Katika mapambano yetu tunajitegemea wenyewe tu
Hisia ambayo nilihisi miongoni mwenu hapa ni nguvu kubwa ambayo tunathamini,na isiyotegemea mapambano yenye muda mrefu yaliyosababisha Umoja isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu na hisia zenu na nguvu za watu wa Kiarabu.
Hisia hii na Imani hii - Enyi Ndugu- ni uwezekano kutoka Mwenyezi Mungu alizotuletea ili tuweze kupambana hadi tushinde.
Leo -Enyi Ndugu-mmepata ushindi baada ya mapambano ya muda mrefu na mmeanzisha Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu kwa utashi wenu, hivyo tunathamini hisia na imani hii, pia tunathamini uaminifu huo, kwani kwa nguvu za hisia,imani na uaminifu kati ya wananchi katika maeneo yote ya Jamhuri sote tunaweza kwa msaada wa Mwenyezi Mungu kufanya bidii kufikisha malengo na matumaini.
Enyi Ndugu:
Leo tunapopokea siku ya kwanza ya Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu na tunaomba kutoka Mwenyezi Mungu atuletee Ushindi, Umoja, Muungano, Uaminifu na Imani.
Sisi -Enyi Ndugu- katika mihangaiko yetu hatutegemii isipokuwa sisi wenyewe , hatutegemea mgeni au mvamizi , lakini tunapopambana tunategemeana pamoja , tena Jamhuri nzima inategemea wana wake na wananchi, basi leo wananchi katika Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu Umoja wakawa chanzo cha nguvu na Imani .
Enyi Ndugu:
Kwa nguvu za wananchi na imani yao, Jamhuri yenu ya Kiarabu iliweza kushinda Waingereza, Wafaransa na Waisraeli … Jamhuri yenu nguvu - ambayo iliungana kabla ya Umoja rasmi ijulikane na iliyopigana katika kaskazini na kusini – imeweza kushinda Uchokozi na kupoteza mataifa makubwa; kulingana na Imani na ujasiri za Wananchi.
Leo –Enyi Ndugu – nyinyi mlijenga Jamhuri hiyo, mlipendelea kudhibiti, na mlitangaza sera ya kujitegemea na kutangaza kwamba wananchi wa kiarabu ambao wanakombozi Waarabu waliokombolewa lazima wasaidie ndugu zao wanaopigana katika nchi zilizonyakuliwa, na wale wanaopiga vita ukoloni.
Leo -Enyi Ndugu- tumeanzisha nguzo huru ya Kiarabu katika pande zote za Jamuhri hii. ambapo kwa Imani na Umoja mliweza kuunganisha nchi za kiarabu , na kwa Imani pia kwa Mshikamano tutaweza kuimarisha nguzo za Jamuhri hiyo, tuwe daima ngoma ya Uhuru na Umoja wa kiarabu...na kwa Imani na Umoja- Enyi Ndugu- tutafikia malengo na matarajio yote.
Leo, katika Jamhuri hii ,tunawakilisha wazo moja, ambalo ni wazo la Uhuru na Utaifa wa Kiarabu.tutashikamana pamoja- Kwa Uweza wa Mwenyezi Mungu- kuthibitisha njia za Uhuru, na kukuza misingi ya Utaifa wa Kiarabu.
Ninyi ni maaskari na ninyi ni jeshi kubwa; Jamhuri nzima, pamoja na wanawe wote, itaunda jeshi kubwa, na vikosi vya jeshi havitakuwa mstari wa mbele ambao husonga mbele, lakini kila wakati tutakuwa mmoja wetu askari ambaye atajizatiti kwa nguvu wake, na imani yake, silaha yake mpaka tuondoe vitimbi vya wavamizi.
Hiyo - Enyi Ndugu- ni Jamhuri yenu ya Kiarabu katika siku zake za kwanza, haya -Enyi Ndugu- ni athari za Umoja, tumtegemee Mwenyezi Mungu, na tusonge mbele kwa nguvu, ujasiri na imani.. Mungu ndiye msaidizi wenu.
Assalamu Alaikum warahmat Allah.
Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser mjini Aleppo.
Mnamo Machi 16, 1958.