Wajibu wetu sasa ni Kuendelea Kujitahidi

Imefasiriwa na / Zeinab Mekky
Ndugu zangu:
Ningependa mfahamu kuwa mapinduzi haya ni mapinduzi yanayowakilisha matumaini na hisia za nchi, na msingi wa kuyaendeleza ni imani yake kwamba ni kielelezo cha kanuni, malengo na maadili na mafanikio ya matarajio ya wananchi walioendelea, na hivyo ni lazima kuhifadhi mapinduzi kwa ajili ya watoto na wajukuu wetu.
Na ikiwa tunaweza kuelewa mapinduzi kwa msingi huo, basi mapinduzi yanasonga mbele bila shaka. Watu wamehukumiwa kuangamia, lakini kanuni na malengo ndiyo yanayodumu kwa vizazi.
Baba zetu na babu zetu walidai kanuni hizi, lakini hazikufikishwa, ni wajibu wetu sasa kuendelea kujitahidi katika njia hiyo hadi tufikie malengo hayo.
Kwa hivyo, tunaweza kufungua njia ... njia ya ukuu, nguvu, na ushindi wazi kwa uhuru na ukombozi wa watu hawa.
Tulikuwa tukihisi jinamizi hilo lililotulia vifuani mwetu, lakini leo tumekombolewa na ni lazima tuendelee kujitahidi hadi tuondoe kabisa jinamizi hilo, na mpaka tuondokane nali kabisa.
(Hapa mmoja wa waliohudhuria alirudia kasema, “Usiwaache nyoka hawa tena.” Gamal Abdel Nasser, Bakbashi, akamjibu.)
Maadamu mmekuwa na Umoja na Mshikamano, haiwezekani kwa nyoka kuonekana juu ya vichwa vyenu, na ni lazima tuungane na kuhakikishiwa na kamwe tusiwe wazembe; ili nguvu za nyuma haziwezi kutushinda tena. Mapinduzi ni mapinduzi ya malengo na kanuni, na maadamu kanuni na malengo hayo yapo, hakuna nyoka atakayeweza kuinua kichwa chake.
(Na hapa mmoja wa wafanyakazi alisema kuwa sisi wafanyakazi katika makampuni tunahisi kuna mite anaitafuna mifupa yetu, lakini unajua kabisa sisi ni nguzo za mapinduzi, unatukuta kila mahali, tayari kuondoka mara moja. kwenye mfereji na sisi tuko ovyo wenu.
Gamal Abdel Nasser akamjibu akisema)
Mite hiyo iko kila mahali, na jukumu letu sasa ni kukamata mite hiyo, na kuonesha kila mtu nafasi yake katika nchi hii.
Ni jambo lisilowezekana kabisa siku ikipita tunamwambia mfanyakazi kuwa kampuni hiyo ni yenu, anayekwambia hivi anakupotosha, na inabidi twende hatua kwa hatua katika kufikia haki ya kijamii miongoni mwa wananchi, na nchi lazima kwa nchi kuendeleza hatua kwa hatua.
Na ikiwa tuliweza kufikia usawa, basi asili ya mambo inahitaji kwamba kila mtu afanye kazi kwa ajili ya mwingine na kwamba wote washirikiane kwa ajili ya ufufuo wa nchi ; ili tuongeze pato la taifa ili tuishi maisha bora.
Tunataka wafanyakazi na wajasiriamali watembee kwa umoja, tukijibu madai yote ya wafanyakazi na kuacha madai ya makampuni, basi matokeo yake ni ongezeko la wafanyakazi wasio na ajira; kwa hivyo, hakuna kampuni itaanzishwa na watoto wako hawatapata kazi.
Hatuwezi kumlazimisha mmiliki wa kampuni kujibu madai yote mara moja; Kwa sababu hii inasababisha kutoweka kwa mtaji, na maslahi ya juu ya nchi yanatuamuru kwamba, kwa upande wetu, tuwatie moyo wamiliki wa mitaji ili makampuni yaenee nchini kote.
Na mjue kwamba serikali haina fedha za kutosha kufanya ufufuaji wa kutosha wa viwanda; lakini lazima tuwahamasishe kila anayetaka kuwekeza fedha zake ili nchi na wafanyakazi wanufaike.
Na tutafanya kazi kila wakati kuleta maoni karibu ili kila mtu achukue sehemu yake ya maisha hayo, na ni jukumu lenu kushikamana na kushirikiana kwa ajili ya kuinua nchi hiyo.
Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser katika ujumbe wa wafanyikazi wa Kafr El Dawar.
Mnamo Aprili 7, 1954.