Mchango wa Lugha ya Kiswahili katika Kukuza Mahusiano ya Afrika

Mchango wa Lugha ya Kiswahili katika Kukuza Mahusiano ya Afrika

Imeandikwa na/ Radwa Ahmed

   Lugha ya kiswahili ina mchango muhimu sana katika kukuza mahusiano ya Kiafrika, kwani Kiswahili inaeneza katika nchi mbalibali za Afrika Mashariki kama vile; Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na sehemu ndogo za Kusini mwa Somalia, Kaskazini mwa Msumbiji, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kusini mwa Ethiopia n.k, ambapo Idadi ya watu ambao wanaongea Kiswahili imefikia milioni 200.

   Lugha ya Kiswahili ni lugha muhimu hasa katika eneo la Afrika mashariki, kwa hivi Umoja wa Mataifa uliainishwa Kiswahili kama lugha ya saba duniani na lugha ya pili baada ya lugha ya kiarabu barani Afrika, na vilevile Umoja wa Mataifa ulitangaza kuwa siku ya saba  Julai ya kila mwaka ni siku ya kusherehekea Kiswahili. Barani Afrika, lugha ya Kiswahili ikawa lugha rasmi ya kazi ya Umoja wa Afrika na pia lugha rasmi ya Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC), jambo ambalo linasaidia kuimarisha na kukuza mahusiano kati ya nchi za Afrika.

   Pamoja na mabadiliko ya sasa na mwelekeo wa kuimarisha matumizi ya kiswahili katika taasisi rasmi mbalimbali, mtazamo unaonesha kwamba lugha ya kiswahili ni ndiyo huchukuliwa kama Lingua Franka kati ya nchi za Afrika Mashariki. Kuenea huku kunasaidia katika kurahisisha mawasiliano kati ya watu mbalimbali na kuimarisha ushirikiano na mahusiano kati ya nchi hizi.

   Jukumu la lugha ya kiswahili linaonekana kwenye nyanja kadhaa, hasa katika kuunganisha Kikanda baada ya lugha ya kiswahili ikawa lugha rasmi katika nchi tano: Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, na Burundi. Lugha hii inatumiwa katika shughuli na taasisi za Jumuiya ya  Afrika Mashariki kama vile Bunge, mahakama na Umoja wa forodha, na vilevile imerahisisha mawasiliano na ushirikiano kati ya nchi wanachama.

   Lugha ya Kiswahili imechangia kukuza ushirikiano wa kiuchumi kati ya Misri na Tanzania, kwani nchi hizo zimeanzisha ushirikiano wa pamoja ili  kujenga Bwawa la “Juluis Nyerere” kuzalisha umeme wa maji ambayo ni mradi mkubwa wa maendeleo ulitekelezwa nchini Tanzania kupitia kampuni ya “Elmukawlun AL-Arab” na “Elswedi Electric”. Waziri wa rasilimali za maji na Umwagiliaji wa Kimisri “Hani Swailem” na Waziri wa maji, usafi wa mazingira na Umwagiliaji wa Kenya “Alice Wahomi” waliamua kushirikiana pamoja kujenga mabwawa 10 nchini kenya, kuchimba visima 10 na kufunza wafanyakazi wakenya katika sekta ya maji na umwagiliaji, jambo ambalo linaleta manufaa kwa pande zote mbili.

   Ama kwa kiwango cha Kibiashara: Kuna ushirikiano nguvu kati ya wafanyabiashara wa kiarabu huku Afrika mwa Mashariki wameochangia kueneza kiswahili- na wafanyabiashara watanzania na wakenya.

  Kwa Kiwango wa Kitamaduni: Kiswahili ni lugha tajiri yenye fasihi, muziki na sanaa,  Waimbaji kama vile “Diamond Platnumz” na “Ali Kiba” wana maarufu kwa nyimbo zao za kiswahili nzuri ndani na nje ya Afrika pia. Umaarufu wa muziki huu unasaidia kuongezeka na kuimarisha mahusiano kati ya nchi za Afrika.

  Kiwango cha Elimu: Lugha ya Kiswahili ikawa inafundishwa sasa katika vyuo vikuu vikubwa ulimwenguni, kwani inafundishwa katika Kitivo cha Alsun (Kitivo cha Lugha), chuo kikuu cha Ain Shams. Kitivo cha Lugha na Ufasiri, chuo kikuu cha Al-Azhar. Kitivo cha Masomo na Utafiti wa Afrika. Nchini Libya inafundishwa katika sehemu za lugha ya Afro-Asian kitivo cha lugha, chuo kikuu cha Tripoli. Chuo kikuu cha Addis Ababa cha Ethiopia kilitangaza siku hizi kwamba kitaanza kufundisha lugha ya kiswahili.

    Mwishoni, Mchango wa lugha ya Kiswahili ni kubwa na muhimu sana katika kukuza mahusiano kati ya nchi za Afrika. Ili lugha kukuza zaidi, inahitaji kufanya mabadiliko kutoka watu wanaowazia kuwa lugha za ulaya ni zenye umuhimu tu, ambapo ni dhana potofu. Kama alivyosema mwanafunzi wa Ghana “Anabile Larke”: “ni wakati wa kuacha kutumia lugha ya wakoloni, na kuwa kwa Afrika kitu chetu wenyewe na kwa ajili yetu”. Ikiwa nchi za Afrika Mashariki zitafanya juhudi zaidi katika kutanganza kufunza Kiswahili katika meneo mengine, tutaweza kufikia maendeleo. Lakini jambo litahitaji nia ya kisiasa, haja ya kiuchumi na uwekazaji wa kifedha ili kujumisha maeneo yote.