Kipindi cha tano "Michango ya Viongozi Vijana Waafrika  katika Amani na Usalama Barani Afrika" 

Kipindi cha  tano cha program ya Raia wa Ulimwengu mzima, wakati wa kumpokea Waziri wa Vijana na Michezo wa Sudan Kusini DKT. Albino Paul kinajadili mchango wa vijana katika mpango wa Umoja wa Afrika wa kusitisha mapigano na kuihifadhi Amani, pamoja na kuzingatia  masuluhisho mapya ya vijana na kurahisisha kwa kuhakikisha maendelo katika nchi zao kwa mujibu wa ajenda ya Afrika 2063 na malengo ya maendeleo endelevu na changamoto kuu haswa mnamo kipindi cha COVID-19.

Mwanzoni mwa kikao, Waziri huyo akiusifu Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kimatiafa na Shule ya majira ya kiafrika 2063, pia juhudi za nchi ya Misri katika uwanja wa kutoa mafunzo wa vijana akisema: ni mwanzo mpya ili kuandaa viongozi wa mustakabali , Misri yatoa juhudi kubwa katika program za kutoa mafunzo kwa vijana haswa Barani Afrika, kama ufuatiliaji wa hatua za Mheshimiwa Rais Marehemu Gamal Abd El Nasser.

 

Katika kikao hicho, Profesa Albino alizungumzia juhudi za Sudan Kusini: "Tunafanya juu chini ili kuanzisha viwanja 3 vya Olimpiki ili kuwashirikisha vijana wa Sudan Kusini. wachezaji wa Sudan Kusini wana mustakabali nzuri sana, haswa katika mpira wa miguu na mpira wa kikapu ."

Kuhusu Changamoto za kazi yake binafsi  aliongeza, “Unaposhika nafasi, si watu wote watakukubali, wengine wanataka kukuondoa, hata hivyo navumilia na kufanya kila niwezalo kuitumikia nchi yangu na kupambana na ufisadi huu. ”

Orodha ya wageni wa programu hiyo inajumuisha watoaji maamuzi na viongozi vijana kutoka mataifa mbalimbali Duniani na katika nyanja tofauti, kwa lengo la kufikisha ujumbe chanya kwa vijana Duniani kutoka katikati ya jiji la Kairo, pamoja na kuunda kiunganishi kati ya vijana. na watoaji maamuzi, linalochangia kuandaa kada wa vijana wenye uwezo wa kufanya mabadiliko halisi.

Vipindi vya programu hiyo vinasimamiwa na Amira Sayed, Mwandishi wa habari wa Gazeti la Egyptian Gazet  ambalo ni gazeti la kwanza kwa lugha ya Kiingereza katika Mashariki ya Kati, pamoja na kuwa yeye ni mwakilishi wa Misri katika Bunge la Vijana la Kimataifa la Maji, na alishiriki katika matukio mengi ya kimataifa ndani na nje ya Misri.

inasemekana kwamba Programu ya  Raia wa Ulimwengu mzima (Global Citizen) ni programu ya kwanza ya moja kwa moja inayolenga kuunga mkono dhana ya Umoja na Ushirikiano wa kimataifa, na pia kuzingatia  majaribio ya vijana wenye mafanikio Duniani kote.