Siku ya Kiswahili Duniani

Siku ya Kiswahili Duniani

Leo ni Kumbukumbu ya maadhimisha ya Siku ya  Kiswahili Duniani, hiyo Lugha  ambayo ni mojawapo ya lugha zinazozungumzwa katika nchi 13 za Afrika Mashariki na Kati, basi  Lugha hiyo ni lugha rasmi ya Tanzania, Kenya na Uganda, katika nusu ya mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na katika visiwa vya Comoros pamoja na lahaja ya Comoro, na uwepo wa Kiswahili hausimami katika nchi za Afrika Mashariki bali pia ilienea katika nchi za Maziwa Makuu kama vile Uganda na Congo, na pia Zambia, Malawi, Msumbiji, Somalia na Burundi, tena Kiswahili kwa herufi zake za Kilatini ni moja ya lugha tano rasmi za Umoja wa Afrika pamoja na Kiingereza, Kifaransa, Kireno na Kiarabu.

Barani Afrika, Kiswahili ni lugha pekee ya Kiafrika inayochukuliwa kama lugha rasmi katika Umoja wa Afrika, aidha, Kiswahili kimeainishwa miongoni mwa lugha 10 zinazozungumzwa na watu wengi Duniani, pamoja na kuwa lugha na taaluma ya masomo katika Vyuo Vikuu vingi vya Ulaya, Marekani, Canada, Asia na Afrika.

Mnamo mwaka 2021, kikao cha 41 cha Nchi Wanachama wa UNESCO kilitangaza tarehe Julai 7 ya kila mwaka kuwa Siku ya Kiswahili Duniani. Ulimwengu waikaribisha siku hiyo kwa shauku na msisimko kwa kuwa Kiswahili tayari kimepata nafasi yake katika vyombo vingi vya habari vya kimataifa ikiwa ni pamoja na BBC, VOA, RFI, Redio ya China, Redio za Misri zinazoelekezwa Afrika Mashariki, Redio ya Tehran, na tovuti ya Harakati ya Nasser kwa Vijana.

Kiswahili ni mojawapo ya lugha rasmi si tu katika Umoja wa Afrika lakini pia katika Jumuiya ya Maendeleo ya Afrika Kusini (SADC) na Kikundi cha Afrika Mashariki (EAC) na nchi zake zikiongozwa na Kenya, Uganda. Kwa hiyo ni lugha muhimu katika kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 na kuwezesha ushirikiano wa kikanda, haswa katika utekelezaji wa Mkataba wa Biashara Huria wa Bara la Afrika (ACFTA).

Inaashiriwa kuwa mnamo miaka ya Hamsini ya karne iliyopita, Umoja wa Mataifa ulianzisha kitengo cha lugha ya Kiswahili katika Redio ya Umoja wa Mataifa huko New York na leo Kiswahili ndiyo lugha pekee ya Kiafrika katika Kurugenzi ya Mawasiliano ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa.

Vyuo Vikuu vya Kenya na Jumuiya za Kiswahili huadhimisha siku hiyo kwa njia tofauti kwa kufanya mikutano na maandamano ya kimtandao,  na Tanzania itaadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kupitia Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKi) na pia Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA) litaadhimisha siku hiyo.