Vijana wa " Udhamini wa Nasser " watembelea Kituo cha Uchunguzi cha Kimataifa cha Al-Azhar

Vijana waafrika wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika uliozinduliwa na Wizara ya Vijana na Michezo "Ofisi ya Vijana ya Afrika na Idara kuu ya Bunge na Elimu ya Uraia" Kwa Ufadhili wa Dkt. Mustafa Madbouly, Waziri Mkuu, mnamo kipindi cha kuanzia tarehe 8 hadi 22 Juni, kwa ushirikiano na Umoja wa Vijana wa Afrika, waliangalia
Kituo cha Uchunguzi cha Kimataifa cha Al-Azhar kwa Fatwa za Kielektroniki ili kujua kazi na jukumu lake katika kupambana na mawazo ya kigaidi Duniani, njia zinazotumika ndani yake kukabiliana na itikadi kali na mashirika ya kigaidi, na jukumu lake katika kusahihisha mawazo mapotofu, pia kueneza maadili ya kuishi pamoja na Amani kati ya wafuasi wa dini na tamaduni mbalimbali.
Washiriki walijifunza mbinu za kazi ya vitengo vya kituo , vinavyojumuisha vitengo 12 vya Kiarabu na lugha za kigeni, kupitia maelezo ya kina kwa kazi zilizofanywa na watafiti, na machapisho na tafiti maarufu zaidi ambazo kituo kinazitilia mkazo mnamo wa miaka kadhaa ya kazi yake yote.
Kwa upande wao, Vijana walielezea Furaha yao kwa juhudi za kituo cha Al-Azhar katika kuangalia , kufuatilia kuchambua mijadala yote yenye misimamo mikali, na wakisifu jukumu la kituo cha Al-Azhar katika kueneza maadili ya kuishi pamoja na Amani kati ya wafuasi wa dini na tamaduni mbalimbali.