Ziara ya kiutalii ya Vijana wa " Udhamini wa Nasser" kwa Ngome ya Qaitbay na Klabu ya Uvuvi

Vijana waafrika wanaoshiriki katika " Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika " walitembelea  kituo cha kijeshi cha Ras El-Tin huko Mkoa wa Aleskandaria, ambapo walisikiliza maelezo ya kina kuhusu juhudi zilizofanywa na kituo cha kijeshi kwa kulinda nchi hiyo.

Hiyo ilikuwa miongoni mwa shughuli za siku ya nane ya "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika" uliozinduliwa na Wizara ya Vijana na Michezo (Ofisi ya Vijana ya Afrika, Idara kuu ya Bunge na Elimu ya kiraia), kwa Ufadhili wa Dokta Mostafa Madbouly, Waziri Mkuu, na kwa Ushirikiano na Umoja wa Vijana wa Afrika, mnamo kipindi cha  8 hadi 22 Juni 2019 katika Kituo cha Elimu ya kiraia huko Al Gazira.

Shughuli za siku hiyo pia zilikuwa pamoja na ziara ya kutembelea Ngome ya Qaitbay ili kujua nafasi yake ya kihistoria katika kukabiliana na Uvamizi na kulinda Usalama wa Misri, ambapo Vijana waafrika walitembelea ghorofa ya kwanza iliyokuwa na msikiti wa Ngome, na ghorofa ya pili ina korido, kumbi na vyumba vya ndani, pia ina chumba kikubwa cha Baraza la Sultan Qaitbay, na shughuli za siku zilihitimishwa kwa safari ya Bahari ndani ya klabu ya Uvuvi huko Aleskandaria.