Wakati uliopita "Napoleon" alipovamia Misri, nani aliyesimama na kupigana?

Wakati uliopita "Napoleon" alipovamia Misri, nani aliyesimama na kupigana?

Enyi ndugu raia:

 

Ninapoona nguvu hii inayowaka katika roho hizi safi na mioyo hii safi, ninapoona nguvu hii na kuigusa kama nilivyoiona leo, na kama nilivyoigusa leo, ninahisi usalama.. usalama kwamba tutafikia -kwa msaada wa Mwenyezi Mungu-malengo ambayo tulichukua ahadi kuyahakikisha.

 

Watu hawa wenye nguvu, watu hawa wenye hadhi, watu hawa safi, wanaojitahidi, wapiganaji waamini katika Mwenyezi Mungu na waamini katika nchi, kisha waamini katika yenyewe, na hii ni siri ya nguvu ambayo kwake tuliweza daima kushinda maadui, hii ni siri ya nguvu ambayo imetuwezesha kuwashinda wavamizi kwa miaka mingi na kwa siku nyingi, na kuwafukuza wameshindwa na wamedharauliwa kutoka nchi zetu, hii ni siri ya nguvu ambayo imetuwezesha kuhifadhi nchi yetu kwa ajili yetu na kwa watoto wetu.

 

Wakati uliopita, Napoleon alipovamia Misri, nani aliyesimama na kupigana? Na ni nani aliyesimama dhidi ya majeshi ya “Napoleon”? Mfanyakazi.. Mkulima anayejiamini, huamini katika nchi yake, na huhisi kwamba nchi hii ni nchi yake. Mtu anayefanya kazi kwa ajili ya nchi yake na hafanyi kazi kwa ajili ya kuinyonya nchi yake, au kwa ajili ya kuwanyonya watu. Maadili haya na sifa hizi daima zimekuwa sifa za watu hawa; ilikuwa ni sifa hizi daima ambazo zimewaunganisha wana wa watu hawa na kuwaleta pamoja; kusimama dhidi ya wavamizi, kusimama dhidi ya vikosi vya kikatili, kusimama dhidi ya majeshi yenye nguvu zaidi, na sifa hizi na maadili haya –Enyi ndugu– ambayo daima yametuwezesha kushinda.

 

Napoleon” alifikia majeshi yake katika mji huu, lakini je, hii ilikuwa sababu ya kuingiza hofu au tisho katika nafsi na mioyo? Je, hii ilikuwa sababu ya watu wa Al-Manzala kutangaza kwamba walisalimu amri kwa “Napoleon” ambaye alichosha majeshi ya dunia Kamwe, kwanini? Kwa sababu watu hawa daima walikuwa wanajiamini, wanaamini Mwenyezi Mungu, na wanaamini nchi yake, na kufanya kazi kwa ajili ya uhuru wa taifa lake na uhuru wa nchi yake, kwa sababu watu hawa daima walikuwa wakiamini kwamba maisha huru ni tumaini lake, na kwamba maisha huru ni lengo ambalo yeye hutoa, kwa ajili yake, damu yake na nafsi yake, kwa hili ya hilo mji huu ulitoka.. ukatoka kwa wana wake, na kila mmoja wao akiwa na silaha na kile anachokiona njiani mwake, wakiwa na fimbo, akiwa na panga, na walikabili jeshi la “Napoleon” na jeshi la wanamaji la “Napoleon”, je matokeo yalikuwa nini?

 

Watu huru, wenye hadhi, waaminifu walishinda, waliwashinda wavamizi; maneno haya yalitokea tangu miaka 160, na watu walikuwa, katika mkoa huu, watu wema.. watu wanaoshindana.. watu wenye bidii.. watu wanaofanya kazi.. watu wanaosimama dhidi ya unyonyaji na dhidi ya udhibiti, dhidi ya unyonyaji wa nje na dhidi ya unyonyaji wa ndani, na kwa sababu hizi, tumeshinda katika wakati uliopita.

 

Hiyo -Enyi ndugu- ni historia yetu.. Historia yetu ya hivi karibuni, na historia yetu ya mbali. Katika Mwaka 1956 tulisimama kukabiliana na ukoloni, kukabiliana na wakoloni na kukabiliana na majeshi ya ukoloni, na watu wa eneo hili walikuwa wakijitolea kusaidia watu wa Port Said waliopigana dhidi ya ukoloni na dhidi ya uchokozi, na watu wa mkoa huu walikuwa wakitoa roho zao na damu yao kwa ajili ya uhuru.

 

Kwa hivyo, sifa hizi sio mpya kwetu, lakini zilipandwa katika damu yetu na katika nafsi zetu, katika mioyo yetu na katika roho zetu, tulirithi mapambano kutoka zamani; kutoka wakati ambapo baba zetu na babu zetu walikuwa wakipambana kupata uhuru na kujitegemea, na waliweza kufanikiwa katika mapambano haya; kwa hivyo walikombolewa, walipata uhuru na walipandisha bendera ya uhuru. Sisi pia tulichukua somo hili kutoka kwao, na tulipigana kwa ajili ya uokoaji; kwa hivyo tulipata uokoaji, na kisha baada ya hapo tulipigana kuzuia uvamizi, na tuliweza kushinda dhidi ya uchokozi na kuwashinda wavamizi.

 

Hiyo -Enyi ndugu- ilikuwa historia yetu ya karibuni kisha tulianza baada ya hilo.. tumeanza katika njia gani? Katika njia ya ujenzi, njia ya kazi, na njia ya kujenga jamii ya kisoshalisti ya kidemokrasia ya ushirikiano.. Jamii ambayo inaishi kwa starehe, jamii inayofanya kazi kuboresha maisha, kujenga maisha yenye furaha kwa kila mtu na kila familia. Tujenge jamii hii, tulilazimika kukombolewa, ilibidi tuondoe ushawishi wote wa kigeni katika taifa letu, ili tukombolewe tulilazimika kupambana, ili tukombolewe tulilazimika kumwaga damu, ili tukombolewe tulilazimika kuwa na kiwango cha juu cha fahamu; tuweze kukabiliana na ukoloni na njama za ukoloni.

 

Na Jana -Enyi ndugu- huko Port Said, nilisema kuwa baada ya kushinda vita vyetu dhidi ya ukoloni, na dhidi ya wasaidizi wa ukoloni, tulishinda.. Baada ya ushindi huu, tulifanya nchi yetu msingi kwa ajili ya uhuru, na tulifanya wenyewe mbele ya uhuru, kwa sababu twaamini na kwa sababu twajua kwamba ushindi wa uhuru mahali popote ni ushindi wa suala la uhuru wetu, na kwamba kupoteza uhuru wa mahali popote ina athari kubwa juu ya suala la uhuru wetu, na suala la uhuru wetu inahusiana sana na kufanya kazi tufikie lengo letu la kujenga jamii ya kisoshalisti ya kidemokrasia ya ushirikiano.

Uhuru na ukombozi, zilikuwa hatua na zilikuwa kipindi kwa ajili ya ujenzi wa ujumla, Ni nini ujenzi huu wa ujumla? Uhuru na ukombozi zilikuwa kipindi kwa ajili ya kuondoa ukabaila, kuondoa unyonyaji, kuondoa kuhodhi, kuondoa ubaguzi kati ya watu, na uanzishwaji wa haki ya jamii.

 

Kila mtu wa taifa hili alikuwa analenga kuanzisha haki ya kijamii kati ya pande za taifa hili; ili aweze kujiaminia siku yake na kujiaminia kesho yake. Tulipokumbana na ukoloni na kukumbana na njama za ukoloni, silaha yetu kuu ilikuwa ni ufahamu na umoja wa kitaifa, kwa sababu ukoloni ulitegemea, wakati uliopita, kutenganisha upande chuki kati yetu, kutuwezesha, na kuanzisha miongoni mwetu wasaidizi kufikia malengo yake. (Kushangilia).

 

Wakati uliopita, ukoloni ulifanya kazi juu ya kutenganisha.. hizi zilikuwa silaha za ukoloni wakati uliopita; ili kutuweka ndani ya nyanja za ushawishi, ili kutudhibiti na kunyonya utajiri wetu, ili kutunyima mali za nchi yetu. Lakini tulikuwa waanfalifu kwa mbinu hizi, hivyo tukaungana kuondoa ukoloni na wasaidizi wa ukoloni, tukaondoa wasaidizi wa ukoloni, tukaondoa ukoloni, na nafasi ikawa nzuri kwetu kuanza kuijenga nchi yetu na kufidia kile tulichokikosa.

 

Lakini je, ukoloni umerudi kwenye mipango uliyoifuata huko nyuma? Je ukoloni umerudi nyuma kwenye mbinu ulizozitumia zamani kuliweka taifa la kiarabu ndani ya maeneo ya ushawishi na kuanzisha, kati ya pande zake, watawala kwake kwa bei ya chini ambayo wanaiuza nchi yao? Ukoloni haukurudi nyuma kwenye mbinu hizi, na ukoloni haukurudi nyuma kwenye lengo lake la kufikia… Je... Je (mashangilio yalifanywa kwa muda mrefu kutoka kwa umati wa watu…. Kisha Rais aliwahutubia maneno haya:) sawa, Shukrani.. bila shaka, sijaanza kuwashukuru kwa kushangilia na kusalimu; kwa sababu mimi nazingatia hii kuelezea umoja wa kitaifa na muungano, na nilikuambieni hapo awali kwamba nazingatia hisia nilizoziona kama nguvu, lakini hisia hizi, kama si hisia zenye utaratibu, hawezi kwa njia yoyote kuwa kuonesha nguvu, ni lazima kwamba sisi si hapa kusema maisha mrefu kwa Gamal, maisha mrefu kwa Gamal, tulikuja kuzungumza na kueleza msimamo wetu, kueleza mambo yetu, na kuchukua nafasi hii tujue tuko wapi? na njia gani ambapo tunatembea.. Niliwashukuru kwa kushangilia, na sitaki vifijo tena baada ya hapo.

 

Tunazungumzia matatizo yaliyotukabili katika siku za nyuma, lakini tunapozungumzia matatizo yaliyotukabili katika siku za nyuma, tusizungumze tu kutoa hotuba, kusema maneno na kupoteza muda, tunazungumza kuchukua kutoka siku za nyuma mahubiri na funzo kwetu, tuwe na ufahamu kwa siku zijazo; kwa sababu mbinu hazibadilish, mbinu ni daima hizi hizi, mbinu zilizotumiwa dhidi yetu wakati uliopita katika siku za “Napoleon”, na ambazo mlipigana kwa ajili yake hapa katika nchi hii, na ambayo mlitoa, katika njia yake, mashahidi na mlimwaga damu na roho, ni mbinu zile zile tulizozikabiliana nazo baadaye katika Mwaka 1801; wakati wa ujio wa Kampeni ya “Fraser”, tuvamie, tudhibiti, na tutiisha chini ya ukoloni wa Uingereza.. Lakini watu walikuwa na ufahamu mkubwa kwamba waliishinda Uingereza na wakashinda kampeni ya “Fraser”, na kampeni ya “Fraser” ilisalimu amri, na watu waliweza kuhifadhi uhuru wao, na watu waliweza kuhifadhi nchi safi kutoka kwa ukoloni na uvamizi wa kigeni.

 

Mbinu hizi pia ni zile zilizofuatwa nasi baadaye Mwaka1882, wakati Uingereza ilikuja kuvamia Misri, walipiga Alexandria katika Mwaka 1882, na walichoma Alexandria mnamo Mwaka 1882, na wakasonga mbele kwa Kafr El-dawar, Lakini watu waliokuwa na ufahamu wa mbinu hizi hawajatishiwa na nguvu, wala hawajatishiwa na meli za Uingereza, wakatoka katika Kafr El-dawar na walipigana katika Kafr El-dawar na walishinda Uingereza tena katika Kafr El-dawar, na Uingereza ilirudi Alexandria iondoke, kisha ipange njama na kufikia kwa udanganyifu isipokuwa ingeweza kupatikana kwa nguvu, Uingereza ilirudi Mwaka 1882 na Ufaransa.. Walifanya njama na Ufaransa kupitia Mfereji wa Suez, na kwa udanganyifu walitudhibiti.

 

Tunapozungumzia wakati uliopita na yale yaliyopita, tunazungumzia tuwe na mahubiri na funzo kutokana na masomo haya, mahubiri tuliyoyachukua Mwaka 1956 wakati “Eden” alipeleka tukabidhi port Said, Ismailia na Suez kwake, mahubiri haya sote tulikuwa tukuyajua nasi sote kuhubiri kwake, tulikataa onyo la Uingereza katika mwaka 1956, na mimi nilikuwa na uhakiki katika Mwenyezi Mungu, katika nchi hii na katika watu hawa.. Nina uhakika kwamba tutashinda.. Nilijua kwamba watu hawa, ambao wakati uliopita, wameshinda dhidi ya “Napoleon”, dhidi ya Uingereza na dhidi ya Wakrusedi, lazima washinde tena kama tuliondoa wasaidizi wa ukoloni, kama tuliondoa unyonyaji, na kama malengo tuliyopitisha yalikuwa malengo kwa ajili ya mtu na kwa ajili ya watu, sio kwa ajili ya watu wachache, wala sio kwa ajili ya watu wachache kutoka kwa wanyanyasaji.

 

Malengo hayo ambayo mashujaa walitoka katika Mwaka 1956 wakichukua silaha kuyatetea, kuiweka mizizi yake ardhini baada ya kumwagilia kwa damu yao, malengo tuliyoyapitisha ni kwamba nchi yetu iwe kwetu, nchi yetu iwe huru kutoka katika unyonyaji, nchi yetu iko huru kutoka kwa utawala wa kigeni, nchi yetu iko huru kutoka katika ukabaila, nchi yetu iko huru kutoka katika kuhodhi, nchi yetu ina haki ya kijamii, na nchi yetu ina usawa. Kila mmoja alikuwa anaenda na kuilinda nchi yake kwa damu yake, na yeye akijua kwamba kwa hili halindi unyonyaji, na halindi ukabaila au kulinda kuhodhi, bali analinda nchi yake ambayo kanuni na maadili yalilelewa.

 

Na damu hizo ndizo tulizomwaga katika Mwaka 1956.. Damu hizo na mashahidi hawa waliotoa maisha yao katika Mwaka 1956 walikuwa nguzo kubwa katika njia ya kujenga Jamhuri hii ya Muungano ya Kiarabu; Jamhuri iliyounganisha Misri na Syria, Jamhuri haitegemei jina milele, lakini yategemea kanuni, yategemea maadili ya juu, yategemea kanuni za ujamaa wa kidemokrasia wa ushirika, yategemea kanuni za utaifa wa kiarabu, na kanuni za umoja wa kiarabu, yategemea kanuni za haki ya kijamii, ulingano wa nafasi na usawa.. hii ni Jamhuri yetu ambayo sote tulikuwa tunaitetea, kuanzia Rais wa Jamhuri hadi mfanyakazi yeyote ndani yake, huu ni Jamhuri yetu ambapo sote tunafanya kazi kuimarisha nguzo zake, tujihakikishie na kuwahakikishia watoto wetu kuishi katika nchi huru, kuishi katika taifa huru.

 

Hii ni Jamhuri ambayo tunasema: ni msingi wa uhuru, na hawa ni watu ambao tunasema: ni mapinduzi ya uhuru; watu ambao hawajawahi kudanganywa katika wakati uliopita. Inawezekana walikuwa, wakati fulani, kuamini na kutuliza, lakini hawakuwahi kutuliza maadui zake kamwe, hakuwahi kuachilia damu yake, hawakuwahi kuachilia roho yake, watu ambao ni akina nani? Watu hawa ni Nini? Watu ni wakulima na wafanyakazi, mfanyakazi kwa ajili ya nchi hii na kwa ajili ya ujenzi wake, wao ni watu, watu hawakuwa kamwe pasha au mawaziri, au wanyonyaji, au wenye kutawala au wanaohodhi, kwa sababu hawa walikuwa wanawakilisha tabaka dhidi ya malengo ya watu.

 

Watu walikuwa wakipigana ukoloni, na wakati huo huo walikuwa wakipigana unyonyaji, kwa sababu waliamini kwamba mapambano ya vita vya ukoloni, wasaidizi wa ukoloni na vita vya unyonyaji wa ndani yalikuwa vita moja.

 

Na walikuwa wanaamini kuwa inapaswa kuondoa ukoloni na wasaidizi wa ukoloni; tuweze kuondoa unyonyaji na kuanzisha haki ya kijamii. Tulipoondoa ukoloni na wasaidizi wa ukoloni, kweli inaonekana leo- baada ya miaka 7 au baada ya miaka 8- tunaweza kusema kwamba tumefanya, pengine sio kazi kwamba kila mtu alitaka_ katika nafsi yake_ kuiona, lakini pamoja na hili tumeongeza mara mbili mapato ya taifa katika miaka saba, na tumeongeza wastani wa mapato kwa kila mtu na 70 %tumeanzisha viwanda, tukabadilisha nchi yetu kutoka nchi ya kilimo kwa nchi ya viwanda, je maadui yatu watakubali kwa hiyo? Je, maadui yetu watasalimu? Au ukoloni na wasaidizi wa ukoloni wakoloni katika eneo hili la dunia wanajaribu kupanga njama dhidi ya Jamhuri ya Muungano ya Kiarabu.

 

Bila shaka, hawawezi kuridhika kwamba Jamhuri ya Muungano ya Kiarabu iwe.. Mfano wa nchi ambayo imepata uhuru wake, imeondoa unyonyaji, imeondoa wanyonyaji, imeondoa ukoloni na wasaidizi wa ukoloni, na ilikuta nafasi nzuri ya kujenga, kufanikisha, na kutoa kazi huru kwa mfanyakazi huru mwaminifu. Hawataweza kukubali hili, hawataweza kukubali kwamba utashi wetu utokanae na ardhi yetu, nchi yetu, dhamiri yetu, na maslahi ya watu wetu, kwa sababu walizoea wakati uliopita, kwamba utashi wao wenyewe ulioshinda katika eneo hili, hawatatosheka na hili kamwe.

 

Kwa msingi huo, vita tunayvokabiliana nayvo kutoka kwa ukoloni na wasaidizi wa ukoloni katika taifa la kiarabu ni vita endelevu kwa muda mrefu kama maisha yatadumu, mpaka tuwaondoe wasaidizi wa ukoloni.

 

Kwa mfano, tunaona katika taifa la kiarabu mifano mingi ya suala hili; katika Mwaka 1956 Uingereza ilikuwa inatawala Jordan, na Mfalme Hussein katika Jordan alikuwa anajulikana kuwa msaidizi wa Uingereza, na yeye ni mtetezi wa ukoloni wa Uingereza, Mfalme Hussein alitoka katika Mwaka1956 na alisema kubwa badilisha jina lake, alibadilisha mwelekeo wake, alitubu usaliti ambao mababu zake walipigwa risasi, yeye ni mzalendo, na ataenda katika njia ya uzalendo na njia ya heshima.. kwa haki ya Mwenyezi Mungu, maneno haya, na tumengoja kuona matokeo.

 

Mfalme Hussein alitukumbusha kwa hadithi ya zamani ambayo pengine sote tunaijua.. Kulikuwa na mtu mmoja katika wakati uliopita ambapo Jina lake  ni Ali Al-Jahsh, Ali Al-Jahsh alikuwa yupo nchi, na alikuwa akikuta watu wangemtazama na kumdhihaki, kulidhihaki jina lake, akawaambia, kwa haki ya Mwenyezi Mungu, nitabadilisha jina langu, walifurahi kwa ajili yake; kama tulivyofurahi kwa Mfalme Hussein, na alibadilisha jina lake na alirudi, wakamwambia,  umebadilisha jina lako? Aliwasema ndiyo, nilibadilisha nina langu. Walimwaambia, umelibadilisha kuwa nini? Aliwasema, nililibadilisha kwa Hassan El-Jahsh. (Kicheko).

 

Hadithi ni hiyo hiyo, Mfalme Hussein katika Mwaka 1956 alituambia nini? Alituambia kwamba nilikawa mzalendo, tulifurahi.. Tulifurahi kwamba alibadilisha njia ambayo alienda, na ambayo mababu zake walienda, na alirudi tuliona na tulimkuta katika Mwaka 1957 Hassan El-Jahsh kama alivyokuwa Ali El-Jahsh, hadithi ile ile na njia ile ile. Sisi kama watu pengine kuwa watu wanaocheka, watu wema, lakini hawadanganywa, Watu wanaocheka, watu wanaoelewa, watu wema, ukoloni hautaweza kwa njia yoyote ile, kuwadangaya, anabadilisha jina lake kutoka Hassan El-Jahsh kwa Ali El-Jahsh twaelewa kwanza na mwisho lengo ni nini, lengo; ni kuwadanganya Watu wa kiarabu, na watu wa kiarabu hawatadanganywa na mwana punda yeyote miongoni mwa wana punda wa ukoloni. (Kicheko).

 

Wasaidizi wa ukoloni katika eneo hili la ulimwengu wote tunawafahamu, na Watu wa kiarabu hawatadanganywa kwa njia yoyote kwa sababu walijua njia yao; lazima waondoe ukoloni, lazima waondoe maeneo ya ushawishi, lazima wawe bwana wa utashi wao, utajiri wao lazima uwe kwao, lazima waondoe kurudi nyuma na unyonyaji, lazima waipandishe bendera ya utaifa wa kiarabu, lazima waijenge nchi yao; iwe nchi yao, na waishi maisha huru na bora. Mwenyezi Mungu akusaidieni.

Amani iwe juu yenu, rehema na baraka za Mwenyezi Mungu. ـــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــ

Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser katika maadhimisho ya Siku ya Ushindi kwenye El-Manzala.

Desemba 24, Mwaka 1960