"Michezo na Afrika" ndani ya Shughuli za siku ya pili ya "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kiafrika "

"Michezo na Afrika" ndani ya Shughuli za siku ya pili ya "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kiafrika "
"Michezo na Afrika" ndani ya Shughuli za siku ya pili ya "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kiafrika "
"Michezo na Afrika" ndani ya Shughuli za siku ya pili ya "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kiafrika "
"Michezo na Afrika" ndani ya Shughuli za siku ya pili ya "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kiafrika "

Mkuu wa Shirikisho la Muungano wa Michezo Afrika “USCA” Meja Jenerali Ahmed Nasser alisisitiza umuhimu wa jukumu la Michezo Barani Afrika haswa kusababisha aina ya ushindani kwa kuzingatia hamu ya kila mmoja kwa kushiriki katika mikutano ya kimataifa, akiashiria kwamba Michezo ni nguvu laini inayohakikisha ukaribu kati ya watu waafrika na kufanya kile ambacho hakiwezekani kutoka kwa Siasa.

Hiyo ilikuwa wakati wa kikao cha "Michezo na Afrika" ndani ya Shughuli za siku ya pili ya " Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kiafrika " uliozinduliwa na Wizara ya Vijana na Michezo  (Ofisi ya vijana ya Afrika na Idara kuu kwa Ubunge na Elimu ya kiraia) ukiwa na Ufadhili wa Dkt. Mustafa Madbuli "Waziri Mkuu", mnamo kipindi cha tarehe ya 8 hadi 22 Juni, 2019,kwa ushirikiano wa Umoja wa Vijana waafrika, katika Kituo cha Elimu ya Uraia huko Algazira.

Nasser aliashiria kuwa "USCA" ina jukumu kubwa katika maelewano kati ya Misri na Afrika kwa kupitia usambazaji wa Michezo mbalimbali na inaunga mkono kwa nchi za bara la Afrika kuunda mahusiano ya michezo, inayohakikisha ushirikiano wa Misri na Afrika katika michezo, kuashiria kuwa "OSCA" ni ufupisho wa neno la Kifaransa lenye maana ya "Shirikisho la  Muungano la Michezo la Afrika" unajumuisha mashirikisho 60 ya michezo ya Afrika, na pia ina jukumu la kusimamia mashindano ya michezo ya Afrika kwa upande wa kifundi na inazingatia upande wa tatu wa pembetatu ya michezo Barani Afrika pamoja na Shirikisho la Kisiasa la Afrika na Shirikisho la Kamati za michezo ya Olimpiki "ANOC", ambayo hupanga na husambaza Michuano.

Nasser alisifu jukumu la Wizara ya Vijana na Michezo inayoongozwa na Dkt.Ashraf Sobhy katika kuunga mkono na kuthibitisha ushirikiano wa kimichezo kati ya mashirikisho yote ya michezo Barani Afrika na uungaji mkono wake kwa mashindano yote yanayoandaliwa na USCA na ANOC huku ,akiashiria juhudi na uangalifu wa Wizara hiyo katika kufanikisha mashindano hayo. kueneza michezo mbalimbali ndani ya Bara la Afrika kwa kuanzia dhima yake ya kijamii katika namna ya kujitolea michezo Kuhudumia jamii ya Afrika ili kutekeleza maoni ya Rais Abd El Fatah El-Sisi ya kuimarisha mahusiano na nchi zote za Afrika.

 

Alitangaza ushirikiano na Wizara ya Vijana na Michezo katika kuandaa mkutano wa kupambana na ufisadi katika michezo Barani Afrika, ambalo limepangwa kufanyika mjini Kairo.

Huko Vijana waafrika walioshiriki katika kikao hicho wakiwasilisha uzoefu wao wa kimichezo na majiribio yao katika michezo mbalimbali katika nchi zote za kiafrika.

 Kwa upande wake, Mkuu wa Shirikisho la Michezo la Afrika (Michezo kwa Wote) Dkt.Imad Al-Banani alisisitiza juhudi za Misri na maandalizi yake ya kuandaa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, huku akionesha jukumu la Wizara ya Vijana na Michezo inayoongozwa na Dkt. Ashraf Sobhy katika kuwaunganisha Vijana waafrika kwa kupitia matukio ya kimichezo yanayoandaliwa na Wizara hiyo, akisisitiza kuwa michezo ni uchawi wa bara la Afrika akiashiria kuwa Vijana wa bara hilo  ni hazina yake, inayohakikisha Maendeleo na ukuaji kwa nchi yao.