Siku ya Uhuru wa Algeria

Kumbukumbu ya miaka 61 ya Uhuru wa Algeria.. Mapambano ya nchi ya mashahidi milioni na kukumbatia Misri kwa mapinduzi ya Algeria
Leo, Watu ndugu wa Algeria wanasherekea siku ya Uhuru ya miaka 61, Uhuru ambao ulilipwa na mashahidi zaidi ya milioni moja na nusu, ambapo Ukoloni wa kifaransa nchini humo uliendelea kwa miaka 133, unaondoa, unapora, unataka kufuta utambulisho wa Algeria na ulikomesha ukuaji wa kistaarabu wa nchi, na zima njia zote za upinzani wa watu wa Algeria na kuweka shinikizo kwao kwa njia za kikatili mbaya zaidi, Lakini mazoea ya ukoloni hayakufaulu katika kuzima upinzani na mapambano ya Watu wa Algeria na ujasiri wao katika kulinda ardhi yao, Upinzani wa wananchi ulijumuisha maeneo yote ya Algeria kwa ujumla, na mapambano yaliendelea hadi mapinduzi ya ukombozi wa Algeria yalipoanza mwaka 1954 kutangaza vita dhidi ya ukoloni na kukaribisha mwisho wake, Mapinduzi yaliendelea kwa miaka saba, na damu ya mashahidi ilimwagika kwa ajili ya uhuru hadi mapambano haya yalifikia kilele cha uhuru mnamo Julai 3, 1962. Tarehe 5 Julai ilichaguliwa kusherehekea Siku ya Uhuru na Vijana pamoja.
Kwa upande wa Misri, kwa uongozi wa Hayati Rais Gamal Abdel Nasser, Misri ilichukua hatua ya kuunga mkono mapambano ya Algeria, kwani Misri iliyapitisha mapinduzi ya ukombozi wa Algeria na kuyapatia msaada wa kijeshi, mali, kisiasa na kimaadili pia.
Huko Misri, kiongozi Gamal Abdel Nasser alimpokea Rais Ben Bella, aliyeongoza Chama cha Ukombozi wa Algeria, na kujadiliana naye njia za kusambaza silaha kwa Waalgeria, na Ben Bella alieleza kwamba Misri imempatia msaada mkubwa tangu mwanzo, na kutokana na silaha hii, mapinduzi ya Algeria yaliweza kupiga hatua , na National Liberation Front ilifanikiwa kupigana vita kote Algeria.
Ikumbukwe kuwa Misri ilifanyiwa uchokozi wa pande tatu dhidi yake kwa sababu ya kuunga mkono mapambano ya Algeria na mapinduzi yake.
Kutoka hapa Umoja wa kitaifa wa Ukombozi wa Algeria ulitoa taarifa ambapo ulisema : "Mualgeria yeyote hasahau kuwa ndugu wa Misri ilikabili mashambulizi mabaya ambapo Misri ilikuwa ni mwathirika wa uungaji mkono wake kwa Algeria na Mualgeria yeyote hasahau kwamba ushindi wa Wamisri katika Vita vya kihistoria vya Port Said ni Ushindi wa Misri ni moja tu ya mapambano mengi yanyotokea nchini Algeria tangu miezi 38 iliyopita, Waalgeria wanaoshiriki katika vita vyake kubwa vya ukombozi watatoa kwa watu ndugu wa Misri na shujaa wake wa milele, Gamal Abdel Nasser, kwa dhati hisia za udugu na mshikamano, uarabu utaishi kwa uhuru wa milele na Waarabu wataishi chini ya bendera ya uhuru, kiburi na utukufu."
Kumbukumbu ya Uhuru ya mwaka huu inaonekana inakuja kwa njia tofauti ambapo inakabiliana na mchakato wa kurejesha mabaki ya viongozi wa upinzani maarufu wa Algeria baada ya zaidi ya miaka 170 iliyopita tangu kuyahamisha kwenye makumbusho ya Paris na koloni katili la Ufaransa.
Muwe na Mwaka mwema na kila la heri ndugu zetu wa Algeria.