Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nchini Misri akutana na Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Imetafsiriwa na: Basmala Hisham
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Mshauri wa Kwanza wa Balozi Ndoko Boo alipokea ujumbe wa viongozi vijana wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaoshiriki kwenye Udhamini wa Gamal Abdel Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika Ubalozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nchini Misri, Zamalek, Kairo. Wakati wa mkutano huo, viongozi hao vijana walielezea uzoefu wao na ufahamu wao kuhusu mpango huo, pamoja na ujuzi wao wa utawala wa Misri, wakiuelezea kama msukumo wa maendeleo na mabadiliko kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.