Je, Mfalme Farouk alitaka kutaifisha mfereji wa Suez?

Je, Mfalme Farouk alitaka kutaifisha mfereji wa Suez?

Imeandikwa na Dkt / Ali Al Hefnawy

Mbele ya kamati ya wataalamu, katika Chuo Kikuu cha Sorbonne, huko Paris, mwaka wa 1951(kabla ya mapinduzi) baba alipotetea kwenye utafiti wake wa Uzamivu katika sheria ya kimataifa kuhusu haki ya Misri katika kutaifisha mfereji wa Suez, hakutarajia uungaji mkono mkubwa wa Mfalme Farouk kwa ombi hili. Nini kilichotokea?

1-Aliporudia Misri, Hassan Hossny Basha Alimzuru, Katibu maalum wa Mfalme Farouk, na alimwambia pongezi ya Mfalme kuhusu utafiti, bali pia alimwambia kwamba Mfalme alimkabidhi kumbukumbu ya Ottoman yaliyopo katika Ikulu ya Abdeen, ambayo ina nyaraka na jumbe zote zilizohusu mfereji wa Suez, tokea enzi ya Mohammed Ali na Mohammed Saed Basha na Khedive Ismael, akimtakia kuiangusha  Kampuni hii ya kikoloni.

2-Kuhusu serikali ya Misri, serikali ya Al-Wafd inayoongozwa na Mustafa Al-Nahhas Pasha, Mohamed Salah El-Din Pasha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri katika serikali ya aal-Wafd, aliandika utangulizi uliochapishwa wa utafiti wake ya Uzamivu kwa lugha ya Kifaransa, akisema. kwamba utafiti huo unaeleza msimamo rasmi wa serikali ya Misri. Kisha akaamuru barua hiyo ichapishwe kwa gharama ya Wizara na isambazwe kwa balozi zote za Misri zilizo ng’ambo.

3- Baada ya kuondolewa kwa serikali ya Al-Wafd, kufuatia moto wa Kairo, Ali Pasha Maher alishika kiti cha Udhibiti wa serikali, na kukutana na baba huyo ili kukubaliana naye juu ya kuanzishwa kwa Wizara maalum ya Mfereji wa Suez,  itakayofanya maandalizi ya kuurudisha tena, sawa iwe wakati kampuni ilitaifishwa au wakati mkataba ulipoisha.

4-kwa kufafanua:Talaat Basha Harb alikuwa wa kwanza aliyeita kwa utaifishaji wa Shirika la Suez Canal katika kitabu chake cha"Suez Canal" "kilichochapishwa mwaka wa 1910.

Ama siri ya kibinafsi ya Uadui wa Mfalme Farouk kwa Shirika ya Suez Canal,maelezo ya picha ya hali hii yametajwa katika kumbukumbu za Dkt.Mustafa Al-Hefnawy,ambapo alieleza malalamiko ya Mfalme wa Shirika hilo,kukataa kuwateua Karim Thabet na Andrws katika Uenyekiti wake.Hii ni pamoja na ukweli kadhaa ulioandikwa,kwa anataka kusema na kutambua ukweli wa historia,badala ya kukataa suala la utaifishaji bila ya kuelewa...

(Kutokana na makala niliyochapisha tangu miaka iliyopita).