu haki za waarabu wa Palestina. Nchi zote za kiarabu zilikubali hiyo katika mkutano wa Bandung, pamoja na hiyo nchi zote za Asia na Afrika. Na tumeeleza hii  wazi katika taarifa tulizitoa nchini India. Katika repoti ya  pamoja iliyotolewa baada ya ziara yetu nchini India, Na pia repoti ya pamoja iliyotolewa baada ya ziara yetu nchini Pakistan.

Swali la Mhoji: Je hii itakuwa na kitendo haraka  kutoka Umoja wa mataifa au kutoka Israeli?

 Rais Nasser: Waisraeli walitangaza kutakata kutekeleza maamuzi ya Umoja wa Mataifa.

Swali kutoka kwa Mhoji: Mheshimiwa Rais, Je, mnaondoa vikwazo vilivyowekwa katika kupitisha meli na bidhaa za Israel kwenye Mfereji wa Suez wakati wa uanzishaji wa kamati au mamlaka hicho, ikiwa imeleta kujadili suala hilo?

Rais Nasser: Ndio, kama Waarabu wa Palestina walipewa fursa wakati huo wa kurudi makwao, lakini ni wazi kuwa Israel haikubaliani na haki ya Waarabu wa Palestina kurejea katika nchi zao.

 Swali kutoka kwa Mhoji: Mheshimiwa Rais, Waziri Mkuu wa Israeli amesema mara nyingi kwamba anafurahi sana kukutana nawe katika sehemu yoyote utakayochagua, ikiwa ni pamoja na Kairo. Ili kujadili na wewe matatizo ya msingi, na sina uhakika kwamba ulijibu kwa kukubali kuonana naye, kwa hiyo heshima yako ingetupa fursa ya kurekodi majibu yako kwake?

 Rais Nasser: Alijijibu mwenyewe, na unaweza kukumbuka kwamba alikuwa kwa siku saba kabla ya uvamizi wa pande tatu dhidi ya nchi yetu katika mwaka wa 1956; "Bwana Ben-Gurion" alikuwa amesema kwamba anatafuta amani, na angependa kukutana nami ili kujadiliana kuhusu mkataba wa suluhu, lakini alitoa kauli hii wakati alipokuwa akifanya njama na Uingereza na Ufaransa kuanzisha uchokozi. na shambulio la nchi yetu, na jana mwakilishi wa Israeli huko Yugoslavia alisema kitu kama hiki. Waisraeli wanajaribu tu kupotosha maoni ya umma ya ulimwengu; Wanasema wako tayari kufanya mazungumzo na Waarabu, kukaa nao kwa nia ya kufikia suluhu nao, lakini kwa sharti moja; Ni kwamba Waarabu wasiwe na masharti yoyote!.. Hii ina maana gani? Ina maana kwamba Waisraeli wanataka kweli tusahau maazimio yote ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za Waarabu wa Palestina.

 Swali kutoka kwa Mhoji: Kwa hivyo huoni faida ya mkutano kati yako na Ben-Gurion?

Rais Nasser: Sijui unawezaje kukutana na mwanaume usiyemwamini, mtu ambaye alitangaza kuwa yuko tayari kukutana na wewe ili kujadili mkataba wa maridhiano wakati alipokuwa akipanga njama ya kukuua wewe na familia yako.

  "Bwana Ben-Gurion" alitangaza siku saba kabla ya uchokozi wake kwamba alikuwa tayari kujadili mkataba wa amani, lakini kwa kweli alikuwa akijiandaa kwa vita. Hiyo ilitokea mnamo 1956.

Swali la Mhoji : Mhe Rais, hili lilitokea wakati wa mapambano ya urais katika Marekani, ambalo linawatatiza wanaogombea kwani walipasua kuahidi na kuhusishwa kwa njia moja au nyingine, hili litarudia mwaka huu.. mwaka wa 1960?

 Linalonihusisha, jambo hilo halitakuwa mshangao kwangu, Sitashangaa kama Jenerali Mkuu akiniambia siku moja kwamba Waisraeli walianza kuvamia nchi yetu kwani hii imekuwa hali mnamo miaka saba iliyopita.

 Swali la Mhoji : Mhe Rais, nadhani kwamba serikali yenu mnamo mwaka wa 1958 mwezi wa Agosti, ilitia saini makubaliano ya kibiashara pamoja na serikali ya Cuba, yaliyosema kwamba kubadilishana bidhaa za kutumika, na bidhaa 21 ziliitwa kwa majina, lakini lililobayana kwamba lilitajwa katika makubaliano : " na bidhaa nyingine", zaidi ya hizo zilizotajwa kwa majina, " bidhaa nyingine" zinamaanisha silaha za kujitetea kwa aina gani?

 Rais : Kwa hakika, makubaliano hayakutaja silaha zozote, na serikali ya Cuba haikutuomba silaha za kujitetea zozote, na nadhani kwamba makubaliano ya kibiashara hayajumuisha silaha za kujitetea, kwani silaha za kujitetea zinahitaji majadiliano maalumu.

 Swali la Mhoji: Mnadhani kwamba majadiliano ya kipekee kama hayo yatafanyiwa kati yenu na serikali ya Cuba?

 Serikali ya Cuba ikituomba hilo; tutazungumza suala hilo, na tuwe makini kuhusu mahitaji yake.

 Swali la Mhoji : Iliripotiwa - Mhe Rais - kwamba kuna makubaliano ya silaha yalishasainiwa kati yenu na Cuba, hii ni kweli?

Hapana, sidhani kwamba hii ni kweli

 Mazungumzo ya Rais Gamal Abdel Nasser yaliyotolewa kwa wajumbe wa kituo cha Redio cha televisheni cha kimarekani "Columbia".

Mnamo Aprili 25,1960.