Waziri wa Kilimo apokea Vijana wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo

Waziri wa Kilimo apokea Vijana wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo

Dkt. Ezz Eldin Abu Steit, Waziri wa Kilimo na Uhifadhi wa Ardhi, aliwapokea Vijana waafrika walioshiriki Udhamini wa "Nasser"  kwa Uongozi wa Kiafrika" katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo, wakati wa shughuli za Udhamini wa "Nasser"kwa Uongozi wa Kiafrika" uliozinduliwa na Wizara (Ofisi ya Vijana wa Afrika na Idara kuu ya Bunge na Elimu ya Kiraia) pamoja na uangalizi wa Dkt. Mostafa Madbouly, Waziri Mkuu, mnamo kipindi cha kuanzia tarehe 8 hadi 22, mwezi wa Juni, mwaka wa 2019, kwa ushirikiano na Umoja wa Vijana wa Afrika.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Dkt. Mohammed Soliman, Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo, Dkt. Naiem Moselhi, Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Jangwa, na Dkt. Shereen Assem, Katibu Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo.

Katika mkutano huo, Waziri wa Kilimo alisisitizia kuwa Misri, linaloongozwa na Abdel Fattah El-Sisi, inajali kuamsha ushirikiano pamoja na bara la Afrika, akiashiria maoni na mkakati wa Misri katika kunyonya mali na rasilimali watu zote zilizopo  Barani Afrika ili kuhakikisha maendeleo endelevu.

Pia, Abu Steit alionesha juhudi za Misri na ushirikiano wa pamoja na bara la Afrika katika uwanja wa kilimo, kulingana na maagizo ya Umoja wa Afrika, akibainisha kuwa kuna mashamba manane ya Kimisri Barani Afrika yanayofanya kazi ndani ya mfumo wa mafunzo na ugani, yanayotarajiwa kuongezeka hadi 22 ifikapo mwisho wa mwaka wa 2020.

Abu Steit alieleza kuwa Ushirikiano wa Misri na Afrika ulikuja tangu enzi za hayati Rais Gamal Abdel Nasser mnamo wa mkutano wa kwanza wa kilele wa Afrika uliofanyika huko Addis Ababa mwaka wa 1963, akiashiria harakati za ukombozi zilizoongozwa na Abdel Nasser katika kiwango cha kisiasa Barani Afrika, zilizoakisi katika maendeleo na ushirikiano wenye tija na bara la Afrika, haswa kuwa kilimo ni nguzo kuu katika maendeleo ya mahusiano kati ya watu.

Waziri huyo aliashiria kuwa uzalishaji wa kilimo unazingatia kama mhimili mkuu unaotegemewa na nchi za Afrika, akisisitiza kuwa ushirikiano wa pamoja kati ya Misri na Afrika unategemea kufanya mikataba na itifaki nyingi zinazochangia maendeleo ya bara la Afrika.

Vilevile, Naibu Katibu Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Dkt. Shereen Assem alionesha juhudi za kuanzisha mashamba ya pamoja katika nchi za Afrika na historia ya Misri na Afrika katika nyanja ya kilimo. Pia aligusia mtazamo na mkakati wa Wizara ya kilimo katika nchi za Afrika na nyanja za ushirikiano wa pamoja na msaada kwa nchi mbalimbali.

Pia, aliwatambulisha Vijana wa Afrika kwa Kituo cha Utafiti wa Kilimo, Kituo cha Utafiti wa Jangwa, nyanja zao, na vituo vyote vilivyohusiana na wizara ya kilimo. Na pia, aligusia programu ya kuendeleza mashamba ya Misri katika nchi za Afrika, pamoja na miradi ya kurejesha ardhi ya kilimo.

Mkutano huo ulimalizika kwa ziara ya ukaguzi ndani ya kituo cha utafiti, iliyojumuisha maabara ya vipengele vya utafiti, uchambuzi wa maji, sumu kuvu, uchafuzi wa kikaboni, vipengele vya udhibiti, bioteknolojia, usalama wa chakula, kupima na kuweka daraja kwa nafaka, na vimiminika  ya kibaolojia.