Uwezeshaji wa Wanawake Kufuatia Mapinduzi ya Julai 23

Uwezeshaji wa Wanawake Kufuatia Mapinduzi ya Julai 23

Imeandikwa na: Rwan Abd El-Naby

Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr


Mapinduzi ya Julai 23 yalikuwa mapinduzi ya kibao na fahari baada ya watu wa Misri walipata uhuru wake baada ya muda mrefu wa ukoloni, kiasi kwamba Mapinduzi ya Julai 23 yalikuwa nukta ya mabadiliko ya kisiasa na kijamii kwa watu wa Misri, pia yalikuwa na mabadiliko makubwa kwa hasa kwa mwanamke wa Misri karika nyanja zote za kisiasa, kijamii, kiuchumi na afya, kwa kuwa mwanamke wa Misri wa leo anatofautiana na mwanamke wa kabla ya Mapinduzi ya Julai 23, kwani sasa hakuna ubaguzi na dhuluma kwenye elimu, kazi na haki za kisiasa.

Mapinduzi ya Julai 23 yalikuwa mwanzo wa kuwezesha mwanamke na kushikilia kwake nafasi nyingi za uongozi, Mapinduzi yale yamefungua milango ya elimu mbele ya mwanamke, kwa kuwa Rais Gamal Abdel Nasser alizingatia kumfundisha mwanamke na ushiriki wake ndani ya jamii kwa hivyo kanuni nyingi zilipitishwa kwa kulinda haki zake.


Mapinduzi ya Julai 23 na Mafanikio ya Mwanamke  


Ilikuwa muhimu kwa Mwanamke kupata haki zao kamili ili waweze kushiriki kwa undani na chanya katika maisha, na kuhusu haki ambazo zilitambuliwa kwa watu wa Misri kwa ujumla na wanawake hasa:

• Mwanamke kupata haki yao ya kupata elimu

Elimu bure iliyoidhinishwa na hayati Rais Gamal Abdel Nasser ni moja ya mafanikio makubwa ya mapinduzi ya Julai 23, yaliyopewa wanawake wa Misri, kwani elimu ilikuwa ya gharama kubwa, kwani ilikuwa ni lengo gumu kufikia, na kwa hivyo familia zilipenda kuwaelimisha wavulana na sio wasichana, lakini baada ya mapinduzi, wasichana waliweza kujiandikisha katika elimu bure na walikuwa na haki ya kupata elimu kama wanaume, na wanawake waliweza kuthibitisha thamani yao na kuthibitisha nafasi zao katika nyanja nyingi na kushikilia nafasi mbalimbali ambazo zilikuwa chache kwa wanaume tu.

• Utunzaji wa kijamii kwa mwanamke


Hayati Rais Gamal Abdel Nasser alifanya kwa kuboresha hali ya kijamii ya mwanamke, kwa njia ya miradi mingi: kama mradi wa familia zalizozalisha, mradi wa kuwawezesha wanawake vijijini, pamoja na kuorodhesha jumuiya za kijamii ambazo zinasaidia wanawake kupata elimu, mafunzo na ujuzi mwingine kuwawezesha kwa kazi.


• Uwezeshaji wa Mwanamke katika maisha ya kisiasa na Bunge


Mwanamke alipata haki yao ya kupiga kura na kushiriki kisiasa katika uchaguzi chini ya Katiba ya 1956, ambapo wanawake wa Misri waliweza kupata haki yao ya kupiga kura kabla ya wanawake kupata huko Uswizi, na ushiriki wa kwanza wa wanawake wa Misri ulikuwa katika uchaguzi wa bunge mnamo mwaka 1957, na wagombea 8 waliomba Baraza na Bi Rawya Attia alishinda, na akawa mwanamke wa kwanza kujiunga na Bunge la Misri.


• Usawa kati ya Wanaume na Uanawake "Usawa wa kijinsia"


Ubaguzi kati ya wanaume na wanawake katika nyanja zote ulikuwa kikwazo kikubwa kinachowakabili wanawake kufikia ndoto zao za elimu na kazi, na usawa ulikuwa mojawapo ya faida kubwa kwa wanawake kutoka mapinduzi ya Julai 23, ambapo kanuni ya fursa sawa kati ya wanawake na wanaume ilitumika katika nafasi zote, na kwa hivyo mishahara ya kazi hiyo hiyo ni sawa kwa wanawake na wanaume, wakati meneja mkuu wa mwanamke wa Marekani anapata mshahara wa chini kuliko mwenzake wa kiume hadi sasa.


  • Mifano ya kike katika njia ya Mapinduzi

 
  Bi. Rawya Attiya
Bi. Rawya Attiya ni mwanamke wa kwanza aliyefanya katika kazi ya kijeshi, na hii mnamo mwaka 1956 ambapo alifanya kazi kama afisa katika jeshi la Misri, na hiyo baada ya shambulio la pamoja la Uingereza, Ufaransa, na Israeli dhidi ya Misri, pia aliwafundisha wasichana 4000 kwa misaada ya kwanza wa afya na uuguzi kwa majeruhi, na alifika kwa nafasi ya kapteni wa jeshi, na katika vita vya Oktoba 1973 alikuwa mkuu wa jumuiya ya familia za mashahidi na askari, vilevile aliitwa mama wa mapigano na mashahidi, pamoja na alipata matuzo 3 ya kijeshi kutokana na jukumu lake katika huduma za jeshi la Misri. 


 Hikmat Abu Zayd


 Alijiunga kwa kitungo cha historia katika kitivo cha sanaa, chuo kikuu cha Kairo, alipata udaktari wa saikolojia kutoka chuo kikuu cha London, Uingereza mnamo mwaka 1955, na baada ya kurudi Misri aliteuliwa kama mwalimu katika kitivo cha wasichana, chuo kikuu cha Ain shams, pamoja na kupigania uhuru dhidi ya Waingereza alijiunga kwa makundi ya harakati ya upinzani kwa kijamii hadi vita vya 1956 vilianza, na alianza mafunzo ya kijeshi pamoja na wanafunzi wa kike, na mnamo mwaka 1962 alichaguliwa kama mwanachama kaika japo ya maandalizi kwa mkutano wa kitaifa, pia wakati alipojadili mkataba na Rais Abdel Nasser na kumvutia sana kwa hiyo alitoa amri ya kumteua waziri wa masuala ya kijamii, mradi wa Hikmat Abu Zayd ambao ni muhimu zaidi ni mradi wa familia zilizozalisha, na mnamo mwaka 1964 alichangia kuandaa sheria ya kwanza inayodhibiti kazi za jumuiya za kijamii, na Rais Gamal Abdel Nasser alitaka amsaidie wakati wa vita vya 1967 kwa kutunza familia za wanajeshi waliokuwa katika vita, na alifanya hiyo kwa ufanisi. 


Mwishoni, tunaweza kusema kuwa athari ya Mapinduzi ya Julai 23 kwa mwanamke inaonekana hadi leo, mnamo tarehe Machi 7, 2024 Ripoti ya Taasisi Kuu ya Takwimu ilionesha asilimia ushiriki wa mwanamke katika nafsi na kazi tofauti kwa kiwango cha nchi yote, kiasi kwamba asilimia ya wanawake wanaofanya kazi wataalamu na wataalamu wa sayansi ni 30.6%, na asilimia ya wanaofanya kazi katika ofisi ni 8.7%, Ripoti ile iliashiria kwamba mwanamke alipata wizara 6 katika Baraza la Mawaziri kwa asilimia 18%  kutoka idadi ya waziri, na alipata viti 162 ndani ya Bunge kwa asilimia 27% kutoka Bunge, na kwa kawaida mwanamke anaweza kuthibitisha uwezi wake na ufanisi wake katika maisha ya kazi au kisiasa na Mapinduzi ya Julai 23 yalikuwa kama mshumaa uliowasha moto wa uwezo wa mwanamke wa Misri.