Kumbukumbu ya Kifo cha Marehemu Rais Nataryamira

Kumbukumbu ya Kifo cha Marehemu Rais Nataryamira

Imefasiriwa na / Mervat Sakr

Cyprien Ntaryamira alikuwa mwanasiasa wa Burundi ambaye aliwahi kuwa Rais wa Burundi mnamo Februari 5, 1994 na alikuwa akijishughulisha na Harakati ya Wanafunzi wa Burundi,tena alishiriki katika kuanzisha kwa Chama cha Wafanyakazi wa Kisoshalisti cha Burundi. Ntaryamira alisaidia kuanzisha Chama cha Siasa cha Demokrasia, kilichopigania kufanikisha uchaguzi halisi wa kidemokrasia nchini Burundi mwaka 1993.

Alichaguliwa na Jumuiya ya kitaifa kuwa Rais wa Burundi. Akashika madarakani Februari 5, akitangaza kwamba vipaumbele vyake vya juu vitakuwa kurudisha Amani, kukuza haki za binadamu, kuwapa makazi wakimbizi, na alikuwa ametafuta bila mafanikio kupunguza migogoro ya kikabila.

Siku hii inaadhimisha kifo cha Rais Ntaryamera, nayo ni likizo rasmi inayoadhimishwa kila mwaka Aprili 6 katika Jamhuri ya Burundi kutokana na mafanikio yake makubwa ili kuendeleza Taifa la Burundi, liwe bora na siku hii inaadhimisha maisha ya Rais Cyprien Ntaryamira katika kumbukumbu ya kifo chake mwaka 1994.

Wakati uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia ulipofanyika Juni 1993, Melchoi Ndadaye akawa Rais lakini baada ya muda mfupi aliuawa miezi michache baadaye, kisha bunge la Burundi likamchagua Cyprien kuwa Rais mpya mapema mwaka 1994, lakini alifariki Dunia Aprili 6, 1994, ndege yake ilipoanguka wakati ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali nchini Rwanda na Rais wa Rwanda, na Juvénal Habyarimana  Rais wa Rwanda alikuwa naye na alifariki Dunia katika tukio hilo hilo.

Likizo hii nchini Burundi ni tukio rasmi sana. Ni Likizo ya umma, hivyo majengo ya serikali, shule na biashara hufungwa siku hii na kusherehekea kupitia sherehe na hotuba rasmi za viongozi wakuu serikalini.