Maadui wa Taifa la Kiarabu wamekuwa wakijaribu kwa kila njia kutenganisha baina ya watu wake na kuzigawanya nchi za Kiarabu
Imefasiriwa na / Aya Nabil
Kweli, kipindi nilichotumia pamoja nanyi ni mojawapo ya vipindi vyenye furaha zaidi nilivyoweza kuhisi, kwa sababu daima kilionesha hisia hizo za heshima, kilionesha undugu na upendo ambazo ni kanuni ya Umoja wa Taifa la Kiarabu bila sheria. Undugu baina ya watu wa Kiarabu katika kila nchi ya Kiarabu, na upendo baina ya Waarabu katika kila nchi ya Kiarabu, tunajiamini sana siku zijazo kwa msaada wa Mungu.kwani tuko njiani kwa ajili ya fahari ya nchi yetu na fahari ya Waarabu wote. tunategemea roho hii inayotoka katika kila nchi ya Kiarabu na kila kijiji cha kiarabu, bila kukutana na watu wake, ni kukutana tu kwa hisia, au kukutana katika upendo wa Taifa letu la Kiarabu, katika uhuru wa nchi yetu ya Kiarabu, na katika kufanya kazi kwa ajili ya Ukuu wa Taifa la Kiarabu.
Maadui wa Taifa la Kiarabu wamekuwa wakijaribu kwa kila njia kuwatenganisha watu wake, na kutenganisha baina ya mataifa ya Kiarabu, na kueneza kampeni za chuki baina ya watu wa Kiarabu katika kila nchi ya Kiarabu.Nchi Ndugu ya Lebanon imekuwa ikikabiliwa na kampeni hizo kwa muda mrefu, na bado kampeni za chuki zinaendelea kuzuka kote nchini Lebanon na katika ulimwengu wa Kiarabu. Zamani kampeni hizo zilifanywa na makundi ya wakoloni wa Magharibi, na sasa zinafanywa na makundi ya wakoloni na wafuasi wa ukoloni, kama vile makundi ya kikomunisti wanavyofanya wanajaribu kuvunja Umoja wa watu wa Kiarabu ili kututawala na kututiisha.
Lakini roho hii na ufahamu huu... Ufahamu mkubwa ambao nimegusa katika kila tukio, na ambao unanifanya niamini zaidi kwamba taifa la Kiarabu, baada ya kuteseka kwa muda mrefu katika siku za nyuma, limeamua kuwa na silaha za ufahamu ili kusimama dhidi ya maadui zake; ufahamu huu ni silaha yetu dhidi ya wale wanaotaka kututawala, dhidi ya wale wanaoeneza chuki na uhasama miongoni mwetu,na dhidi ya wale wanaotutamani,wawe wakoloni au wakomunisti,kwa hiyo tunaelekea siku zijazo kwa dhamira na imani, kwa udugu, upendo na mshikamano.tunakwenda kwa siku za usoni tukiunganishwa na Umoja.. Umoja wa mioyo, Umoja ulioudhihirisha leo kwa hisia hizo nzuri zinazodhihirisha upendo safi, upendo usiotaka bei, na hautaki chochote isipokuwa imani yake katika haki yake ya uhuru na haki yake ya kuishi, akiwa bega kwa bega na ndugu zake Waarabu katika kila nchi ya Kiarabu.”
Roho hii na hisia hizi nilizoziona leo; ni silaha yetu kuu katika vita vyetu vikubwa kwa ajili ya uhuru na mshikamano wa Taifa la Kiarabu, kwa ajili ya Umoja wa Waarabu dhidi ya maadui wa Waarabu, kwa ajili ya mshikamano wa Waarabu dhidi ya maadui wa Waarabu, kwa ajili ya kuunda nchi ya Kiarabu yenye heshima katika kila nchi ya Kiarabu, na kwa ajili ya Umoja wa Kiarabu ambao sasa unatuunganisha pamoja hapa bila Umoja wa kikatiba wala Umoja wa kisheria, kwa sababu ni Umoja wa hisia. Na umoja ambao tunauonesha kwa kubadilishana hisia, kubadilishana upendo, kubadilishana udugu, kubadilishana matumaini ya mema kwa kila mmoja wetu katika nchi yoyote ya Kiarabu.
Huo ndio Umoja wa kweli unaotuunganisha na chochote kinachotokea Lebanon kinatuathiri kwetu, chochote kinachotokea kwetu kinatokea Lebanon, chochote kinachotokea kwa nchi yoyote ya Kiarabu kinatokea kwetu sote. Huo ndio umoja wetu, na huo ndio ufafanuzi wetu wa Umoja wa Kiarabu; Umoja wa kuungana dhidi ya maadui zetu, sio Umoja unaotegemea pupa, wala umoja unaotegemea kufanya kazi kwa ajili ya wageni, wasaidizi wa ukoloni au kwa ajili ya wageni kwa utegemezi, lakini ni Umoja safi bila tamaa, bila msaada wa kikatiba. Na ndiyo inatuleta hapa sasa, Sisi ni wana wa Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu na wana wa Lebanon, na sote tunahisi upendo ukipepea juu ya vichwa vyetu, udugu unatuunganisha, na hisia nzuri na matumaini mazuri hutoka kwa hisia zetu na hutoka katika roho zetu.
Kwa roho hii tunatumaini katika siku zijazo, na kwa roho hii tunahisi kwamba kuna nguvu kubwa nchini Lebanon dhidi ya kampeni za chuki zinazolenga Lebanon kama zinalenga Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu, dhidi ya kampeni za chuki zinazolenga kutuvuta sote kujisalimisha kwa utawala wa ukoloni,na dhidi ya kampeni za chuki ambazo Wakomunisti wanafanya ili kutufunga kwenye gurudumu la utegemezi.
Kwa imani hii, kwa roho hii njema, kwa upendo huu, pamoja na udugu huu, tutashinda daima - kwa uweza ya Mwenyezi Mungu - mnamo siku zijazo kama tulivyoshinda zamani.
Nawatakia nyinyi na nchi ndugu ya Lebanon na Rais wa Lebanon, kila fahari maendeleo yote na ustawi, na nawaomba kuwapelekea watu wa Lebanon salamu zangu na hisia za watu wa Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu, na asanteni sana.
______________
Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser kwa wajumbe wa Lebanon kutoka Ikulu Mjini Kairo.
Mnamo Aprili 23, 1959 .