Siku ya Kimataifa ya kufuta Ujinga wa Kutojua Kusoma na Kuandika

Siku ya Kimataifa ya kufuta Ujinga wa Kutojua Kusoma na Kuandika

Imetafsiriwa na/ Mariam Islam
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled 

UNESCO limetangaza mnamo mwaka 1966 kwamba siku ya 2 ya Septemba ni Siku ya Kimataifa ya Kufuta Ujinga wa Kutojua Kusoma na Kuandika, hii ilikuja kulingana na shughuli za mkutano wa kimataifa ya Wizara ya Elimu uliofanyika ili kujadili mambo kuhusu kufuta ujinga wa kutojua kusoma na kuandika mjini mkuu wa Iran (Tahran) katika siku ya 18 na 19 Septemba, mwaka 1965 .

Huo ulliofanyika kukumbusha Jumuiya ya Kimataifa Umuhimu wa kuunga mkono ili kufuta ujinga wa kutojua kusoma na kuandika kwa watu binafsi, vikundi na jamii, na ili kuhamasisha na kuimarisha ufanyaji wa kazi wa kuimarisha juhudi zinazofanyikwa ili kufikia jamii yenye maarifa kubwa ya kusoma na kuandika.


Kuna vijana na watu wazima milioni 733 ulimwenguni wanahitaji kujua ujuzi wa kimsingi wa kusoma na kuandika, kwa hiyo kuna dharura ya kubadilisha sera ya kitaifa ya elimu ili kufikia maendeleo ulimwenguni, na ili kuhakikisha ushiriki wenye faida na tija kwa wanajamii wote katika upande zote za kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Pia kama kauli iliyosemwa na Gobran Khalil Gobran " nchi zinajengwa kupitia mambo matatu: ( Mwalimu anayelea vizazi, Mkulima anayelisha wanake, na Askari anayelinda raia).

 Kwa upande mwingine, UNESCO lilitangazia rasmi kwamba Misri imepata zawadi ya Confucius 2021 ya kufuta ujinga wa kutojua kusoma na kuandika kwa kujaribu kwa Chuo Kikuu cha Ain-Shams kwa Ushirikiano na Mamlaka ya Kijumla ya Elimu ya Watu Wazima na inayohusika na kupanga madarasa ya kufuta ujinga wa kutojua kusoma na kuandika mtandaoni kwa maeneo ya vijijini na yenye umaskini katika Jamhuri ya Kiarabu ya Kimisri.

 Tunaweza kusema kuwa tuzo hii ni kama zawadi kwa juhudi kubwa za kimisri kwa kuunga mkono Rais Abdel-Fatah Al-Sisi, ili kukabili suala la kufuta  ujinga wa kutojua kusoma na kuandika, ili kujenga Jamhuri Mpya na isiyo na umaskini, ujinga na ugonjwa kwa kufikia mwaka 2030.

 Ama Kupitia historia, na kulingana na wasimamizi wa mradi na wanaohusika nayo, inasemwa kuwa Kiongozi wa zamani Gamal Abdel Nasser alikuwa akijali kabisa kwa elimu ya serikali.

 Mradi wa kufuta ujinga wa kutojua kusoma na kuandika wakati wa utawala wake ulikuwa ukianza kwa kijiji cha "Al-Shurfa" kama mwanzo wa kuendelea elimu katika miaka ya 60 ya karne iliyopita, kwa nembo ya "Kitabu kwa kila mkulima mwanaume na mwanamke" mnamo mwaka 1964,  na maeneo ya kiutamaduni lilikuwa likiushiriki, na pia misikiti ilifanya somo ya kila wiki kwa jina la "Dini za mbinguni linatoa witu kujizidisha maarifa" ambapi misikiti ilikuwa msingi na roho ya mradi na sababu ya motisha ya wanakijiji wakati huo.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy