Kumbukumbu ya miaka 60 ya uhuru wa Algeria ... mapigano ya nchi ya mashahidi milioni na kukumbatia Misri kwa mapinduzi ya Algeria

Kumbukumbu ya miaka 60 ya uhuru wa Algeria ... mapigano ya nchi ya mashahidi milioni na kukumbatia Misri kwa mapinduzi ya Algeria

leo, ndugu wa Algeria wanasherehekea Siku ya Uhuru wa 58, uhuru uliogharimu zaidi ya mauaji ya watu milioni na nusu, ambapo ukoloni wa Ufaransa uliendelea nchini humo  kwa miaka 133 umekuwa ukinyang'anya, unaiba na kujaribu kutokomeza kitambulisho cha Algeria na kusimamisha ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo, na kukandamiza njia zote za mapigano ya watu wa Algeria na kuwashinikiza kwa njia ngumu, lakini harakati za ukoloni hazikufanikiwa kuzuia upinzani na mapambano ya watu wa Algeria na kupinga utetezi wa nchi zao, basi Upinzani maarufu ulijumuisha pande zote za Algeria kwa jumla, na mapigano yakaendelea hadi mapinduzi ya ukombozi ya Algeria yalipoibuka mnamo 1954, na kutangaza vita juu ya ukoloni na  ukaribu wa mwisho wake, na mapinduzi yakaendelea kwa miaka saba, Damu za mashahidi ziliendelea kutiririka kwa ajili ya uhuru hadi mapambano haya yakipata uhuru mnamo tarehe 3 Julai 1962. Na siku ya Julai 5, ilichaguliwa iwe siku ya kusherehekea Uhuru na vijana pamoja.

Kwa upande wa kimisri ,  chini ya uongozi wa Rais marehemu Gamal Abd El Nasser, Misri iliunga mkono mapambano ya Algeria, wakati ambapo Misri ilishikilia mapinduzi ya uhuru ya Algeria na ilitoa kwake njia zote za misaada ya kijeshi, vifaa, siasa na roho pia, na nchini Misri kiongozi Gamal Abd El Nasser alimpokea Rais Bin Bella "aliyeongoza harakati ya ukombozi ya Algeria", na walijadiliana njia za kupeleka Silaha kwa watu wa Algeria, na Ben Bella alielezea kwamba mwanzoni Misri ilikuwa imempa msaada mkubwa, na kulingana na silaha zile mapinduzi ya Algeria yaliweza kuendeleza katika kufanikiwa, na Upande wa Ukombozi wa kitaifa ulifanikiwa kupigana huko pande zote za Algeria. 

Inayopasa kutajiwa ni kuwa Misri iliwekwa chini ya Uchokozi wa nchi tatu dhidi yake kwa sababu ya uungaji  mkono wake kwa mapambano ya Algeria na mapinduzi yake.

Kwa hivyo, Upande wa Ukombozi wa kitaifa wa Algeria ulitoa taarifa ukisema: " Hakuna mtu yeyote wa Algeria anayesahau kuwa Misri nchi ndugu ilishikwa na uchokozi mkali kutokana na msaada wake kwa watu wanaopambana wa Algeria, na hakuna mwalgeria mmoja anayesahau kuwa ushindi wa  watu wa Misri katika vita vya kihistoria vya Port Said sio ushindi tu , bali ushindi kwa  upande mmoja wa pande nyingi za mapigano, zinazofanyikwa huko nchini Algeria kwa muda wa miezi thelathini na minane, na watu wa Algeria wanaojihusisha katika vita vyake vikubwa vya ukombozi, hupeleka kwa ndugu wamisri, na shujaa wake adhimu Gamal Abd El Nasser, hisia za dhati za ndugu na mshikamano, na Kiarabu kidumu na kiishi  huru, na Waarabu waishi chini ya bendera ya uhuru, kiburi na utukufu." 

 

Kumbukumbu ya uhuru mwaka huu inakuja kwa njia tofauti, wakati ambapo mchakato wa kurudisha mabaki ya viongozi wa upinzani maarufu wa Algeria baada ya zaidi ya miaka 170 tangu  kuyahamishwa na kuingizwa kwenye Jumba la Makumbusho la Paris na mkoloni mkatili wa Ufaransa.

Siku njema ya Uhuru kwa wapendwa wa Algeria.