Siku ya Kimataifa ya Utofauti na Diplomasia kwa Amani

Siku ya Kimataifa ya Utofauti na Diplomasia kwa Amani

Imetafsiriwa na/ Amira Roshdy 
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled


"Sijui kuwa kuna enzi ambayo watu wa ulimwengu wameungana kwa lengo moja, kama wanavyofanya enzi ya kisasa, kwa kushirikiana kwa juhudi za kufanikisha mifumo ya kimataifa wa kufanya kazi, je, tunaweza kufikia matumaini yetu ili iwe ukweli wa kisasa?"

- Rais Gamal Abdel Nasser katika Mkutano wa Bandung,  mnamo Aprili 1955

"Kamati Kuu ilipitisha uamuzi wa kutangaza "Siku ya Kimataifa ya Uanuwai wa Vyama na Diplomasia kwa ajili ya Amani " (A/73/L.48) mwezi wa Desemba, mwaka wa 2018, kwa kura zilizosajiliwa kwa idadi kubwa ya kura 144, na iliiomba Kamati Kuu pamoja na nchi wanachama, watazamaji na Mashirika ya Umoja wa Mataifa kusherehekea Siku ya Kimataifa mnamo Aprili 24, kila mwaka kwa lengo la kuhamasisha  Uanuwai wa Diplomasia kwa ajili ya Amani.

Na vilevile, kuangazia umuhimu wa kudumisha maadili ya ubunifu na ushirikiano wa kimataifa, ambayo yanajengwa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa na Mpango Endelevu wa Maendeleo wa mnamo mwaka wa 2030, kama msingi wa kusaidia na kuimarisha nguzo tatu za Umoja wa Mataifa - maendeleo, haki za binadamu, na amani na usalama, kama jambo muhimu katika kuongeza kiwango cha kufuata viwango vya kimataifa na mifumo na kanuni zilizosimamia mahusiano ya kimataifa katika miongo saba iliyopita dhidi ya ubinafsi na changamoto zinazoongezeka zinazotokana na hilo. Aidha, masuala ya kimataifa, kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, mvutano wa kijiografia, na migogoro ya kibinadamu katika maeneo mbalimbali, yanahimiza kupata makubaliano yanayoheshimu maadili na maslahi ya mataifa, na yanahitaji uangalifu na kazi ya pamoja kupitia ubunifu na diplomasia.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy