Siku ya Mwalimu ya Kimataifa

Imetafsiriwa na/ Rahma Ragab
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled
Tukio hilo linakuja ili kufufua maadhimisho ya kupitishwa kwa hatua za kimsingi za upendekezo wa pamoja kati ya UNISCO na Shirika la Kazi la Kimataifa kuhusu masuala ya walimu yaliyofanyika mnamo Oktoba 5, 1966, Maadhimisho ya Siku ya Mwalimu ya Kimataifa yalianza tangu 1994 inayolenga kutia Mwangaza majukumu ya kimsingi ya walimu kwenye mipango ya kielimu na kujikita mafanikio yao, kutafuta njia za kuandaa walimu na kuwaajiri, pamoja na kuonesha umuhimu wa haraka na hitaji iliyo muhimu zaidi kutosheleza nafasi kwa walimu kushiriki kuunda maamuzi yanayohusiana na elimu, kuunga mkono walimu kwa namna kubwa ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu na kuainisha lengo la nne na linalotarajiwa kupatikana elimu mzuri, adili na kamili kwa wote na kuimarisha nafasi za kujifunza maishani mwote kwa wote.
Kwa msingi, mchakato wa kuimarisha taaluma ya ufundishaji na kuongeza kiwango cha elimu kunazingatia ongezeko la uwekezaji kwenye kusherehesha walimu ulimwenguni ambapo idadi yao ni walimu milioni 71, pamoja na kuboresha ufanisi wa mafunzo na kuendelea uwezo wao wa kitaalamu, kupanuza njia kwa vipaji vyao, kuandaa mahali pa kazi yao, na kuangalia changamoto zinazowakabili kwa lengo la kuziba mapengo na kufanya kazi kwa usimamizi mzuri wa mabadiliko yaliyotokea hivi karibuni kwenye uwanja wa elimu kutokana na janga la kimataifa, inawezekana hiyo kama shukurani kwa jukumu tukufu linalofanywa na mwalimu kwa binadamu na watu wote.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy