Ziara kwa Makumbusho ya Misri
Leo, Ijumaa, Wizara ya Vijana na Michezo imeandaa ziara ya Makumbusho ya Misri kwa washiriki wa Udhamini wa Nasser wa Afrika", ikiwa ni miongoni mwa ya shughuli za siku ya 14 ya Udhamini huo.
wakati wa ziara yao kwenye makumbusho ya kimisri, washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika walitazama yaliyomo ndani ya Makumbusho ya Misri, ambayo ni mojawapo ya makumbusho makubwa na maarufu zaidi ulimwenguni ambapo
yanajumuisha zaidi ya vibaki 150,000 . vilevile , walitazama vitu vya kale vizito kama vile majeneza ya mawe, masanamu, michoro ya ukutani,maandishi,
Sanamu za miungu, maiti za kifalme,vitu vikale vya maisha ya kila siku, picha za mummy, nakshi hazijakamilika, masanamu na vyombo vya Wagiriki na Waroma, na mambo ya kale maalum yanayohusiana
na itikadi ya maisha mengine, pamoja na kupiga picha za kumbukumbu mwishoni mwa ziara yao.