kipindi cha kwanza cha Programu ya "Mwananchi wa Ulimwengu"

Programu hiyo inaanza sehemu yake ya kwanza kwa kumpokea mfano wa vijana maarufu zaidi duniani. Programu hiyo ni programu ya kwanza ya moja kwa moja kwa lugha ya Kiingereza inayozinduliwa kwa lengo la kusaidia dhana ya Umoja na Ushirikiano wa kimataifa na pia kuangazia mwangaza juu yamifano bora ya vijana wenye mafanikio ya kimataifa.
Orodha ya wageni wa programu hiyo ni pamoja na idadi ya watoa maamuzi na viongozi wachanga kutoka nchi tofauti za ulimwengu na katika nyanja tofauti kadhaa , ikilenga kueneza ujumbe chanya kwa vijana wa ulimwengu kutoka kwa Kairo na pia kuwaunganisha vijana na watoa maamuzi, inayochangia kuandaa viongozi wa vijana wenye uwezo wa kufanya mabadiliko yanayoonekana kiutendaji.
Programu hiyo inakuja kulingana na mkakati wa Wizara ya Vijana na Michezo, inayohangaika kuwawezesha vijana na kuimarisha jukumu lao kukabili misiba ya kimataifa, ikiamini katika uwezo wa vijana kukabiliana na misiba ile kupitia shughuli , harakati na mipango kadhaa ya kuingiliana.
Vipindi vya Programu hiyo vinashikiliwa na Amira Sayed, mwandishi wa habari kwenye Gazeti la El Egyptian Gazet , linalozingatiwa gazeti la kwanza linalotamka kwa Kiingereza kwenye Mashariki ya Kati, pamoja na yeye ni mwakilishi wa Misri katika Bunge la Vijana la Kimataifa kwa Maji na ameshiriki katika matukio kadhaa ya kimataifa ndani na nje ya Misri.