Siku ya Kimataifa kwa Watu Wa Asili Duniani

Siku ya Kimataifa kwa Watu Wa Asili Duniani

Imetafsiriwa na: Basmala El-Ghazly
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr

Leo Agosti 9, dunia inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Watu wa Asili, iliyoanzishwa na Umoja wa Mataifa(UN) mnamo mwaka 1994, ambapo watu wa asili walibaki kwa miaka mingi bila uangalizi na sauti zao hazikusikika na masuala yao ya kutengwa, umaskini na ukiukwaji wa haki hayakushughulikiwa kwenye majukwaa ya kitaifa na kimataifa.

Maadhimisho ya siku hii yamekuja kuzikumbusha nchi za dunia kuhusu haki za watu hawa na kuhakikisha zinakuwa na utaratibu na mbinu maalumu zilizotangazwa na Umoja wa Mataifa na mashirika ya haki za binadamu ili kuboresha maisha ya watu wa asili na kuwalinda ndani na nje ya nchi.

Idadi ya watu wa asili duniani inakadiriwa kuwa milioni 400, ikichukua asilimia 22 ya uso wa dunia, ikizungumza kuhusu lugha 7,000 za ulimwengu, na inawakilisha tamaduni 5,000 tofauti. Inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 86 ya watu wa asili duniani wanafanya kazi katika uchumi usio rasmi, ikilinganishwa na 66% kwa wenzao wasio wa asili.