Mwanachama wa Harakati ya Nasser kama balozi katika mfano wa vikao vya Umoja wa Mataifa

Mwanachama wa Harakati ya Nasser kama balozi katika mfano wa vikao vya Umoja wa Mataifa

Imetafsiriwa na: Habiba El-Sayed
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr 

Arwa Hatem, Mwanafunzi wa mwaka wa nne katika Kitivo cha Al-Alsun, Chuo Kikuu cha Ain Shams, mwanachama wa kamati ya tafsiri ya mradi wa "Shule ya Kitaifa ya Maandalizi ya makada" na mwanachama wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, alishiriki katika toleo la tatu la Mkutano wa Mfano wa Umoja wa Mataifa wa Uigaji nchini Ufaransa chini ya kauli mbiu "Twapanda amani katika giza la ulimwengu", kama balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kama toleo hili lilifanyika mnamo tarehe 26 na 27 Novemba 2023, katika Kitivo cha Al-Alsun, Chuo Kikuu cha Ain Shams, chini ya usimamizi ya Prof. Dkt. Salwa Rashad, Mkuu wa Kitivo, chini ya usimamizi wa Prof. Dkt. Nasser Abdel Aal, Makamu Mkuu wa Elimu na Masuala ya Wanafunzi, Prof. Dkt. Youmna Safwat, Makamu Mkuu wa Huduma za Jamii na Maendeleo ya Mazingira, Prof. Dkt. Rania Adel, Kaimu Mkuu wa Idara ya Lugha ya Kifaransa, na uwepo wa kikundi cha wanachama wa kitivo katika Idara ya Lugha ya Kifaransa katika Kitivo.

Hii ilikuja na ushiriki wa wanafunzi wa 92 kutoka idara mbalimbali za lugha ya Kifaransa katika vyuo vya Chuo Kikuu cha Ain Shams (sanaa, sheria, biashara na lugha katika mifumo yake miwili) na kwa masaa 8 kwa siku, Uigaji wa vikao vya Umoja wa Mataifa ilifanyika, ambapo kila mwanafunzi anawakilisha nchi ya ulimwengu kuhusu jambo fulani, kwa mfano, ama suala la kuenea kwa amani ya nyuklia kulingana na Kamati ya Silaha, au suala la kulinda watoto wakati wa vita ambayo Kamati ya UNICEF ni msingi, na tukio hili la mwanafunzi ni shughuli ya kila mwaka ambayo huongeza mwingiliano wa kidiplomasia na ujuzi wa masuala ya kimataifa. na nafasi ya kila nchi juu ya mada hizo.

Kwa upande wake, "Hatem", katika uwezo wake kama balozi wa Taifa la Iran kwa mfano, na fursa ya kujifunza kuhusu msimamo wa Iran kwa undani zaidi juu ya ulinzi wa watoto wakati wa vita, alionesha kuwa alikutana na changamoto kadhaa katika kuwakilisha msimamo wa Irani na kucheza jukumu hilo, ikiwa ni pamoja na kikwazo cha kiakili, kitamaduni na lugha, akionesha kuwa vyanzo viliwezesha kazi yake katika kuelezea upande wa Tehran, pamoja na matumizi ya wanafunzi wa lugha ya Kiajemi, na wanafunzi wa uchumi na sayansi ya kisiasa, akisisitiza jukumu la Harakati ya Nasser kwa Vijana katika kukuza na kuunda ufahamu wake juu ya masuala ya kikanda na kimataifa.