Nakuta Kuna Balaa Mkubwa Unatukabili, Ni Ukoloni wa Kimawazo na Kiakili Uliofanya Kazi ya Kueneza Ubaguzi na Kuondoa Maadili

Nakuta Kuna Balaa Mkubwa Unatukabili, Ni Ukoloni wa Kimawazo  na Kiakili Uliofanya Kazi ya Kueneza Ubaguzi na Kuondoa Maadili

Imetafsiriwa na/ Naira Abdelaziz
Imehaririwa na/ Nourhan khaled

Enyi Wananchi:

Tulikuwa tukiimba anguko la Waingereza au dhidi ya chama fulani, kukizingatia hiyo kuwa njia ya kufikia malengo ya nchi. 

Lakini baada ya kufikiria, nilikuta kuwa kulikuwa na dosari, mara nyingi tulikimbia kuhamisha ukoloni, uhuru, kwa Kuondoa ukoloni.
 Ukoloni uliwakilishwa na aina fulani ya sare ya kijeshi na nyuso nyekundu, lakini hii haikuwa dosari lenyewe.

Hatimaye nilipatwa mwangaza ulioniwezesha  kushikilia njia. Niligundua kuna balaa  kubwa linalotukabili, ni ukoloni wa kimawazo na kifikra uliofanya kueneza ubaguzi na kudhoofisha maadili, koloni huu wa kimawazo umeotawala nchi yetu kwa muda mrefu, tusipoiondoa, hatutafikia lengo letu katika ufufuo wa taifa letu. 

Kuwepo kwa tabia ya kiburi iliyoeneza miongoni mwa watawala wa Khedive, kwa askari polisi, kwa mwananchi asiye na uwezo wowote, kila mmoja akiwakandamiza walio chini yake katika cheo. 

Kuna dosari yetu nyingine; Ni kwamba kila mtu anadhani kwamba anajua kila kitu, Na hawezi kukosolewa tu,  kulaumu wengine, na hajui chochote na hana ujuzi wa kufanya chochote. 

Kuna dosari ya tatu; Ni wivu na kinyongo ndio huwakilisha sera ya uharibifu. Hii inaelezea kufupisha mazoefu, wakati tunaona katika nchi zingine,iwapo uzoefu  unaonekana,  wananchi huchukua hatua ya kuusukuma ujitokeze, kwa sababu wanajua kwamba huyu  ndiye anayefika leo, baadaye atasaidia wengine kufika. Ikiwa tunaweza kujua ukweli- ukweli haumaanishi uwongo - na ikiwa tukitambua masomo ya zamani, tutafikia malengo yetu. Ni lazima kwanza tushinde ukoloni wa kiakili na kimawazo, kisha tunaona njia iliyo wazi mbele yetu. 


Wassalamu Alaikum warahmat Allah.

Hotuba ya Bekbashi Gamal Abdel Nasser katika kambi  ya mafunzo ya vijana huko mjini Alexandria

Mnamo Septemba 18, 1953

Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy