Niko tayari kukubali suluhisho lolote la mgogoro wa Mfereji wa Suez,ikishurutiwa kutoshughulikia udhibiti wa Misri, lakini nakataa wazo la usimamizi wa kimataifa wa Mfereji 

Niko tayari kukubali suluhisho lolote la mgogoro wa Mfereji wa Suez,ikishurutiwa kutoshughulikia udhibiti wa Misri, lakini nakataa wazo la usimamizi wa kimataifa wa Mfereji 

Niko tayari kutia saini mkataba unaohakikisha uhuru wa urambazaji, kwa ajili ya kusaini mkataba unaohakikisha uhuru wa urambazaji kwenye Mfereji huo.

 Misri ndiyo inayokabiliwa na tishio la nchi mbili kubwa,nazo ni Ufaransa na Uingereza, na sio Misri yenyewe inayotishia nchi hizo mbili.

Tunataka kufikia suluhu, na tunaamini kwamba suluhu hilo lazima lifikiwe kwa mjadiliano, Lakini tunakabiliwa na tishio kutoka kwa mataifa makubwa mawili, na tunachoweza kufanya ni kutetea nchi zetu.

Nami sioneshi mgogoro huo wa Mfereji mbele ya Umoja wa Mataifa; ambapo naogopa kwamba moja ya mamlaka kubwa itatumia kura ya VETO,pia nilikata matumaini katika Baraza la Usalama, tunapendelea kutegemea msaada wa maoni ya umma na tabia ya kimaadili Duniani.

Hatuwezi kukubali usimamizi wa kimataifa wa Mfereji; Kwani maana yake ni ukoloni wa pamoja, ama kampuni iliyofutwa haikuwa chochote ila ni mabaki ya ukoloni na dola ndani ya dola.

Tunahisi kuwa sehemu ya ukuu wetu itaondolewa kutoka kwetu kupitia wazo la usimamizi wa kimataifa,nami nina uhakika wa haki ya nchi yangu na nimehakikishiwa kuhusu hisia za watu wa Misri na kumwamini Mwenyezi Mungu. Hatutaki vita, lakini tunapigana ikiwa tunashambuliwa. Sitaki vita izuke kwa sababu ya mgogoro wa Mfereji wa Suez, lakini nitapigana ikiwa ni lazima, hakuna mtu ulimwenguni anayetaka vita, lakini tutajilinda ikiwa tunashambuliwa.

Vikwazo vya Magharibi vilivyowekwa kwa Misri kama jaribio la kueneza njaa kati ya watu wa Misri, lakini jaribio halitafanikiwa.

Misri haina mpango dhidi ya mali nyingine za Magharibi katika Mashariki ya Kati, Misri inakusudia kujitolea juhudi zake kwa ajili ya kutekeleza miradi yake ya kiuchumi na kuinua kiwango cha maisha miongoni mwa watu wa Misri. Na Marekani lazima iwe ya haki na bila ubaguzi na kutojitoa mhanga nchi ndogo kwa ajili ya maslahi ya nchi za kikoloni.

Nimesikitishwa na kauli ya kwanza ya Rais Eisenhower kuhusu  hali ya kimataifa ya Mfereji;  jambo lililopelekea Misri kufanya maandamano,lakini ufafanuzi uliotajwa na Rais Eisenhower katika mkutano wake na waandishi wa habari umehakikishia hisia za Misri kwa kiwango cha kuridhisha, na Marekani lazima izingatie haki ya kimataifa inaposhughulika na nchi ndogo.

Waelekezi wa nchi za Magharibi wanaweza kuacha kazi zao, lakini baada ya kutuarifu mapema kabla ya kuacha kazi.

Misri itapata waelekezi wengine kutoka nchi rafiki ikiwa waelekezi wa magharibi wataacha kazi zao kwenye Mfereji.

Siwezi kusema: Nitapata msaada kutoka Urusi ikiwa Ufaransa na Uingereza zitatumia nguvu, Lakini ni kawaida ikiwa mtu anakushambulia, hutafuta msaada kutoka kwa mtu yeyote.

Misri imepokea maombi kutoka kwa raia wa Urusi kujitolea katika Jeshi la Ukombozi la Misri, na tumepokea ofa kutoka nchi nyingi, tunatazama mienendo ya majeshi ya Kiingereza na Kifaransa katika Bahari Nyeupe ili kuona nini kitakachofuata. Sikuchukua Mfereji kama wengine wanavyodai - tulitumia tu haki yetu ya kutaifisha kampuni, ama Mfereji wenyewe ni wa kimisri, uko ndani ya nchi ya Misri, pia kampuni iliyokuwa ikiisimamia ilikuwa kampuni ya kimisri, na kusimamia biashara ya Mfereji ni mojawapo ya haki zetu, kwa mujibu wa  makubaliano yaliyoidhinishwa katika suala hilo.

Mamlaka za usalama za Misri ziligundua Mkusanyiko wa kijasusi wa Uingereza, na mkusanyiko huo tayari umeshafahamu kitu fulani cha mipango ya kimisri, Ndio maana zikaamua kuwakamata wanachama wake ili kukomesha shughuli zake.

__________

Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu kutaifishwa  Mfereji wa Suez

Mnamo Septemba 2, 1956.