Mapinduzi ya Julai 23 ...... Hatua kuelekea kuunda mustakabali wa Misri na Bara la Afrika

Mapinduzi ya Julai 23 ......  Hatua kuelekea kuunda mustakabali wa Misri na Bara la Afrika

Imeandikwa na / Kariman Wael Al Kalamawi

Wakati wa Ujihusishaji wa wamisri kwenye Ujinga na Umaskini kulingana na kutawaliwa na matabaka na watu wanaomiliki ardhi juu ya haki nyingi zinazohakikisha Maisha Bora, kulikuwa na Jumuiya iliyoundwa kwa siri na kwa udhibiti ndani ya jeshi, inaitwa jumuiya ya Maafisa  Huru , mojawapo ya malengo muhimu zaidi ya Jumuiya hiyo ilikuwa ni kuikomboa nchi kutoka kwa Ukoloni wa kiingereza  unaotawaliwa kwa nchi hiyo na hautaki kuikomboa bila ya kuangalia idadi kadha ya majaribio. Lakini dhati ya Jumuiya hiyo na imani yake ya kufikia lengo lake ake haswa baada ya kushindwa kwa Vita vya Palastina, vilikuwa ni vitu viwili vilivyoiwezesha Jumuiya hiyo kufikia lengo lake mnamo Julai 23, 1952.

Mapinduzi yalizuka na maafisa wa jeshi walifanikiwa kuikomboa nchi, lakini nini baadaye? moja ya sababu muhimu za mafanikio ya mapinduzi hayo ni utaratibu mzuri  uliowezesha Maafisa Huru wa Jeshi kufikia malengo yao kwa nchi, ambapo walikuwa na kanuni kadhaa,muhimu zaidi ni: kuondolewa kwa mfumo wa ukabaila ili mkulima aweze kuishi maisha mazuri, na kuanzishwa  maisha bora ya kidemokrasia ambayo kila mtu anatafutia kushiriki kikamilifu katika kujenga jamii na kuunda serikali,na hatimaye kufikia uhuru wa nchi, lililokuwa lengo muhimu zaidi ambalo Maafisa Huru wa Jeshi wanataka kufikia.

Mpangilio mpya wa nchi ulianza kuunda pamoja na Uongozi wa Rais wa kwanza wa Misri Muhammad Naguib, na kisha Rais Gamal Abdel Nasser, aliyefanikiwa kuchukua hatua za ufanisi kufikia lengo muhimu, lililokuwa ukombozi wa Misri kutoka kwa ukoloni wa kigeni kwa kutaifisha Mfereji wa Suez na kuondolewa kwa vikosi vya Kiingereza moja baada ya nyingine hadi mwanajeshi wa mwisho aliondoka kutoka kwa ardhi ya Misri mnamo Juni 18, 1956.

Uhuru wa Misri haukuwa mwisho wa mapambano yaliyoanzishwa Gamal Abdel Nasser, bali alianzisha kampeni kwa uongozi wake ya kusafisha ulimwengu wa Kiarabu na Kiafrika dhidi ya janga la ukoloni kwa namna zote na udhihirisho wake, akipitia Sudan, Morocco, Ghana, Jamhuri ya Somalia na hata Namibia mwaka 1990.  

Kampeni hiyo ya maendeleo ilikuwa moja ya sababu za moja kwa moja za kuundwa kwa Bara la Afrika na ulimwengu wa Kiarabu kwa misingi ya uhuru na umoja, lakini wakati huo huo uhuru ulitiwa doa na shinikizo la kiuchumi na kijamii ambalo sote tunatumai kuwa sisi na nchi zetu ndugu tutafanikiwa kushinda ili tupite zinazojulikana kama nchi kubwa hivi karibuni.