Ubalozi wa Yemen mjini Kairo apokea wahitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa 

Ubalozi wa Yemen mjini Kairo apokea wahitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa 

Mohamed Marem, Balozi wa Jamhuri ya Yemen mjini Kairo, aliwapokea wawili Muhammad Abdullah, na Suleiman Bashadhi, wahitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, toleo la tatu, katika makao makuu ya Ubalozi wa Yemen kwenye Jamhuri ya Kiarabu ya Misri.

Mkutano huo ulishughulikia kutambulisha Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa  katika toleo lake la tatu, kujadili jinsi ya kuamsha na kutekeleza ushirikiano wa nchi mbili kati ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri na Jamhuri ya Yemen katika upande  wa vijana, na kujadili shughuli na programu zinazoweza kutekelezwa mnamo kipindi kijacho. Kwa upande wake Balozi huyo amewapongeza vijana wa Yemen wanaoshiriki katika kongamano hilo la kimataifa  akiashiria kuwa nchi hiyo inahitaji vijana  hodari na wenye bidii, pia  ubalozi huo hautaacha jitihada zozote katika kuwaunga mkono na kuwasaidia vijana wa Yemen katika kuendeleza ubunifu na kipaji chao katika nyanja tofauti za elimu na maarifa.

Mwishoni mwa mkutano huo, Balozi Marem aliwatunukia vijana walioshiriki ngao ya ubalozi na medali za kutia moyo, ili wahamasishwe kufikia Ubora  na ubunifu zaidi wa kuihudumia nchi na kuiendeleza mnamo siku zijazo.

Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri ilikuwa  imeandaa shughuli za Udhamini wa Nasser  kwa Uongozi wa Kimataifa, katika toleo lake la tatu pamoja na Ufadhili wa  Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kwa Ushiriki wa viongozi vijana 150 kutoka  nchi  zisizofungamana kwa upande wowote  na nchi rafiki, mnamo kipindi cha kuanzia tarehe  Mei 31 hadi  Juni 17, 2022  kwenye Jumba la Mamlaka ya Uhandisi mjini Kairo.

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unalenga kuwasilisha uzoefu  mkale wa  Misri katika kuanzisha na kujenga taasisi za kitaifa, pamoja na kuunda kizazi cha viongozi vijana kutoka nchi zisizofungamana kwa upande wowote wenye maoni yanayosambamba na ushirikiano wa Kusini-Kusini, na kuongeza ufahamu wa jukumu la harakati ya kutofungamana kaa upande wowote kihistoria na jukumu lake mnamo siku zijazo, pamoja na kuamsha jukumu la kundi wa vijana wa nchi wanachama katika  harakati isiyofungamana kwa upande wowote NYM, na kuunganisha viongozi vijana wenye athari kkubwa katika ngazi ya nchi zinazofungamana kwa upande wowote  na nchi rafiki .

Pamoja na kutoa fursa sawa kwa jinsia zote mbili kama vile lengo la tano la Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 linavyoainisha, vilevile kuwawezesha  vijana  na kuwapa washiriki wa nchi ulimwenguni fursa ya kujuana na kuanzisha mashirikiano katika nyanja mbalimbali, si tu Barani, bali  kimataifa pia , kama vile  lengo la kumi na saba la malengo ya Maendeleo Endelevu linavyoashiria.