"Uruguay"... Uasi wa Watu waowaongoza kwenye Uhuru

"Uruguay"... Uasi wa Watu waowaongoza kwenye Uhuru

Imetafsiriwa na/ Osama Mustafa 
Imeharirwa na/ Mervat Sak

Leo, Uruguay inaadhimisha kumbukumbu ya uhuru wake Mnamo Agosti 25, 1825, Uruguay ilichukua hatua zake za kwanza kwenye barabara ya Uhuru, katika Mkutano wa Florida (uliofanyika tarehe hiyo), eneo la Mashariki (leo Uruguay) ilitangaza Uhuru wake kutoka Dola ya Brazil, na kujitangaza kuwa sehemu ya majimbo ya Umoja ya Rio de la Plata (sasa Argentina). Miaka michache baadaye, mnamo Agosti 27, 1828, Uruguay ilitambuliwa kama huru kabisa kutoka Argentina na Brazil na Mkataba wa Montevideo.

Tangazo hili la uhuru, lililoelezwa katika sheria iliyopitishwa na Chama cha Manaibu wa Wilaya ya Mashariki mnamo Agosti 25, 1825, lilitanguliwa na mfululizo wa maandamano yanayochukuliwa kuwa sababu kuu ya mchakato wa uhuru. 

Pengine muhimu zaidi ni Uasi wa Uruguay dhidi ya jeshi la Brazil, limelochukua eneo la mashariki tangu 1820, ambapo Harakati hii ya mapinduzi ilianza Aprili 19, 1825 chini ya Uongozi wa Juan Antonio Lavalija, na kumalizika na kuzaliwa kwa jamhuri huru "Uruguay".

Idumu Uhuru!


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy