Ghazali ni Mzungumzaji katika Kongamano la Kimataifa la Vijana huko Indonesia
Taasisi ya "Youth Power" nchini Indonesia ilimpokea Mwanaanthropolojia Hassan Ghazali, Mwanzilishi wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, kupitia "Video Conference", Jumatano, Aprili 8, kwa kuwepo kikundi cha wazungumzaji kutoka mataifa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Indonesia na Pakistan, pamoja na mahudhurio ya zaidi ya Viongozi Vijana 500 wa eneo la Indonesia; kuzungumzia uzoefu wake wa upainia katika uwanja wa diplomasia ya vijana na programu zake za kimataifa kama mfano wa kimataifa wa kufuatwa katika uwanja wa uwezeshaji wa vijana kwa uongozi.
Wakati wa hotuba yake, Ghazali alizungumzia pointi kadhaa muhimu, ikiwa ni pamoja na mazungumzo yake kuhusu dhana ya Uongozi wa kimataifa, akiwaelekeza kiongozi Ahmed Sukarno, Jawaharlal Nehru, Joseph Tito, Kwame Nkrumah na kiongozi asiyekufa Gamal Abdel Nasser, Waanzilishi wa Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote, kama mfano na aina ya uongozi tunaouhitaji kwa wakati huu kutokana na mizozo na migogoro ambayo nchi nyingi za Dunia zinakabiliwa nayo, haswa kwa sababu ya mgawanyiko wa kimataifa unaoendelea Duniani, akiashiria kuwa Harakati ya Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa iliweza kuimarisha diplomasia ya vijana na kwa kipindi cha miaka minne iliyopita, iliweka wazi nafasi za mazungumzo na jukwaa la kubadilishana uzoefu na fursa za ushirikiano kati ya viongozi vijana wanaoshiriki kutoka nyanja tofauti.
Katika hotuba yake, Ghazali alisisitiza kujali kwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa kwa kufufua misingi ya Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote ya Nchi na mchango wake wa kihistoria katika kujenga Amani na kuleta utulivu katika jamii, akiashiria warsha zinazofanyikwa wakati wa Udhamini huo, pamoja na kichwa cha "Global Citizen Talks" ili kuunda dhana za Kutofungamana kwa upande wowote na kanuni zake kutoka kwa mtazamo wa vijana unaoendana na changamoto za zama.

Katika muktadha unaohusiana na hayo, Ghazali aligusia umuhimu wa elimu, nafasi ya elimu sambamba na uwezo wake wa kibunifu usio na kikomo katika kuweka nguvu za vijana na kuwawezesha, akisisitiza ari yake ya kuchangia katika kuimarisha jukumu la elimu sambamba kupitia miradi yote na programu ambazo anazindua, tena aliashiria mchango wa Al Azhar kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 1083 kwa kuanzishwa kwake, Taasisi hiyo kubwa ya zamani zaidi yenye thamani ya kiroho, kielimu na kiutamaduni kwa watu wa Dunia na haswa watu wa Indonesia.
Mwishoni mwa hotuba yake, Ghazali alithamini sifa za vijana wa Indonesia katika uongozi katika nyanja mbalimbali, huko akieleza kuwa alishuhudia mifano yao kwa karibu wakati wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika matoleo yake yaliyopita, miongoni mwao ni kiongozi kijana “Safi Effendi. ", Mkuu wa Baraza la Vijana la Kitaifa, akisisitiza uwakilishi wake wa heshima wa nchi yake na alikuwa kama Balozi wa unyenyekevu mkubwa na tabia njema tena akili timamu.