"Ghazaly " Mzungumzaji kuhusu Vijana, Utamaduni na Tafsiri kwenye Baraza kuu la Utamaduni

"Ghazaly " Mzungumzaji kuhusu Vijana, Utamaduni na Tafsiri kwenye Baraza kuu la Utamaduni

Hassan Ghazaly, Mwanzilishi wa mradi wa Bozor na mjumbe wa kamati ya vijana ya baraza la Utamaduni alishiriki kwenye kikao cha majadiliano kuhusu "Vijana na upeo wa Utamaduni, na Tafsiri" kilichofanyika siku ya Jumanne jioni , Disemba hii, tarehe 13, kwenye makao makuu ya Baraza huko Jumba la Opera, pamoja na Ufadhili wa Dkt. Neven Alikilani Waziri wa Utamaduni, na Dkt. Hisham Azmy kitabu mkuu wa Baraza kuu la Utamaduni.

Wakati wa mazungumzo yake, Ghazaly alidokezea uhusiano wa Utamaduni na Tafsiri, akielezea umuhimu wa ukarabati wa mfasiri, na kuimarisha stadi zake, sio tu kwa upande wa kazi kwenye utaalamu wake, lakini pia kuendeleza utamaduni wake, na afadhali kwenye muhula wa masomo katika chuo kikuu, na jambo hilo lina athari kuu kwenye safari yake ya kazi na elimu baada ya kuhitimu, akiashiria juhudi zake kwenye uundaji wa mwanachama mwenye Utamaduni, a uwezo wa maendeleo ya Utamaduni, kupatia mradi wa Bozor kwa elimu ya sanjari iliyoziduliwa mnamo mwaka wa 2015, na ilitekelezwa juu ya watafsiri vijana mnamo mwezi wa Aprili mwaka wa 2022 na  tuko ndani ya mchakato wa kuhitimu kundi lake la kwanza  baada ya siku chache.

Kwa upande unaohusiana kikundi cha washindi walishiriki kwenye shindano la "Watafsiri Vijana" kuhusu masuala ya mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa lililoandaliwa na Baraza Kuu la Utamaduni  na miongoni mwao Omnia Samir kwa Kiswahili, Shaimaa Mohamed kwa 
 Kifaransa, Kyaty Ashour kwa Kiingereza, kreles Bekhet kwa Kireno, Mirna Magdy kwa Kirusi, walioonesha stadi zao kwenye majaribio yao yenye thamani kwenye nyanja ya tafsiri, yaliyojumuisha maudhui mbalimbali kama "Kuimarisha ustahimilivu wa mabadiliko ya hali ya hewa kwa Kiswahili" na pia yanajumuisha "masuluhisho yanayotegemea mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa" na pia Sosholojia ya mabadiliko ya hali ya hewa na jamii, pamoja na "viumbe hai tofauti wa Afrika na Amerika Kusini" na "Tathmini ya mabadiliko katika uzalishaji wa ngano chemchemi".